DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

Ingekuwa clouds ndio waliovamia kwa makonda saa hizi na hukumu ishatoka, alipwe fidia na kifungo juu, kamanda wa polisi kuwa na mipasho inatia kinyaa, anataka ushahidi gani zaidi ya ile clip ikimuonesha maknda akivamia hapo clouds na maaskari wake na mitutu?!
 
Nikimkumbuka al Akhiy Suleiman Kova, nilidhani hatatokea msanii wa aina yake. Ila nikimuangalia siro leo, nimebaki nacheka tu. Yaani aheri ya Kova.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.



Chanzo: mwananchi

Huu no upuuzi wa hali UA juu aama
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.



Chanzo: mwananchi

Huu ni upuzi wa hali ya juu sana, upelelezi upi kwa kwa jambo lililo wazi hivi
 
Kwani Clouds wao wametaka kumpeleka mtu mahakamani..? Nadhani kwao limeisha na wanachosisitiza wao ni wa Bashite kuomba radhi kwa tukio lile.. Sasa huyu Sirro hii ameitoa wapi..?
Uvamizi ni tukio la jinai. Na jinai iko chini ya mamlaka ya Police. Hivyo Clouds wanatakiwa watoe ushirikiano. Kama ni kuombana radhi kwa nini hawakuyamaliza nyuma ya pazia?
 
Ruge namkubali. Wape ushirikiano tu... maana ushahid unao mpaka zile cctv camera iliyoonyesha jamaa akingiia clouds na askari.
Hakuna cha kuficha..

And siro angalia rc anakuchafulia heshima yako mbele ya jamii. usoni unaonekana kuwa hupendezwi na hii hali lakin sababu ndio kibarua chako bas huna bud kufuata amri.

Mbona sasa Ruge anakimbia kutoa ushahidi?
 
Hakuna watu wanafiki kama mapolisi hawa jamaa hawajawahi kuwa serious na kazi yao, wiki mbili nilikuwa A..town kuna muuza mirungi maarufu sana alikuwa alifariki, huyu jamaa alikuwa "ANATAFUTWA" na polisi kwa kosa la kuuza madawa ya kulevya akawa amaejificha tu, alikuwa mgonjwa akafariki siku ya msiba maaskari ndio walikuwa wanatoka machozi kuliko majirani, tumeenda kumzika kwao njini masafara ukisimamishwa polisi wanauliza huu msafara ni wa marehemu fulani rafiki yangu? mkisema ndio basi gari haikaguliwi walikuwa wamemgeuza jamaa ATM, kwa hiyo huwa wanawajua wahalifu wanawapa taarifa zote za upelelezi, kusema wanahitaji upelelezi ni uongo tu kesi haigusiki wanaogopa.
 
Kila utawala na mambo yake sisi ni wapiga kelele tu na hakuna lolote tutaloweza Fanya mwenye dollar atabaki hivo basi
 
Dah! Sirro, hebu achana tu na hili suala, huna ubavu nalo, mhalifu yuko juu ya sheria nasi tunafahamu hilo na hakuna wa kukulaumu.
 
Maana hapa bashite lazima ahojiwe yeye ndio mtuhumiwa namba moja.
 
Huku uraiani huwa wanalazimisha kutafuta ushahidi na wanaupata ila kwa hao jamaa wanaombwa kupitia kwenye vyombo vya habari pasipo kufika directly kama mamlaka inayohusika na upepelezi wa kesi
No wonder kibiti kuna mushkeli!
 
Na lazima Ruge atoe ushirikiano hili jambo lieleweke vizuri na akijifanya kupuuzia mengi yanaweza kuibuka upande wa clouds na hasa Ruge.Namhurumia sana Kusaga kwani ni mtu muungwana sana na inawezekana amebebwa tu juujuu na Ruge katika hili swala.Wafanya kazi wa clouds nao wanachezeshwa ngoma ambayo hawaijui undani wake.Na mtaamini haya clouds itakapoanza kuporomoka down to ground level.
Mnataka muwageuzie kibao? Mtaumbuka wenyewe nawashauri muwe makini.
 
Afadhari ametoa ruksa kuoa WP woman polisi kuna Traffic mmoja pale kona ya Serena kibandani na sometimes huwa pale near Mahakamani ya kisutu, Mweusi kajazia vizuri mwili wake huwa natamani anisimamishe kwa ukaguzi ili nipate nafasi ya kumtongoza lakini hanisimamishi sijui ameshajua Dhamira yangu ila why anakwepa?
 
Nyie watu akili zenu zinasoma juu chini. Kesi ni ushahidi, malalamkijai anamnyima ushirikiano mpelelezi, ili mpelelezi apate facts/ushahidi wa kupeleka kesi kwa mwanasheria wa serikali hatimaye kesi ianze dhidi ya huyo anayedaiwa kuvamia. Sasa mnataka Sirro afanye nini?
ibambasi huwezi kutoa maoni bila matusi
 
Hivi hao Clouds tangu wamevamiwa kwanini hawaendi kushtaki polisi na kutoa ushirikiano kwenye UPELELEZI ??
Duh! Ulitaka wawe na ufunguo ndio ujue walienda kufungua hiyo kesi? Kama ni kuhusu kureport, waliliport ndio maana sirro leo katoka hadharani kusema watoe ushirikiano
 
Back
Top Bottom