DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

Sirro is looking for a grand excuse; nini maana ya hii kauli? Kwamba Clouds hawampi ushirikiano ndiyo maana mpaka sasa hajachukua hatua? Uvamizi wa Clouds media si ndiyo classic example ya zile kesi Rais aliyopata kuzungumzia kwa kusema hazihitaji hata upelelezi kwani mtu kakamatwa 'red-handed'? Sasa Sirro anaongea as if mpaka sasa hajachukua hatua kwa sababu hajapata ushahidi! Ni bora tu angenyamaza kuliko kutukebehi. Tunajua hawezi kuchukua hatua yoyote bila idhini ya wanasiasa. Si hata yeye mwenyewe amejidhalilisha kwa kutelekeza weledi wake kwenye maigizo ya vita vya dawa za kulevya? Watanzania wote siyo kondoo na mwenye macho huwa haambiwi tazama. Thir is a regime of double standards, period.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.

Chanzo: mwananchi

Kuna kitu hapa hakipo sawa

1: mtu wa kawaida hufanyiwa uchunguzi akiwa ndani(lockup) ila mkuu wa mkoa mtuhumiwa yupo nje na uchunguzi unaendelea

2: raia wa kawaida huitwa kituo cha polisi(akikubali bila shuruti) ama kupelekwa kwa lazima aki resist ila kwa mtuhumiwa huyu ni tofauti na hivyo

3: kamanda anasema anaomba ushirikiano kutoka kwa mlalamikaji(clouds media) lakini hajaomba ushirikiano kwa mtuhumiwa ina maana hana haitajiki katika kujiridhisha na uchunguzi wao,ushahidi utatimia vipi hapa??

hayo ni baadhi ya maswali yaliokuja kichwani baada ya kusoma tamko la kamanda
 
Jamani anayeuwa kwa upanga Naye atatendwa hivyo hivyo,muheshimiwa msipindishe ushahidu Nape alikabidhi ripoti lkn wahusika wameikanyagia chini,Siro Mungu anakuona IPO Siku hayo mambo yatakugeukia malipo ni hapa duniani huo ndio ushauri wangu......
 
Jamani anayeuwa kwa upanga Naye atatendwa hivyo hivyo,muheshimiwa msipindishe ushahidi Nape alikabidhi ripoti lkn wahusika wameikanyagia chini,Siro Mungu anakuona IPO Siku hayo mambo yatakugeukia malipo ni hapa duniani huo ndio ushauri wangu......
 
Clouds wauza nguna hao, wataifishwe tu na vongozi wao wachukuliwe hatua....hawa jamaa ni wauwaji ile mbaya, sina hamu nao na wala siwasikilizi.
 
Hivi hao Clouds tangu wamevamiwa kwanini hawaendi kushtaki polisi na kutoa ushirikiano kwenye UPELELEZI ??
Ndo nashangaa pia, najiuliza kama mie au wewe Mkaruka ungekuwa umevamia pale sidhani kama ungesalimika maana ungefunguliwa kesi ya uhaini
 
Ndo nashangaa pia, najiuliza kama mie au wewe Mkaruka ungekuwa umevamia pale sidhani kama ungesalimika maana ungefunguliwa kesi ya uhaini
Basi tushirikiane tu kushangaa mkuu, maana hata kama wana wasiwasi basi waitoe CCTV CLIP Nzima ya tukio la uvamizi kwenye public court - watu wajue mbivu na mbichi
 
Ingekuwa Lissu amevamia siku hiyo hiyo angeshafikisha mahakamani.
Huenda anafikiria endapo akiipeleka mahakamani halafu akakutane na Lissu kwenye hiyo kesi, sijui kitakachotokea.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.

Chanzo: mwananchi

Upelelezi !!! Upi huo utakao toa ushahidi wa kulidhisha kuliko ile video???
 
Kamanda Sirro ananitia mashaka sana jinsi anavyozijenga hoja zake inanifanya nimtilie mashaka ya kuwa ni mbaguzi wa kidini mfano ni pale alipomtaja kuwa huyu ni mpemba au pale aliposema alikua akitamka Allahu akibar hii yote yanitia mashaka sana
 
Siro mambo mengine jinyamazie kulliko kujiwekea mazingira ya kwenda ICC. Kilichomuua Mamba kilitoka kwenye mdomo wake!
 
Clouds waligoma kwa kuwa ilibidi kwanza wamuhoji guajimah,jamani hata kama nikupenda basi iwe kwa kiasi.to much power to the wrong hands
 
Back
Top Bottom