DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

Huku uraiani huwa wanalazimisha kutafuta ushahidi na wanaupata ila kwa hao jamaa wanaombwa kupitia kwenye vyombo vya habari pasipo kufika directly kama mamlaka inayohusika na upepelezi wa kesi
Hivi hao Clouds tangu wamevamiwa kwanini hawaendi kushtaki polisi na kutoa ushirikiano kwenye UPELELEZI ??
 
Wanapeleleza nn sasa......

Si watumie ile report ya nape inatosha mbona wanatifanya watanzania kama wajinga sana

Hiii ni dharau tena kubwa alafu eti mwanasheria atizame kama ata peleka kesi mahakamani au lah

Daaaah ina pain sana ila hakuna namna ndo nshazaliwa tz ntafanyaje ss
 
Siasa ni tamu sana ukiijua

Wazee wa system wameona issue ya Makonda inapoa wameenda kuipasha Moto ichemke Tena na kweli imechemka!

Niliwahi kuandika hii issue ya Bashite upande unaoshambuliwa ndio unaofaidika zaid
 
Sirro Mungu anakuona.

Watanzania sio watu wa kudanganywa na kufanyiwa maigizo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.

Chanzo: mwananchi
 
Ingekuwa Lissu amevamia siku hiyo hiyo angeshafikisha mahakamani.
Kila mtu na nyota yake, Lisu upelelezi wake upo tayari robo tatu automatcally, akitenda kosa ni kukamilisha tu robo iliyobaki.
 
Ngoja nisichangie kitu chochote zaidi ya hiki nilichochangia
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hivi hao Clouds tangu wamevamiwa kwanini hawaendi kushtaki polisi na kutoa ushirikiano kwenye UPELELEZI ??
Mpaka anasema upelelezi unaendeleaje maana yake kumbe tayari clouds walisharipoti!
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.

Chanzo: mwananchi
Siro kama mke wa Mzee Malecela alifukuzwa kazi kwa kosa ambalo aliletewa na watendaji, Kitwanga hakupimwa ulevi akamfukuza, huyu akavamia clouds akaambiwa chapa kazi, kweli una haja ya kumsumbuka na upelelezi?
 
Back
Top Bottom