DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

DAR: Kamanda Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

intellejensia ya polis embu mufanye mambo mengine ya maana hasa suala la mauaji Kibiti....Ukachelo wenu unaonekana kwenye mikutano ya wapinzani tu mambo mengine intellejinsia yenu hatuielewi.
 
Sirro anawatafutia nini Clouds? Si awaache? Wao walisema wanataka kuombwa msamaha hawataki kesi wala kumshitaki Bashite, yeye anawalizimisha kwa nini ? Kama Bashite Anaona hana kosa si basi wakae kimya
 
Hivi jamani haya mambo ya Bashite si yalishaisha? naona yanarudi kwa kasi...kulikoni tena?
mwenyewe hawezi kuishi bila kiki hata kama ni kunywa maji ya mvua yaliyotuama kwenye dimbwi!
 
Sirro anawatafutia nini Clouds? Si awaache? Wao walisema wanataka kuombwa msamaha hawataki kesi wala kumshitaki Bashite, yeye anawalizimisha kwa nini ? Kama Bashite Anaona hana kosa si basi wakae kimya
Umeonaee maana maumivu ya Karusha live Dar mpya hayajaisha...
 
Uvamizi ni tukio la jinai. Na jinai iko chini ya mamlaka ya Police. Hivyo Clouds wanatakiwa watoe ushirikiano. Kama ni kuombana radhi kwa nini hawakuyamaliza nyuma ya pazia?
Matukio mangapi ya jinai yanayomalizika nje ya mamlaka ya Polisi..? Utamlazimisha victim akatoe taarifa polisi hata kama yeye ameamua kusamehe..? Halafu toka siku ya kwanza Clouds hawakuwa na nia ya kuendelea na hii kadhia.. Nashangaa tuu Sirro kuibuka nalo leo.. Kama hana kazi aende akasaidiane na Polisi wengine kibiti huko..
 
Aibu sana,mkubwa tena mwenye familia kuwa mtumwa wa mwingine
 
Matukio mangapi ya jinai yanayomalizika nje ya mamlaka ya Polisi..? Utamlazimisha victim akatoe taarifa polisi hata kama yeye ameamua kusamehe..? Halafu toka siku ya kwanza Clouds hawakuwa na nia ya kuendelea na hii kadhia.. Nashangaa tuu Sirro kuibuka nalo leo.. Kama hana kazi aende akasaidiane na Polisi wengine kibiti huko..
Kama hawakuwa na nia kwa nini walisambaza taarifa?
 
Wanapeleleza nn sasa......

Si watumie ile report ya nape inatosha mbona wanatifanya watanzania kama wajinga sana

Hiii ni dharau tena kubwa alafu eti mwanasheria atizame kama ata peleka kesi mahakamani au lah

Daaaah ina pain sana ila hakuna namna ndo nshazaliwa tz ntafanyaje ss
Ndio hivyo tena. Ushazaliwa Bongo. Nchi ile ni bongolala.
 
Ukiwa mtumwa wa wanasiasa wanakugeuza mbwa wao na wanakufanya watakavyo. Ni mbaya sana unaburuzwa na jinga la std 7 wakati una shahada tena ya sheria.
 
Ingekuwa uvamizi huo umefanywa na kiongozi wa upinzani, angekuwa ashafungwa toka siku ile ile ya uvamizi bila hata kusikilizwa mahakamani. Sirro naye vyeti vyake vihakikiwe.
Lakini kutoa malalamiko polisi sio automatically ndio umefungua kesi. Phase 1. Wamewasilisha malalamiko Yao. Phase 2,wanatakiwa kutoa maelezo na vielelezo vya kujitosheleza kuhusu kuvamiwa. Unajua mtu kuonekana kwenye video anaingia na kutokea kwenye jengo sio necessary awe kavamia. Clouds wenyewe walisema jamaa Alikuwa anatia team kwao mara nyingi, sasa Kuna ushahidi gani kuwa clips zile ni uvamizi na sio tríp zake za kawaida hapo clouds ?
Mi Naona hamna shida clouds waende kutoa ushahidi kwa kadri watakavyoitwa
 
Hujue bhana hata kama mtoto mdogo una mdharau inafika mda unamwambia ukweli Kuna usemi anasema mrisho mpoto vitu vya kitoto mtoto kumwambia mtoto mwenzie tunasema wanacheza lakin kitu cha kitoto MTU mzima kumwambia MTU mzima mwenzie kuna walakin siku zote kamanda siro kamsubir jamaa akahiojiwe ndo atoe tamko au clouds malalamishi wameyapeleka Leo anataka kuongeza chumvi baharin kwa kutia kijiko kimoja Naamin Ccm wote wanavyet fek
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amewataka uongozi wa Clouds Media Group kushirikiana na jeshi la polisi katika upelelezi wa tukio la uvamizi wa kituo chao cha matangazo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Sirro amesema kesi yoyote inahitaji ushahidi na uvamizi wa Clouds bado upelelezi wake unaendelea ukikamilika utapelekwa kwa wakili wa Serikali ili aone kama anaipeleka kesi hiyo mahakamani au kutoipeleka.

"Ndugu zetu wa Clouds watoe ushirikiano kwa mpelelezi wa kesi yao, wao wanataarifa za kutusaidia kukamilika kwa upelelezi ila nasi tuweze kuipeleka katika hatua inayofuata. Na sio kwamba tukio limesahaurika bali upelezi wake unaendelea," amesema Sirro.



Chanzo: mwananchi

Kweli ukiajiriwa na jpm,lazima ujitoe ufahamu,hivi kweli siro unaubavu wa kumchunguza makonda,nape ametumbuliwa hadharani kwa sababu ya bashite,wewe umetumwa
 
Back
Top Bottom