Nashawishika kuamini kuwa ajali ya gari iliyowahi kumpata Mama Helen Kijo-Bisimba na hii ya sasa iliyomfika Mwandishi Maarufu Jenerali Twaha Ulimwengu siyo ajali za bahati mbaya - kwa kadri ya mazingira zilivyotokea.
Ajali ya Dr.Bisimba iliyotokea tar.8/11/2015, siku 3 tu baada ya Magufuli kuapishwa kuwa Rais, kwa maoni yangu ililenga kuwaziba LHRC wasikosoe namna Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ulivyoendeshwa. Tukumbuke kuwa siku chache tu kabla Tume hawajatangaza matokeo yao, polisi walikuwa wamevamia Makao Makuu ya LHRC na kubeba computer zote, na kuwakamata wafanyakazi wa kituo hicho.
View attachment 388297
Baada ya Mama Bisimba, sasa ajali amepelekewa Jenerali Ulimwengu, na huyu kuna kila dalili kuwa ilikuwa 'aondolewe' kabisa maana gari yake imeogongwa upande wa dereva. Hii imetokea siku chache tu baada ya Jenerali kumkosoa Magufuli namna anavyoendesha nchi.Kwa kuwa taarifa zilizopo ni kuwa ameumia sana kichwani, tunamwombea Mwenyezi Mungu amponye na amwepushe na mauti.
View attachment 388302
MUNGU ATUEPUSHE NA MABAYA YOTE YA UTAWALA HUU, NA ATUSAIDIE KUWAADHIBU WATESI WETU! AMEN.
Mmmmmmmmmmmmmmhhhhh