DAR: Jenerali Ulimwengu apata ajali, alazwa Muhimbili

DAR: Jenerali Ulimwengu apata ajali, alazwa Muhimbili

Mwanahabari, Mwandishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Raia Mwema Jenerali Ulimwengu amepata ajali Dar es Salaam asubuhi mapema leo.

Yupo hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.

Tutaendelea kuwaletea taarifa.

Mwanahabari HuruView attachment 388029

View attachment 388027

Pole sana Jenerali hope Mungu atakujalia kupona haraka na afya njema. STAY BLESSED
 
Pole sana General wa watanzania.Munguba akulinde kwa hili na lengine.Get well soon
 
Pole yake, hiyo ajali ilitokeaje?

Get well soon Jenerali
 
Kwani hiyo picha unayoiona unafikiri ni gari gani? au umekaririr benzi lazima liwe kama teksi?

Soma nilicho andika, usitake kulazimisha mambo - yaani kwa akili zako unafikiri Ulimwengu anaweza kuendesha gari aina ya kill the driver save the engine!!!
 
Mbona umekomalia suala hili, shida yako nini?? unataka kusingizia watu kwa ajali ya kawaida!!!
Kwani anayesababisha ajali ni nani? si ni mtu huyo huyo, nilichokosea ni wapi kusema ni man made?

Ha ha unafeli kaka, haitaji hasira.
 
Mwanaharakati ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu amelazwa katika Taasisi ya Upasuaji wa Mifupa (MOI), baada ya kuokotwa na wasamaria wema eneo la ubalozi wa Ufaransa, Masaki, usiku wa kuamkia leo akiwa hajitambui baada ya kupata ajali ya gari.

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Uhusiano wa MOI Patrick Mvungi alisema wamempokea Ulimwengu akiwa ametokea katika kitengo cha dharura hospitali ya taifa Muhimbili na kumfanyia vipimo mbalimbali mchana wa leo.

“Tumempokea akitokea kitengo cha dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hapa kwetu amekuja kwa dharura, tumefanikiwa kumfanyia vipimo kadhaa na sasa amelazwa wodini. Tatizo kubwa alilolipata ni kuumia kichwani,” alisema Mvungi.

Chanzo:Mwananchi
 
Nashawishika kuamini kuwa ajali ya gari iliyowahi kumpata Mama Helen Kijo-Bisimba na hii ya sasa iliyomfika Mwandishi Maarufu Jenerali Twaha Ulimwengu siyo ajali za bahati mbaya - kwa kadri ya mazingira zilivyotokea.

Ajali ya Dr.Bisimba iliyotokea tar.8/11/2015, siku 3 tu baada ya Magufuli kuapishwa kuwa Rais, kwa maoni yangu ililenga kuwaziba LHRC wasikosoe namna Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ulivyoendeshwa. Tukumbuke kuwa siku chache tu kabla Tume hawajatangaza matokeo yao, polisi walikuwa wamevamia Makao Makuu ya LHRC na kubeba computer zote, na kuwakamata wafanyakazi wa kituo hicho.
Dr Bisimba.jpg

Baada ya Mama Bisimba, sasa ajali amepelekewa Jenerali Ulimwengu, na huyu kuna kila dalili kuwa ilikuwa 'aondolewe' kabisa maana gari yake imeogongwa upande wa dereva. Hii imetokea siku chache tu baada ya Jenerali kumkosoa Magufuli namna anavyoendesha nchi.Kwa kuwa taarifa zilizopo ni kuwa ameumia sana kichwani, tunamwombea Mwenyezi Mungu amponye na amwepushe na mauti.

Jenerali.jpg


MUNGU ATUEPUSHE NA MABAYA YOTE YA UTAWALA HUU, NA ATUSAIDIE KUWAADHIBU WATESI WETU! AMEN.
 
Back
Top Bottom