A
Anonymous
Guest
Hali ya barabara katika mitaa yetu ya TABATA (NSSF) sasa imefika hatua ambayo si kero tena, bali ni janga la miundombinu linalohatarisha usalama, afya, na uchumi wa kila mkazi. Kama picha zinavyoonyesha, barabara ambazo ilipaswa kuwa kiunganishi cha familia zetu zimegeuka kuwa mashimo ya maji, mifereji ya matope, na madimbwi yasiyopitika. Uozo huu ni kioo cha kusahaulika kwa makusudi na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na upuuzaji wa sheria za mipango miji unaofanywa na mamlaka za mitaa.
Uharibifu huu wa barabara ni tishio la moja kwa moja kwa afya zetu. Madimbwi yaliyojaa maji taka katikati ya barabara yamegeuka kuwa mazalia ya mbu na vyanzo vya magonjwa ya mlipuko, jambo ambalo ni hatari kwa watoto na afya kwa ujumla. Aidha, mzigo wa kiuchumi kwa wakazi unaongezeka kila uchao. Wamiliki wa vyombo vya moto wanalazimika kutumia sehemu kubwa ya kipato chao kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya garage kutengeneza matairi, na rim zilizopata hitilafu, gharama ambazo tunatwishwa kutokana na kushindwa kwa serikali kulinda na kukarabati mali za umma.
Hata hivyo, ni lazima tuseme ukweli: barabara hizi hazijaharibika kwa bahati mbaya, bali ni kutokana na kuruhusiwa kwa malori makubwa kuingia na kufanya kazi kwenye mitaa ya watu. Barabara hizi zimejengwa kwa ajili ya magari madogo ya nyumbani, si kwa ajili ya uzito wa tani kumi au ishirini za malori ya mizigo. Kwa kuruhusu malori haya kupita katikati ya makazi, mamlaka husika zinabariki uharibifu wa lami na udongo ambao haukuwa na uwezo wa kubeba uzito huo. Tunahoji: Kwa nini malori haya yanaruhusiwa kuacha barabara kuu na kuingia kuharibu misingi ya nyumba na barabara zetu?
Jambo la kusikitisha zaidi ni uvamizi wa maeneo ya wazi (Open Spaces). Katika mipango miji, maeneo haya ni mapafu ya mtaa; ni sehemu za michezo ya watoto, mikutano ya kijamii, na njia za asili za kupitisha maji ya mvua. Badala yake, maeneo haya yamegeuzwa kuwa karakana na maegesho ya kudumu ya malori makubwa. Ikumbukwe kulikuwa na viwanja vikubwa vilwili tulivyotumia wakati tunakua kwa ajili ya michezo na mikutano. Huu ni wizi wa ardhi ya umma na ukiukaji wa sheria za ardhi. Inajenga mazingira ya hatari ambapo watoto wetu wanalazimika kucheza pembeni ya mitambo mikubwa, huku kukosekana kwa mifereji kwenye maeneo hayo kulikosababishwa na ujenzi holela wa "yard" za malori kukiongeza mafuriko mitaani.
Sisi kama wakazi, tunatoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka. TARURA na mamlaka zote zinazohusika lazima itoe mpango wa wazi wa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha kudumu, ikiwemo mifereji ya maji. Vilevile, tunaitaka Halmashauri ya Manispaa na Jeshi la Polisi kuweka zuio kali la uzito wa magari yanayoingia mitaani na kuyaondoa malori yote yaliyopaki kwenye maeneo ya wazi kinyume cha sheria. Hatuombi upendeleo; tunadai haki yetu ya msingi ya kuwa na miundombinu bora na usalama kama walipa kodi. Wakati wa kukaa kimya umepita, tunataka hatua zionekane sasa!