Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

Baba yangu Mkubwa Anaish Dar mwaka wa 28 huu ndo msomi zaid na mwenye kipato kikubwa zaid ndan ya familia ila ndo maskn zaid kwenye familia yao.

Sitak kuweka maelezo meng Jitahd hvyo hvyo tu unielewe
Cha ajabu utakuta ndo aliyewasomesha na kuwawezesha kupata hayo mafanikio lakini hamkumbuki yote na mnamwona boya

Omba uwe na ndugu anayetambua mchango wako katika maisha yake yaani we acha tu
 
lile tu joto kwangu huwa naona kama nipo ahela,yaani joto kulidhibiti unatumia gharama?
Mie home ni Dar na kuna mijengo na ma kila kitu babaake ila sitamani hata kurudi. Niko maeneo ya karibia na mlima mkubwa Africa, hali ya hewa safi hamna kero ya usafiri vyakula cheap, nikiwaza lile joto la bongo unalala na feni still unavuja jasho. Sitamani hata kurudi bongo mazee!
 
Ninyi nyote kwa kifupi mawazo yenu ni finyu na uwezo wa kutoka ndani ya kundi la wajanja hamuwez, kwa kifupi mnarudi kwenye ule msemo wa kizamani kwamba jogoo wa shamba.....niwaulize mnawaza habari ya eti kodi ya nyumba, chakula maji, kwa hio huko mikoani kuna nyumba za bure? Kama kamji kadogo namna hii mnaona ni kupoteza muda inakuwaje ungetupwa jiji kama NY, Milan ama London ukaambiwa utafute connection mtoboe? Wasema Dar ni kupoteza muda lakini tambua nyumba nzuri kushinda zoote Tanzania iko Dar, viwanja vikal viko Dar, Tajiri namba 1 Tanzania yuko Dar, hata gari ya kifahari nchi nzima inaendeshwa Dar..nyie endeleeni kukusanya matembele huko na kujigamba mnamilik nyumba huko ambayo ukiileta dar itathaminishwa na ilioko tandale

Wapi nimesema mkoani kuna maisha mazuri mkuu?
Nilichosema ni kuwa mkoani ni rahisi kutoka kuliko dar , baas !!! Hakuna sehemu yoyote ambayo nimesema maisha ya dar ni mabaya , Nilichosema ni kuwa najutia muda niliopoteza kuishi dar
Umeamua kunitafrisi unavyotaka wewe na kujenga hoja kutokana na tafsiri yako, Again typical mindset ya sie watu wa dar !
Sio kila mtu atakubaliana na wewe. FYI im not your typical Dar dweller. Kwahio hio typical mindset yako ni wewe na wenzio hainihusu ndio maana mawazo yako na yangu yanapishana.
 
Basi heri mkuu
Karibu supu
IMG_20180919_085251.jpg
 
Mtoa mada alitakiwa aseme baadhi ya mikoa kutoboa ni rahisi kuliko Dsm mana ipo mikoa maisha ghali sana kuliko Dsm hasa ukiwa unafanya kazi rasmi pia ubaguzi na changamoto nyingi ukiingia kwenye uwekezaji kuliko Dsm

Kwenye mifano mizuri hapo ni k'njaro+Arusha kama wewe sio Mangi flani hivi/haupo kwny system flan flan hivi jiandae kupambana na dhoruba kama unataka kuwekeza.
 
Yeah na wanawake wadangaji wanapapenda kwa sababu ya watu wenye vipato vikubwa excess wapo hapo.
Mi sikufichi, Dar kwa hali ya sasa kama huna kipato cha elfu 80 mpaka laki kwa siku utapaona pachungu hasa kama unapenda kuishi comfortably, uendeshe gari na home familia ile vizuri, ule bata bila kusahau ku save kwa ajili ya maendeleo! Gharama za maisha ni kubwa sana.
Comfortability ya maisha ya mtu anaeingiza laki kwa siku Dar ni sawa na ya mtu anaeingiza elfu hamsini kwa siku kwa mikoa mingi tofauti na Dar.
Huyo anaeingiza elfu hamsini kwa siku huyo si tajiri wa kutupwa.ndani ya wiki atakuwa kama na laki 3.kwa mikoani huyo anamaliza yote.tajiri namba 1 wa mji mzima.kiufupi maisha yawe ya mikoani au Dar. Ukiingiza 15 kwa siku wewe umetoka kimaisha.wengi huwa wanaishia kupata buku 5 siku ikiwa powa buku 10 kwa siku.Ukipiga dili ukalipwa 15000 au 20000 yani siku hiyo utachoka balaaa ni kazi ngumu sana.Kiufupi Tanzania yote maisha ni magumu sana.Labda uishi kijijini kabisa.Huko kuna angalau na ukiwa kijijini ukubali kuishi maisha ya ukijijini.Maisha yetu watanzania yanasikitisha sana hasa vijijini.Nimekaa morogoro.Mbeya,Dar,Songwe nimepita Njombe ,Iringa,pwani.Kwa kweli maisha ni duni sana. Yani tunaishi kwa neema tu.Dar kuna wabongo wachache wenye pesa.Ila sio pesa nyingi.Wanahela sana wenyenyumba za kupangisha Dar.Maana kodi wanakusanya kwa miezi 6.labda unakuta chumba 50,000.amepangisha vyumba nane anakuwa na million kadhaa ambazo zinasaidia kumtoa kimaisha.
 
Yeah kichwa lazima kiume ukikatisha usingizi, ina maana ulikuwa unalala masaa 5 tu badala ya atleast 7 ambayo ndio recommeded kwa afya!

Na hapo bado sijapita kwny vikao vya pombe vya kurudi home saa 8 usiku,maisha si lelemama.
 
Dar ina wenyewe. Dar ni bongo hata mwanzoni jina bongo lilihusu watu wa Dar tu japo sasa ni tz nzima.
Uamuzi wa kurudi ni mzuri sana na wengine watabaki.
Hivi mtu anayemiliki nyumba Dar na mwingine Kishapu tofauti ni nini. Au Nairobi na Kericho. Wazo lako ni zuri
 
Huyo anaeingiza elfu hamsini kwa siku huyo si tajiri wa kutupwa.ndani ya wiki atakuwa kama na laki 3.kwa mikoani huyo anamaliza yote.tajiri namba 1 wa mji mzima.kiufupi maisha yawe ya mikoani au Dar. Ukiingiza 15 kwa siku wewe umetoka kimaisha.wengi huwa wanaishia kupata buku 5 siku ikiwa powa buku 10 kwa siku.Ukipiga dili ukalipwa 15000 au 20000 yani siku hiyo utachoka balaaa ni kazi ngumu sana.Kiufupi Tanzania yote maisha ni magumu sana.Labda uishi kijijini kabisa.Huko kuna angalau na ukiwa kijijini ukubali kuishi maisha ya ukijijini.Maisha yetu watanzania yanasikitisha sana hasa vijijini.Nimekaa morogoro.Mbeya,Dar,Songwe nimepita Njombe ,Iringa,pwani.Kwa kweli maisha ni duni sana. Yani tunaishi kwa neema tu.Dar kuna wabongo wachache wenye pesa.Ila sio pesa nyingi.Wanahela sana wenyenyumba za kupangisha Dar.Maana kodi wanakusanya kwa miezi 6.labda unakuta chumba 50,000.amepangisha vyumba nane anakuwa na million kadhaa ambazo zinasaidia kumtoa kimaisha.

15,000 per day kwa dar na 15,000 per day ya huko katavi/bariadi/mtwara/lindi/ ni mbingu na ardhi,cheki yo' facts again boss.
 
Hii thread niliiona tangu jana nikaibeza kumbe imejaa ujumbe kamili.

Hili jambo nimelishuhudia kwa watu kibao sana. Wamekaa Dsm lakini hakuna cha maana wanachorudi nacho zaidi ya Nguo na simu na mademu tu.

Ila wakija mkoani wanatusua tena kwa muda mfupi tu.
Huu ni mrejesho mtamu kwa mtoa mada.
 
Na hapo bado sijapita kwny vikao vya pombe vya kurudi home saa 8 usiku,maisha si lelemama.
Hahah ila mi naona Dar nzuri kwa biashara kuliko ajira ila uwe umeinvest pesa ndefu. Sio biashara za kuchonga miwa na kuuza pipi.
Kwa ajira ukipata unayokunja at least 2 to 3m kama take home ndio utainjoy life la mjini. Ila kinyume na hapo ni shida tu mzee baba!
 
Cha ajabu utakuta ndo aliyewasomesha na kuwawezesha kupata hayo mafanikio lakini hamkumbuki yote na mnamwona boya

Omba uwe na ndugu anayetambua mchango wako katika maisha yake yaani we acha tu
Ndugu ulichoandka kimejaa assumptions labda na refference to your own life,nikikuambia uthbitshe ulichokiandka kutoka kwenye ulichoquote hutaweza, comment yang haipo positive wala negative na ndo mana mwisho nikasisitiza jitahd unielewe, sasa mwenzangu na mimi ukaelewa kwenye negatv tu. ila sio tabu una uhuru wa chochote ndugu and its "where we dare to talk openly"
 
Back
Top Bottom