Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
 
1. Dar kwa kijana ambaye ni jobless ni ngumu sana kujitegemea.

2. vijana wengi wazaliwa wa Dar hawawezi/hawapendi kwenda mikoani kuanza maisha huko, wanaamini watafanikiwa palepale Dar.

3. wataendelea kuwa tegemezi hadi siku watakapoamua kuondoka Dar na kwenda mikoani kuanza kutafuta maisha ya kujitegemea huko.
 
Kweli ndivyo ilivyo, ila hii inachangiwa na kitu kimoja....
Vijana wa mikoani wamezoea hustle na kuna umri ukifika wao husema wanaenda kutafuta maisha hivyo huamia mikoa na kujikuta wanaondoka nyumbani rasmi, Kwa Dar iko tofauti unatokaje Dar unaenda kutafuta maisha mkoani?
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Na wanaojenga dar es salaam asilimia kubwa ni watu kuja .
 
Back
Top Bottom