Dar: Halima Mdee kulala Korokoroni Polisi hadi jumanne

Dar: Halima Mdee kulala Korokoroni Polisi hadi jumanne

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
693
Reaction score
889
Jeshi la Polisi limekiri kumshikilia Mbunge wa Kawe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Halima Mdee baada ya kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar leo Jumamosi, Novemba 16.

Mkuu wa Kituo hicho amesema wamemshikilia na watampeleka Mahakamani Jumanne wiki ijayo.

MY TAKE:

Kama Mahakama imeagiza akamatwe, wamkamate na kumpeleka kwa Mhimili uliomujitaji. Unashikilia wa kazi gani. Hii ni chuki ya Wazi ya vyombo vya Dola kukumoa Viongozi na Wanachama wanaopinga maovu na unyonyaji wa CCM. Yaani Polisi wanakuwa wanawinda Viongozi wa Vyama vya Upinzani wanakosa sababu ya kuwakamata, so wakipata nafasi, wanataka wamalizie hapo Hasira zao.

Wanaamini kama watawanyanyasa Upinzani basi wanaweza andishwa vyeo. Na kutaka cheo.


=========

[https://res]

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Oysterbay, kwa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Novemba 2019 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mdee anashikiliwa baada ya kujisalimisha kituoni hapo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mdee alikwenda katika kituo cha polisi cha Oysterbay, kwa ajili ya kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RCO).

Hata hivyo, Polisi wamesema watamshikilia Mdee hadi Jumanne ijayo ya tarehe 19 Novemba 2019, watakapomfikisha mahakamani.

Jana tarehe 15 Novemba 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliamuru Mdee pamoja na wabunge wengine watatu wa Chadema, kukamatwa kutokana na kushindwa kufika mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, bila ya kutoa taarifa.

Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Wabunge wengine ambao mahakama imeamuru wakamatwe ni Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini.
 
FB_IMG_1570952637609.jpg
 
Ninaipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya mtukufu Dr.Pombe kwa kuendelea kukamata kamata wapinzani wake.
safi sana mheshimiwa endelea kuwatesa wapinzani .
Inabidi bunge litoe azimioi la kupongeza na hili.
 
Back
Top Bottom