Dar: Halima Mdee afikishwa Mahakamani Kisutu, apewa dhamana

Dar: Halima Mdee afikishwa Mahakamani Kisutu, apewa dhamana

Halima Mdee aliyekaa akisalimiana na Esther Bulaya

Mbunge wa Kawe Halima Mdee, hatimaye amefikishwa Mahakamani Kisutu Dar es Salaam.

Bado sijajua atashitakiwa kwa makosa yapi kwani ndo yupo Kisutu.

Hapo awali Mdee aliwekwa Korokoroni Oysterbay Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi. Hata baada ya Masaa 48 kuisha, hakuachiliwa huru kwani aliendelea kushikiliwa.

Halima Mdee(Mb, CHADEMA) akamatwa na Polisi. Apelekwa Oysterbay...

Stay tuned..

UPDATES:

"Mdee alitoa lugha ya matusi na maudhi kwa kiongozi wa nchi, tulimuhoji na baada ya mahojiano tumemfikisha Mahakamani."- Kamanda Mkondya

"Mhe. Halima mdee tulimkamata maeneo ya Ubungo kwa sababu alikua na kikao na waandishi wa habari akipinga maamuzi ya Rais"- Kamanda Mkondya
---------------

UPDATE: 10, JULAI, 2017

Mbunge Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili. Ushahidi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi August 7, 2017.
Mimi nadhani mahakama ina majukumu makubwa zaudi kuliki hizi fabricated cases...
Watu wako mahabusu zaidi ya miezi kwa visingizio tofauti bado mna pika kesi nyingine

Sent from my Phantom6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwanini mara kwa mara hawa watu wawili hawakosekani kwenye matukio; Mdee na Bulaya. Kila anapokuwepo mdee lazima utamkuta bulaya. wapo karibu sana inaelekea.
Kwani kuna ubaya mkuu?
 
Mithali 21: 3; ''Kutenda haki na hukumu humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka.''
 
Hivi kwanini mara kwa mara hawa watu wawili hawakosekani kwenye matukio; Mdee na Bulaya. Kila anapokuwepo mdee lazima utamkuta bulaya. wapo karibu sana inaelekea.
Nayo mwataka iwe kesi?

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
kwa kwa mamlaka za hovyo zinadai heshima kwa nguvu mamlaka zenye nidhamu zenye kujenga nchi na utawala bora hazingoji kuweka watu ndani ndio ziheshimike au kuuwa watu na kuwachomeka vitu vigumu kweny malinda yao upuuzi mtu atakaye kufa nakufunikwa kiloalfu za mchanga kujigeuza miungu kisa madaraka ni ajabu . acheni upuuzi wa kufanya nchi hii ni yenu peke yenu akili ya hovyo kabisa utawala mbovu unaokusanya bilioni 700 baada ya miaka miwili upewe heshima gani sijui
Povu jingi,with no substance.Hata hivyo ni vizuri watu wakakumbuka kwamba uchaguzi umekwisha na mwingine ni 2020.Tusubiri.Hakuna sababu ya kuendelea kusigana na mamlaka iliyopo.
 
Kukosoa ukosoaji ufanyike lakini lazma taasisi ya Urais iheshimike tusishabikie kila kitu kisa tu kimefanywa na mpinzani. ...Mamlaka hutoka kwa Mungu bila Mungu kupanga hakuna litakalowezekana hivyo lazima mamlaka iheshimiwe....Rais anastaili kuheshimiwa na kukosolewa kwa lugha inayofaa si ya kejeli na matusi.
 
Kabisa kabisa. Yoyote atakayejifanya mabangi kama Mdee hakuna jinsi akanyee debe tu
 
Back
Top Bottom