Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,419
- 3,627
Wakuu
Kama muonavyo picha
Mwanasiasa mkongwe, Wilbroad Slaa (76) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa X (zamani twitter).
Dk Slaa amefikishwa mahakamani hapo leo Januari 10, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.
Mapema leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kumshikilia Dk Slaa.
"Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye," - Kamanda Muliro.
Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.
Soma:
- Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni
- Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria