Dar: Hafla ya BAWACHA Mikocheni yazingirwa na Polisi, wapewa dakika 30 tu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,112
Hii ni baada ya Polisi kuruhusu Bawacha wakutane kwa dk 30 tu huku polisi nao wakitaka kuwemo ndani ya ukumbi ili kusikia yanayozungumzwa , kabla ya ruhusa hiyo zimepigwa danadana kuanzia polisi kinondoni , DC hadi RC wakipiga danadana huku kila mmoja akijitoa asionekane kuruhusu jambo hilo .

Ikumbukwe kwamba BAWACHA waliandaa hafla yao ya halali Mikocheni na kupeleka taarifa kwa DED kama sheria zinavyoelekeza , jambo ambalo limeiogopesha Mamlaka ya Tanzania .

Bawacha wamegoma kuendesha kongamano lao chini ya pingu za polisi .

Malisa_GJ_on_Instagram:_“Jana_Lissu_alisema_Mwendazake_amekufa_lakini_waliokua_wakimsaidia_kut...jpg



UPDATES
============

Video : Mwamba Mbowe awasili kwenye hafla hiyo huku akipenya katikati ya mitutu ya bunduki

 
Jana Lissu alisema Mwendazake amekufa lakini waliokua wakimsaidia kutesa na kuumiza watu hawajafa. Bado wapo. Wanaweza kuwa wameficha makucha tu kwa muda lakini wakishamsoma mama, watarudi tu.

Na hiki ndicho kilichotokea. Polisi wenye silaha wamezingira ukumbi wa Hekima Garden, Mikocheni kuzuia hafla ya chakula cha jioni iliyoandiwa na Baraza la wanawake la Chadema (BAWACHA).

Iko hivi, Bawacha wameandaa hafla ya kuwakutanisha wanawake wa Chadema kubadilishana mawazo na kuzungumza mambo yao kama akina mama.

Wakaandika barua kwa Mkurugenzi kumpa taarifa. Lakini Mkurugenzi akasema wapeleke maombi yao kwa DC. Wakapeleka barua kwa DC Gondwe. Katika hali ya kushangaza Gondwe eti nae akaagiza barua ipelekwe kwa RC. Yani danadana zisizo na ulazima wowote. Yani akina mama kukaa na kula kuku zao hadi RC atoe ruhusa?

Anyway, barua ikapelekwa kwa RC lakini Makalla akaingia mitini. Hataki kujibu. Baada ya kusumbuliwa sana akaagiza waende kwa RPC Kinondoni. RPC kaagiza waende kwa OCD Oysterbay. OCD akaruhusu hafla ifanyike kwa masharti yafuatayo;

1. Pasiwepo na mziki.
2. Pasiwepo na pombe.
3. Hafla ifanyike kwa dakika 30 tu.
4. Askari waingie ukumbini kusikiliza wanachojadili.
5. Wakimaliza kula watawanyike haraka.

Wanawake wa BAWACHA wamegomea masharti hayo, wanataka wawe huru kufanya mambo yao.

#MyTake;
Mama kemea hawa watu watakuharibia sasa hivi. Hawa akina mama ni wanawake wenzako. Wameamua kukaa, kula na kujadili mambo yao. Kwanini wananyanyaswa? Mwendazake aliwabagua watu kwa vyama vyao. Wapinzani wakawa mistreated kama vile magaidi. Wakapigwa, wakateswa na kunyanyaswa bila sababu.

Wewe ulianza vizuri kwa kuliunganisha taifa. Ukaahidi kuganga makovu yetu. Ukasema tusahau yaliyopita na tufute machozi. Lakini badala ya kutufuta machozi, mbona watu wako wameanza kutuletea machozi tena? Tafadhali wakemee. Jana tumefanya kongamano zuri la Katiba, na dunia imekupongeza kwa sababu polisi hawakutusumbua. Lakini leo hawa akina mama wanasumbuliwa? What happened?
 
Wazee wa SIASA za matukio tena.

Kuna wakati mnawalaumu tu POLISI.

Kuna kitu leo nishee hapa.

Hivi mnajua kuwa KUIJENGA NCHI NA KUISIMAMISHA NI KAZI SANA ZAIDI YA KUIBOMOA?!!!

Nchi inasimamiwa na Serikali iliyoko madarakani.

Na Serikali yoyote ile duniani Ni lazima IOGOPE machafuko/mapinduzi kwa FAIDA YA NCHI ,watu wake na VIONGOZI WA HIYO SERIKALI.

Sasa huwa tunawalaumu sana Polisi wa hizi nchi zetu za Afrika wakati mwingine KIHISIA tu.

Hebu tufikiri hivi..

Ni juzi tu mh.Mbowe AMENG'AKA MNO.....aliyoyaongea jukwaani ni "alarming point" kwa SERIKALI yoyote hata ingekuwa ni ya CHADEMA.

Baada ya "kung'aka kwake" yakafuata matamko ndani na nje ya nchi....haswa kutoka kwa mh.Tundu Lissu kuwa ,kuhusu KATIBA MPYA ni lazima ipatikane kwa HERI AMA KWA SHARI ....so put yourself in that position....would you let things going without putting your nose on it?!!!

TUTAFAKARI JAMA.....

POLISI WAKO SAHIHI NANYI BAWACHA....2 months ago ,BAWACHA from LAKE ZONE wanted to demonstrate in Dodoma against Speaker's decision on "Covid-19 members of parliament's" before cancelling their gathering following Police's ban.....

Jamani jama ,NCHI HA ZIENDESHWI KILIBERALI eti tu kwa kuwa Kuna UHURU WA VYAMA VYA UPINZANI...UHURU WA KUKUSANYIKA.....

#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom