Dar Firm (VIP Engineering and Marketing) Account Seized in Holland

Dar Firm (VIP Engineering and Marketing) Account Seized in Holland

Kikwete na wapambe wake wakina MAKINDA na PINDA hawawezi kukubali iundwe tume ya bunge kufichua uchafu wao kwani bado wana maumivu ya athari za uchunguzi wa EPA!! Walikula hela za EPA kwa mgongo wa wakina MARANDA ; wakati Maranda na Farijalla wanaozea jela wao wako nje wanakula bata!!! Ukisikia nchi imenyimwa msaada wa Millenium Challenge kutoka marekani ujue itakuwa kwa sababu ya corruption ya fedha za ESCROW; kwani wafadhili wamelivalia njuga suala la rushwa hii!!

Wakinyimwa watapata akili,
 
Nikichaguliwa kuwa Raisi wa Tanzania, ndani ya siku 100 ntaweka mambo sawa na kuhakikisha, Pesa zote ambazo zimetoroshwa nje ya Nchi kijanja janja zinarudishwa na Wezi wote wako ndani,Mikataba yote ya kilaghai kwenye Madini,Mafuta na Gas,na kwenye Makampuni mbali mbali ka Tanesco nafutilia mbali, yaani ndani ya siku 99 ni mchakamchaka wa Hatari siku ya mwisho nakabidhi Madaraka kwa Spika Mweledi kama Mimi sio huyu 6 wa sasa alafu narudi Uraiani nikiwa na Amani Moyoni, kwani ntakuwa nimewapa Wananchi kile ambacho walikihitaji yaani Rais Mchapakazi na Muadilifu.
 
Nakumbuka Mkuu itakuwa poa sana huyo aliyemuita Tumbili naye awemo katika list ya wale watakaopandishwa kizimbani, lakini kwa Serikali hii iliyojaa mafisadi tusishangae hii kesi ikapotezewa kama zilivyopotezewa nyingine za nyuma, "Serikali imefanikiwa kupata pesa zote bilioni 200 hivyo wahusika wa wizi wa pesa hizi hawatachukuliwa hatua zozote za kisheria." Hata majina ya wezi yanaweza kufanywa siri. Kuna kingunge mmoja alidai pesa zile si za Serikali.

Hawezi kupandishwa mahakamani. Nina kuhakikishia hilo.
 
Nikichaguliwa kuwa Raisi wa Tanzania, ndani ya siku 100 ntaweka mambo sawa na kuhakikisha, Pesa zote ambazo zimetoroshwa nje ya Nchi kijanja janja zinarudishwa na Wezi wote wako ndani,Mikataba yote ya kilaghai kwenye Madini,Mafuta na Gas,na kwenye Makampuni mbali mbali ka Tanesco nafutilia mbali, yaani ndani ya siku 99 ni mchakamchaka wa Hatari siku ya mwisho nakabidhi Madaraka kwa Spika Mweledi kama Mimi sio huyu 6 wa sasa alafu narudi Uraiani nikiwa na Amani Moyoni, kwani ntakuwa nimewapa Wananchi kile ambacho walikihitaji yaani Rais Mchapakazi na Muadilifu.
Nimeipenda sana comment yako lakini inanipa wasiwasi kitu kimoja ambacho ni tatizo la karibia kila Mtanzania. Kwamba kila mtu anataka kuitumikia nchi yake pale tu atakapopewa urais na si vinginevyo!
Sasa ni kwa nini tusijiulize, aliyesema 'ukweli na uwazi' alideliver kiasi gani cha hiyo filosofi yake na je, aliyesema 'maisha bora kwa kila Mtanzania' ni wangapi maisha yao yamekuwa bora mbali na hawa wanaofungiwa accounts na wanaopokea hiyo michango ya $1,000,000!????
Kukomesha haya mambo ni bora kuanza uwajibikaji katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na kuunganisha nguvu badala ya uzalendo wa vyeo. Kama kweli mnataka mabadiliko basi badilisheni falsafa kwa kuweka chama chenye mawazo, ofisi, watu, propaganda tofauti ili tuone kama miaka 50 iliyopita inaweza kuwa mibaya au mizuri na 20 ijayo!

inatiaaaa hasira huyu jamaaa rugemalila mtu unaweza mmeza mzima mzima nchi hii kaichezea anavyotaka......
 
Hii nchi sijui nani atakuja kuiokoa ....!!
 
Hii nchi sijui nani atakuja kuiokoa ....!!

Wewe mwenyewe.

Siyo Mungu wala "A Man of the People".

Just you lakini ni mpaka pale utakapoamua kufanya hivyo.
 
Wewe mwenyewe.

Siyo Mungu wala "A Man of the People".

Just you lakini ni mpaka pale utakapoamua kufanya hivyo.

Kweli kabisa EMT watu bado wana mawazo sijui jesus au Mohammad atakuja kutukomboa....saa ya ukombozi ni sasa....na mashujaa ni sisi wenyewe
 
hivi kweli hii benk ya kanisa haikuliona hili? na kwanini meneja wake hakuwa na wasiwasi na hizo transaction
 
Hapa cha kuangalia ni kwanini pesa hizo zilipitia mkombozi? Kulikuwa kuna lengo gani? Mfano Labda Anna Tibaijuka anaweza kusema sababu za pesa za mchango wa Babro Johnson zilipitia mkombozi bank na sio account ya shule moja kwa moja! Pengine ni nani kati yao alipendekeza pesa zipitie huko na kwa sababu gani?
Inawezekana kweli mpokea pesa alipokea pesa bila kujua ni haramu au lah lakini kuna maswali anapaswa kuyajibu!

Mimi Jana nilitetea pengine hana kosa lolote na hajui lakini nimeanza kujiuliza why mkombozi account na sio Mama ana au Babro johnson bank account?

Halafu swala la kusema BOT waifungie Mkombozi kisa imepokea pesa hilo si sawa,Mkombozi wanafanya biashara na hawawezi bagua wateja na katika hili sijaona kosa lao kabisa labda ikithibitika wamehusika!

Hosea kusema atawashitaki walio pokea pesa hili nalo linaweza lisiwe sawa maana kupokea pesa linaweza lisiwe kosa kabisa labda kama ithibitike watuhumiwa walikuwa wanajua ni pesa haramu na walikuwa kwenye deal!

Kwangu Mimi naona Anna Tibaijuka ana maswali machache ya kujibu kwenye hili sakata na kujinasua!

Cc nyumba kubwa

Mkuu Ruttashobolwa nawe tayari umeishapigwa upofu na hela ya ugoro?
 
Last edited by a moderator:
Hata bank ya Vatican imekuwa ni chaka lakupitishia fedha haramu,kama sijakosea nilisoma mahali kuwa papa mpya amesema ifungwe ,naunga hoja kanisa nabenki wapi na wapi,ngoja tusubili na benki yetu ya pale Mwenge karibu na Patel Contractors.

Mkuu ni Afadhali ile ya MWENGE manake ni mtu binafsi Ufisadi haiwezi kuwa issue lkn CATHORIC ni taasisi.....ila dah,,,,,,
 
Hawezi kupandishwa mahakamani. Nina kuhakikishia hilo.

You are very right kuwa hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wezi hawa kwani wanaotakiwa kutoa uamuzi wa kuwafikisha mbele ya haki wanahusika na wizi huo directly or indirectly through their assistants!!
 
Mkuu Shark linapokuja swala la ufisadi wa pesa za walipa kodi, mie sioni ukakasi wa aina yoyote ile. Wote waliopokea pesa za wizi wanastahili kuanikwa hadharani na pia kupandishwa kizimbani.

BAK kuna uzi uliletwa hapa kwamba kuna page 24 ya jinsi transaction zilivyofanyika mkombozi na jina la Anna Tibaijuka ni la kwanza ila akasema kuna viongozi wakubwa wa vyama viwili vya upinzani hudhani kwamba hapo litaleta ukakasi katika uchangiaji bungeni
 
Last edited by a moderator:
Wakinyimwa watapata akili,

Mbona wameishanyimwa kwani mradi wa Vyandarua Hati Punguzo umeisha futwa na kitakachofuata ni kunyimwa ARV za UKIMWI na hapo ndipo tutakapojua ubaya wa hiki chama cha majangiri (CCM)
 
Mkuu Shark linapokuja swala la ufisadi wa pesa za walipa kodi, mie sioni ukakasi wa aina yoyote ile. Wote waliopokea pesa za wizi wanastahili kuanikwa hadharani na pia kupandishwa kizimbani.

Akiwemo na Tibaijuka
 
Last edited by a moderator:
Habari ndiyo hiyo, Serikali iliyojaa mafisadi kamwe haiwezi kumtosa mwenzao/wenzao kwa kumpandisha kizimbani kwa wasiwasi huyo mwenzao anaweza kuanika mengine ya uchafu mkubwa zaidi.

Hawezi kupandishwa mahakamani. Nina kuhakikishia hilo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom