Dar Firm (VIP Engineering and Marketing) Account Seized in Holland

Dar Firm (VIP Engineering and Marketing) Account Seized in Holland

BAK
kuna uzi uliletwa hapa kwamba kuna page 24 ya jinsi transaction
zilivyofanyika mkombozi na jina la Anna
Tibaijuka
ni la kwanza ila akasema kuna viongozi wakubwa wa
vyama viwili vya upinzani hudhani kwamba hapo litaleta ukakasi katika
uchangiaji bungeni

ni la kwanza kwa maana ya A au ndo alipewa nyingi?
 
Last edited by a moderator:
huyu kaka ruge hana washauri, hizi pesa angeweka crdb pangekuwa shwari tu. ona wameshachoma utambi.
 
BAK kuna uzi uliletwa hapa kwamba kuna page 24 ya jinsi transaction zilivyofanyika mkombozi na jina la Anna Tibaijuka ni la kwanza ila akasema kuna viongozi wakubwa wa vyama viwili vya upinzani hudhani kwamba hapo litaleta ukakasi katika uchangiaji bungeni

Hakika hayo Majina yatajwe tu, lakini sitoshangaa nikisikia ni Cheyo na Mrema, Maana hawa sikuwaona Bungeni wakipiga kelele kuhusu zile hela.
 
Hakika hayo Majina yatajwe tu, lakini sitoshangaa nikisikia ni Cheyo na Mrema, Maana hawa sikuwaona Bungeni wakipiga kelele kuhusu zile hela.

kama ni hao itakua afadhali ya mjadala lakn cjui kama TLP ni chama kikubwa cha upinzan
 
tulisema kuna kitu kilikua hakiko sawa ila FaizaFoxy akawa anatoa mawazo yake binafsi kama naye kagaiwa fungu ..... UCHUNGUZI HURU wa hii kitu utafunga wengi sana .... ngoja movie iendelee!!!

Kikwete na wapambe wake wakina MAKINDA na PINDA hawawezi kukubali iundwe tume ya bunge kufichua uchafu wao kwani bado wana maumivu ya athari za uchunguzi wa EPA!! Walikula hela za EPA kwa mgongo wa wakina MARANDA ; wakati Maranda na Farijalla wanaozea jela wao wako nje wanakula bata!!! Ukisikia nchi imenyimwa msaada wa Millenium Challenge kutoka marekani ujue itakuwa kwa sababu ya corruption ya fedha za ESCROW; kwani wafadhili wamelivalia njuga suala la rushwa hii!!
 
Hapa cha kuangalia ni kwanini pesa hizo zilipitia mkombozi? Kulikuwa kuna lengo gani? Mfano Labda Anna Tibaijuka anaweza kusema sababu za pesa za mchango wa Babro Johnson zilipitia mkombozi bank na sio account ya shule moja kwa moja! Pengine ni nani kati yao alipendekeza pesa zipitie huko na kwa sababu gani?
Inawezekana kweli mpokea pesa alipokea pesa bila kujua ni haramu au lah lakini kuna maswali anapaswa kuyajibu!

Mimi Jana nilitetea pengine hana kosa lolote na hajui lakini nimeanza kujiuliza why mkombozi account na sio Mama ana au Babro johnson bank account?

Halafu swala la kusema BOT waifungie Mkombozi kisa imepokea pesa hilo si sawa,Mkombozi wanafanya biashara na hawawezi bagua wateja na katika hili sijaona kosa lao kabisa labda ikithibitika wamehusika!

Hosea kusema atawashitaki walio pokea pesa hili nalo linaweza lisiwe sawa maana kupokea pesa linaweza lisiwe kosa kabisa labda kama ithibitike watuhumiwa walikuwa wanajua ni pesa haramu na walikuwa kwenye deal!

Kwangu Mimi naona Anna Tibaijuka ana maswali machache ya kujibu kwenye hili sakata na kujinasua!

Cc nyumba kubwa
colosal amounts of money involved indicate that there is a syndicate of people involved. By following the money trail you can know who involved. You can not under estimate an influence of a cabinet minister in facilitating this obvious dubious deal. Anyway it is you choice to be a devil's advocate
 
Let it be CHADEMA and CUF.
Lakini niliona hawa jamaa wa CHADEMA wakishiriki kukomalia hii kitu, au kuna uwezekano walikuwa wanazuga?

mkuu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu ucje ukaongea na mwanasiasa eti off record ipo cku atakutaja hadharani kama itakua na manufaa kwake
 
sasa mwanasheria amemtukana kijana tumbili kumbe yeye ndio tumbili anakula shamba la wa TZ
 
Mkuu kuuliza maswali ni kupotosha? Unajuaje hayo uliyo yasema pengine nilikuwa siyajui? Kuuliza ni kupotosha?
Mimi si mtetei mtu tunachotafuta hapa ni ukweli!

Ila na wewe una tatizo la ukabila ndugu. Unless unafanya masihara kwenye threads za watu, mbiNguni hatuendi kwa dhana ya kunyanyapaa ukabila. Elimu haikusadiii, na ni worse. Halafu nasikia eti umesomea sheria pale law of school.
 
Nchi imeoza Mkuu Bulldog sasa wanataka kumuingiza fisadi mwingine ili aendeleze ufisadi wao. Kiongozi aliyeipenda Tanzania na Watanzania na alijali maslahi ya nchi ni Mwalimu tu(RIP) wengine wote wezi na mafisadi.

Mwalimu alianzisha viwanda kibao, sasa hivi vimekufa vyote
 
Ndiyo hivyo Mkuu.

Wanajinasibu kwa usomi.

Lakin believe me ndan ya jii miaka 50 ya uhuru hawa ndio wamesababisha umaskin ndan ya Taifa hili.

Wizi na ufisadi huu unaofanyika chini chini wao wanahusika kwa kias kikubwa sana.

Hiki tukitambue uhalisia wake.

Mkuu unachekesha sana, huu uzi umeuvamia tu. Kwa hiyo siyo ccm tena bali ni hawa ndugu zetu, ambao ni akina nani sasa???!!! Unachekesha sana kuliko kawaida, kibaya zaidi serikali mbili itaendelea kama kawa ili hao ndugu unaowananga watafune zaidi, kwani wa tz kama wewe akili hamna kabisa na siyo uwongo.
 
tulisema kuna kitu kilikua hakiko sawa ila FaizaFoxy akawa anatoa mawazo yake binafsi kama naye kagaiwa fungu ..... UCHUNGUZI HURU wa hii kitu utafunga wengi sana .... ngoja movie iendelee!!!

Uchunguzi huru hauwezekani kwasababu wameshika kila sehemu, mkitaka kuibua ukweli mtaishia kuuliwa na usalama wa taifa wao
 
Mnaoilaumu Mkombozi bank kwenye hii saga mnaweza kuwa sawa au sio sawa. Kama JR alikuwa na documents zote za jinsi hela ilivyopatikana kama KYC/AML procedures zinavyotaka bank haiwezi kukataa kuziweka na ukizingatia pesa yenyewe imetoka BOT ambao ndio wasimamizi wa Ant Money Laundry (AML) procedures sio rahisi kuwa na doubt.

Watu wanaoilaumu MKOMBOZI BANK wanakosea sana, wale wanafanya biashara na wameshahakikisha sheria zote zimefuatwa.
 
Tukidai maelezo tunaitwa tumbili au hatujasoma kiasi cha kuulizwa elimu yetu. Mungu mkubwa wazungu wamewabana wanafanya tuliotaka wafanye.

Upinzani ukiingia inabidi ishughulikie ufisadi wote ambao umeshatokea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom