Watu
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 3,231
- 1,470
Asilimia kubwa ya chanzo cha Ajali ni uzembe wa dereva na wahusika wa wa Basi lenyewe, tulijaribu kuwapigia simu maajenti wa Arusha wakasema kama ni Gari ya Robert (driver) huo ndio mwendo wake na wakenya ndio maana wanaipenda. Tuliriport kwa Inspector wao wa Same akamuonya ila baada ya kutoka Korogwe speed iliendelea na hatimae alipofika Mkata likatokea la kutokea na tulipowajulisha maajenti wa Arusha walichouliza kwanza ni kama gari lao limeumia sana badala ya kuuliza hali ya wateja wao. Huu ni mwanzo wa mwisho wa enzi ya Dar Express wanaandaa kaburi lao soon,siku chache zilizopita Benzi lao liliteketea lote kwa MOTO na mengine kila siku yanafia njiani,uzembe wa madereva na huduma hafifu ndani ya gari na mengineyo meengi ndio mwanzo wa mwisho wao
Hiace baada ya kugongwa na kurushwa zaidi ya mt tano na Dar express #T844 BDR
Dereva wa hiace Iliyogongwa hoi
Hiace baada ya kugongwa na kurushwa zaidi ya mt tano na Dar express #T844 BDR
Dereva wa hiace Iliyogongwa hoi