Dar Express #T844 BDR la Nairobi to Dar es salaam 23/10/2012 kidogo lituuwe

Sehemu za limit zinaonyeshwa na ni 50km/hr au 80km/hr..na zingine hakuna limit ni kukanyaga tu hivyo ni umakini wa driver na gari lake..
Mkuu speed limit ni 80kph isipokuwa maeneo maalum kama vile kwenye vivuko vya watu/wanyama, vijiji ndo spidi inatakiwa iwe pungufu 50 au 30kph au pungufu ya hapo kutegemea na eneo husika.

Hata mabasi yanaposajiliwa hiyo 80kph huwa ni mojawapo ya masharti, ndo maana kipindi fulani ilitengenezwa sheria ya "Speed governor". Hadi sasa haijafutwa hiyo sheria isipokuwa ufuatiliaji ndo umekuwa tatizo. Hata hivi karibuni walitaka kufunga "car track" kwa kila bus, lengo kuu pamoja na mambo mengine ni kufuatilia mienendo ya madereva hasa kwenye suala la spidi. Na ndio maana utakuta trafiki wanakaa na kifaa cha kupima spidi na akikukamata umekwenda zaidi ya 80kph lazima aku-charge.

Kama unaendesha gari kuwa makini sana, ukikamatwa umekwenda spidi zaidi ya 80kph hilo ni kosa.
 
Inasikitisha sana kuona kampuni iliyokuwa nzuri kama Dar express ikianza kusuasua. Sio siri, huduma za hawa jamaa zimedorora sana ukilinganisha na walikoanzia. Uongozi wa Dar express fanyeni kitu, kuiokoa kampuni. Bado mna wateja wengi tu wenye imani na kampuni yenu.
 
nilienda mbeya na prince muro marcopolo ilikua inatembea balaa,ila sumry walikua wanatupita kama tumesimama asee gari za mbeya ndo balaa
 
Dar express ni UOZO mtupu kwa sasa! Mimi na familia yangu hupenda kutumia KILIMANJARO express. Nimewaachia skrepa zao na madharau yao...
 
Huyo dereva afungwe maisha au mgemlamba risasi hukohuko njiani.
 
Hivi kuna watu bado wanapanda hilo gari! hao Jamaa hawana utu kabisa. Ikitokea ukasizia, hata zile soda au maji inakuwa imekula kwako. Wajanja walishahama hapo siku nyingi.
 
Kulalama hakwishi Je ungepanda Bazuu washawasha si ungeshuka njiani
Jamani safari ndefu hazina mwendo wa kobe...Aajali ni ajali ikipangwa utokea cha msingi tuko makini na madereva wetu na kuwasikiliza wateja wetu....
 
Asilimia kubwa ya chanzo cha Ajali ni uzembe wa dereva na wahusika wa wa Basi lenyewe, tulijaribu kuwapigia simu maajenti wa Arusha wakasema kama ni Gari ya Robert (driver) huo ndio mwendo wake na wakenya ndio maana wanaipenda. Tuliriport kwa Inspector wao wa Same akamuonya ila baada ya kutoka Korogwe speed iliendelea na hatimae alipofika Mkata likatokea la kutokea na tulipowajulisha maajenti wa Arusha walichouliza kwanza ni kama gari lao limeumia sana badala ya kuuliza hali ya wateja wao. Huu ni mwanzo wa mwisho wa enzi ya Dar Express wanaandaa kaburi lao soon,siku chache zilizopita Benzi lao liliteketea lote kwa MOTO na mengine kila siku yanafia njiani,uzembe wa madereva na huduma hafifu ndani ya gari na mengineyo meengi ndio mwanzo wa mwisho wao



View attachment 69176



View attachment 69177

View attachment 69179

Hiace baada ya kugongwa na kurushwa zaidi ya mt tano na Dar express #T844 BDR

View attachment 69178

Dereva wa hiace Iliyogongwa hoi

Pole sana Ndugu kwa ajali Mbaya Hiyo!! Ila kutoa malalamiko specifically Dar Express wanataka kutuua naona ni zaidi ya Ajali!! Inaweza kuwa ni Uzembe wa dereva na sio Kampuni!! Ila na wewe ulivyosema ulifanya malalamiko yote kwa mmiliki kwa nini usipige Namba za Mpinga (Kamanda) alizokuwekea Kunako Kiti cha dereva!! Hiyo ni ajali kama ajali nyingine na poleni sana mlioathirika!!
 
Hivi kuna watu bado wanapanda hilo gari! hao Jamaa hawana utu kabisa. Ikitokea ukasizia, hata zile soda au maji inakuwa imekula kwako. Wajanja walishahama hapo siku nyingi.

Soda tu bro inakutoa Imani? Angalia usalama Kwanza!!
 
Unaweza kukuta Huyo dereva wa Hiace alisimama Ghafla!! Sasa ulitegemea dereva wa bus Kubwa afanyeje? Naona mambo ya ""Dar Lux"" Yanaanza tena!! Kampuni iliyoshindwa kuzinduliwa!!
 
Picha ya iyo Dar express iko wapi?? ila kweli wamekuwa wazembe sana siku hizi.. juzi nilikua na KLM express wako vizuri zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom