Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Kwa tunaosafiri sana kuelekea mikoa ya Kaskazini tunatambua nafasi na heshima ya kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express, iliyojiwekea kwa kipindi kirefu. Tuliamini ilichukua nafasi ya Dar Express, ikawa hawana mpinzani.

Ila hivi karibuni imekuwa tofauti, nimesikia mara nyingi watu wakisema hawapandi tena mabasi ya Kilimanjaro, ni kama sikuelewa hadi yaliyonisibu jana.

Safari ilianza saa moja na nusu asubuhi, Arusha. "Disappointment" ya kwanza ni kwenye gari tulilokuta stendi, tofauti na matarajio yangu. Tuliambiwa gari ni "luxury", kwa nauli ya 40,000/-. Lakini kitu pekee cha ki-luxury ndani ya basi hilo kilikuwa ni choo, hakuna zaidi.

"Seat covers" chakavu, zulia la chini lilikiwa na vumbi lilitimka kila watu walipopita.

Gari halikuwa na kiyoyozi, hii sikutegemea kabisa, hasa kuwa nilishaandaa koti la kuvaa nikiwa ndani.

Safari iliendelea lakini gari hakikuwa na mwendo wa kuridhisha, na kufika eneo la Makuyuni, Korogwe, likazima kabisa. Muhudumu wa ndani ya gari akatangaza kuomba radhi na kuwa abiria wasubiri kidogo. Hapo abiria wakawa wakali wakihoji sababu ya kusubiri. Hapo ndipo nikajua wengi hawakuwa wameridhika na hali ya basi lile.

Tukateremka, watu wakajitafutia hifadhi kwenye vivuli vichache na wengine kwenda madukani kujitafutia chochote kitu. Baadae sana dereva akatafuta basi dogo la abiria kutuchukua hadi hitelini kwao Korogwe.... hapo sasa tulikaa kuanzia saa saba na nusu mchana hadi saa mbili na nusu usiku tulipopata nafasi kwenye basi jingine la kampuni hiyo hiyo.

Tarehe 8 Desemba, nilipanda tena basi Lao la mchana kuelekea Arusha. Tulipofika kipande cha kuanzia Same hadi Njia Panda kulikuwa na mvua kubwa. Sikutegemea, ila basi lilikuwa linavuja na nililazimika kusimama hadi Moshi, bikapata nafasi ya kukaa baada ya abiria kadhaa kushuka. Hapo nilitambua pia kuwa kulikuwa na siti zingine kadhaa zimelowa. Hii ni aibu kwa basi la kampuni ya Kilimanjaro.

Hii inanitafakarisha, kwa nini kampuni za kitanzania zinashindwa kuendelea baada ya kufika kilele cha mafanikio, zinaporomoka. Hadithi ilikuwa kwa Scandinavia, ikaja kwa Dar es Express na sasa Kilimanjaro Bus linaelekea kulekule.

Ni kuwa tunalewa mafanikio au tunashindwa kuwa na fikra za mbali zaidi?

Ningependa kujua maoni ya wengine, ila kwa sasa, naona nitasimama kwanza kupanda mabasi ya Kilimanjaro, safari za kubahatisha ni hatari.
 
Mimi niliacha kupanda baada ya kukaa kwenye ofisi yao ya Moshi kwa zaidi ya saa mbili, hili lilikuwa basi la kwanza kutoka Arusha, kisha basi la kwanza na la pili yakakutana Moshi, tulipofika Mombo basi likawa daladala mpaka nikaamua kupiga kelele, toka hapo sina uhusiano nao.
 
BM ndo basi kwa sasa ambalo nalo baada ya miaka 7 litakuwa sio basi la kupanda.

Biashara hufa maana katika kilele cha mafanikio hawa matajiri ufungua miradi mingine na kukopa sana.

Kitendo cha kukopesheka sio sababu ya kukopa bila mipango, hapa ndo wanaharibu, Kilimanjaro ishakufa.
 
Mimi niliacha kupanda baada ya kukaa kwenye ofisi yao ya Moshi kwa zaidi ya saa mbili, hili lilikuwa basi la kwanza kutoka Arusha, kisha basi la kwanza na la pili yakakutana Moshi, tulipofika Mombo basi likawa daladala mpaka nikaamua kupiga kelele, toka hapo sina uhusiano nao.
Hata hili la jana ni luxury la 40,000/- lakini lilikuwa linasimama kila kituo.
 
Back
Top Bottom