Dar Express na Simba zagongana mto Wami...

Hii ni overtaking..hawa madereva wanaovertake kihuni sana...poleni wote mlipatwa na mkasa huu...
 
attachment.php
 
Hizi ni hujma za CDM tu, ndo maana mdau wa CDM kawa wa kwanza kutoa taarifa.
 
inavyoonekana Dar Express ndo alikuwa na makosa, mbona yuko upande wa kulia badala ya kushoto?

It seems so. Dar Express sio my favourite ilishapoteza mvuto tangu mzee Mremi kuwa na tabia ya fukuza fukuza ya madereva. Mabasi ya kistaarabu ya kutoka Arusha -Dar ni Kilimanjaro na Mtei tu. ajali za Dar express ziliongezeka exponentially baada ya madereva kutokuwa na security kufuatia sera mpya ya kuwafukuza hata kwa vikosa vidogo vya kuwahi au kuchelewa Dk 5
 
Dar Express ilikuwa na jina zuri upande wa usafiri wa barabara sasa kama wameanza hivi tena basi, kumenuka kote anga nao haitabiriki nimesikia Precision imepasua matairi, ATCL nako hali tete Baharini nako kunateketea tunasafiri vipi jamani Dah! Mungu atunusuru sisi waja wake, poleni mliopatwa na ajali.
 
Dar Express sina hamu nao kabisa! Juzi jmosi muda wa saa sita kuelekea saa saba eneo la Sango barabara ya Moshi - Njia panda dereva wa basi (namba sikuweza kuzikariri) alianza ku-overtake gari ya mbele yake ili hali mie nlikuwa natokea upande wa pili bado sijapishana nae! Ni busara ya kumpisha tu kidogo ndio iliyoniokoa vinginevyo angenigonga upande wote wa dereva! Leo kusoma kuwa wapata ajali sioni ajabu kwa sababu sielewi madereva huwa wanakuwa na haraka ya kukimbilia wapi! Japo sijui chanzo cha hiyo ajali sishangai kuona wamepata/sababisha ajali! Nilikuwa mteja/abiria wao mimi na familia yangu kwa muda mrefu ila tangu mwanzoni mwa mwaka huu nimebadilisha basi kwa sababu ufanisi ktk huduma zao ulififia kupita kiwango! Nawashauri madereva wa Dar Express kuwa makini barabarani. Poleni kwa ajali na pole kwa abiria wote waliosababishiwa usumbufu.
 
Mkuu Himawari ni kweli huduma za Dar Express zimeanguka. Mabasi yao yameanza kuharibika hovyo njiani. Lakini kuhusu kipande cha barabara kuanzia Njia panda Himo mpaka mjini Moshi kumejazwa matuta barabarani kiasi kwamba naona hakuna sababu ya kuwepo barabara ya lami. Ingeachwa barabara ya vumbi na mashimo ingetosha.
 
Back
Top Bottom