Dar Express na Simba zagongana mto Wami...

It seems so. Dar Express sio my favourite ilishapoteza mvuto tangu mzee Mremi kuwa na tabia ya fukuza fukuza ya madereva. Mabasi ya kistaarabu ya kutoka Arusha -Dar ni Kilimanjaro na Mtei tu. ajali za Dar express ziliongezeka exponentially baada ya madereva kutokuwa na security kufuatia sera mpya ya kuwafukuza hata kwa vikosa vidogo vya kuwahi au kuchelewa Dk 5

Huu ni ushabiki usiokuwa na maana. Inaelekea unataka kusema Dar Express lina makosa kwa sababu bosi wake ana sera ya kufukuza madereva. Inaelekea hiyo ni chuki yako. Pili, unasema Dar Express siyo favorite yako. Kwa hapo unaeleweka kwanini unaponda.
 
Yalikuwa yakitoka Arusha kuelekea Dar na Tanga, hakuna aliefariki ila kuna majeruhi ambao wamepelekwa kwenye hospitali ya Mombo..

Yalikuwa yanatokea Arusha!? Sasa yaligonganaje USO kwa USO wakati yalikuwa yakitokea njia moja!?
 
inavyoonekana Dar Express ndo alikuwa na makosa, mbona yuko upande wa kulia badala ya kushoto?

Sikuelewi. Dar Express iko upande wa kulia wa barabara au upande wa kushoto wa Simba Mtoto. Kama ndivyo Mbona Simba Mtoto naye yuko upande wa kushoto aw Dar Express? Je, hayuko upande wa kulia!?
 
naona mistari miwili mieupe ikiwa imenyooka kabisa lakini bado mtu anaovertake, driving school inahitajika kwa sana!
 
si kweli, ukiangalia mistari ya barabara utagundua Dar Express alikuwa upande wake ila wakati ajali inatokea kila dereva akaamua kuokoa roho yake, na ndio maana unashauriwa ukikaa seat za mbele jitahidi kuchagua seat iliyo nyuma ya dereva.
 
Dah hawa madeva bana yaani alama za barabarani chini zinaonesha wazi hapo c mahali pa ku overtake, bt dereva wa Dar Express akafanya hivyo, yalipomshinda akaona bora awachomekee upande wa abiria ili yeye apone. Sijui kama mafunzo ya veta na lesini mpya zina maana yeyote
 
Back
Top Bottom