Dar Express na Simba zagongana mto Wami...

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Basi la Dar Express na simba mtoto yamegongana uso kwa uso maeneo ya wami.......
darexpress.jpg
 
Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na basi la Simba Mtoto lililokuwa linaenda Tanga yamegongana uso kwa uso maeneo ya Wami. Mwanahabari wa "Globu ya Jamii" aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa ya watu kupoteza uhai yaliyoropotiwa ila, watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Chalinze. 540517575.jpg 540517575.jpg
 
Yalikuwa yakitoka Arusha kuelekea Dar na Tanga, hakuna aliefariki ila kuna majeruhi ambao wamepelekwa kwenye hospitali ya Mombo..
 
dahh...! Sikuelewa kama simba ni basi niliposoma heading. Hebu tupe habari kamili, wamesalimika abiria wote?
 
Poleni sana. Nikiangalia hiyo picha inaonyesha kama Dar Express ndio ameingia lane ya Simba
 
inavyoonekana Dar Express ndo alikuwa na makosa, mbona yuko upande wa kulia badala ya kushoto?
 
hizi ajali naona sasa zimezidi nashauri kila baada ya kilomita 10 zijengwe hospitali za kisasa kwajili ya kupokea majerui na maiti
 
hizi ajali naona sasa zimezidi nashauri kila baada ya kilomita 10 zijengwe hospitali za kisasa kwajili ya kupokea majerui na maiti

Kwa vifaa gani tulivyonavyo, Muhimbili tu hakuna. sasa hizo km 10 kumi si ndo hata plasta hakuna!
 
Pole kwa abiria kwa mshtuko, dah na washukuru Mungu amewanusuru ajali si mchezo!!
 
Back
Top Bottom