Dar es Salaam ya Kunenge ni raha sana

Dar es Salaam ya Kunenge ni raha sana

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,738
Reaction score
3,228
Niwe mkweli nimpongeze RC Aboubakar Kunenge Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa kuruhusu wana CHADEMA na wafuasi wao kumpokea Makamu Mwenyekiti Mh.Tundu Lisu..

Niwapongeze wanachadema kwa utulivu wao wote kwa kipindi chote walichokuwa wanamsubiria Mh Tundu Lisu...kwa kweli wamekua watulivu sana muda wote hasa viongozi wao walikuwa wakiwasihi kuwa watulivu hasa eneo la Uwanja wa Ndege eneo ambalo ni la kibiashara,kiutalii na zaidi ni eneo sensitive sana .

Niwapongeze pia polisi kufanya kaz bila kufuata maagizo ya viongozi wa CCM

TAIFA letu linahitaji ushirikiano ili kuendelea kuwa na amani ili amani iendelee ku-maintai tunahitaji kulinda haki za bindamu,kuruhusu mawazo kinzani yenye kulisaidia Taifa.

Wapinzani pia kuacha kutumika wa watu wa magharibi kuvuruga amani yetu ..tuendeleze tamaduni zetu za kuheshimu mamlaka,kulinda mila na desturi zetu ...mwenye nacho apewe heshima.

Narudia tena kusema siasa zetu zisituchonganishe sisi sote ni ndugu ,wamoja na wote ni watanzania
20200727_200818.jpg

Hongera Mh Kunenge-Rc Kunenge
HONGERA polisi
Hongera CDM
Hongera wananchi wapenda demokrasia na maendeleo.
 
Wana ccm wazoefu walijua
Mbinu hii ya ccm mpya haiwezi kuuwa upinzani
Baada ya miaka minne ya kuwavunja miguu; kuwauwa ; kuwafilisi leo Mgonjwa aliyekua wanadhani anakufa kawa kama vile kapata ARV zikamkubali ghfla ... mji wote umelipuka
Nadhani Magufuli Itabidi abadilishe kabisa washauri wake wa siasa
Ccm ya kina Nape na Kinana ilikua wanatambaaa na hoja hii ya nguvu imewapa nguvu zaidi upinZani

Alafu Taifa wameligawa tunashindwa kumzika Mkapa kwa umoja
 
Mwenyezi Mungu ni mwema. Umati huu ni uthibitisho tosha wa mapenzi ya Watanzania kwa Chadema na Lissu. Na kama atatia mguu mikoani itakuwa hatari tupu.

Nyalandu na Membe wakae pembeni wamruhusu Lissu afanye yake.
 
Wana ccm wazoefu walijua
Mbinu hii ya ccm mpya haiwezi kuuwa upinzani
Baada ya miaka minne ya kuwavunja miguu; kuwauwa ; kuwafilisi leo Mgonjwa aliyekua wanadhani anakufa kawa kama vile kapata ARV zikamkubali ghfla ... mji wote umelipuka
Nadhani Magufuli Itabidi abadilishe kabisa washauri wake wa siasa
Ccm ya kina Nape na Kinana ilikua wanatambaaa na hoja hii ya nguvu imewapa nguvu zaidi upinZani

Alafu Taifa wameligawa tunashindwa kumzika Mkapa kwa umoja
Siasa ya chuki huatarisha amani.
Hakuna viongozi wa kisiasa hasa wa upinzani wanapenda amani itoweke ,usipokuwa viherehere wachache wanaodhani wakiwanyanyasa wapinzani wanapata credibility
 
Hii issue hairatibiwi na Kunengee bali amri zinatoka Centricom na kubwa viongozi wa jeshi hasa TPDF wameingilia kuzuia kuvuruga msiba wa Amiri jeshi mkuuu mstaafu
Kwa Sasa kutokana na msiba TPDF are in charge na Unajua huwa hawatakagi ugomvi na wananchi ambao ikitokea vita ndio wanawategemea slogan yao ni UMOJA
 
niseme kweli katika jambo ambalo serikali hii imefanya kama ninavyotaka ni hili LA Leo, waendelee kutufurahisha tumzike Mzee wetu mkapa kwa amani zaidi maana najua lissu atahudhuria na rais atawaomba msamaha na kuwasihi tuishi kwa amani, safi sana tukio LA leo linaleta muungano wetu na kusahau tofauti zetu!
 
Hii issue hairatibiwi na Kunengee bali amri zinatoka Centricom na kubwa viongozi wa jeshi hasa TPDF wameingilia kuzuia kuvuruga msiba wa Amiri jeshi mkuuu mstaafu
Kwa Sasa kutokana na msiba TPDF are in charge na Unajua huwa hawatakagi ugomvi na wananchi ambao ikitokea vita ndio wanawategemea slogan yao ni UMOJA
nimekupata mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom