beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 18, 2021 amezindua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi, Bohari Kuu Kurasini
Pia amekagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake
UPDATES:
RAIS AWATAKA POLISI WASITUMIE MAKOSA KAMA KITEGA UCHUMI
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Polisi wasitumie makosa kama kitega uchumi kwa kutoza faini mbalimbali badala yake wajikite kwenye kudhibiti makosa
Ameyasema hayo alipokuwa katika Ziara ya Kuzindua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi, Bohari Kuu Kurasini ambapo Polisi waliliripoti kupungua kwa mapato kutokana na kupungua kwa makosa
Rais Samia amewataka wajikite zaidi kwenye kuelimisha Umma ili kupunguza makosa na sio wao kutegemea kukusanya fedha kutoka kwenye makosa mbalimbali
RAIS SAMIA: UDHIBITI WA VITENDO VYA UJAMBAZI UTATUMIKA KUTENGUA NA KUTEUA MAKAMANDA WA POLISI
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema miongoni mwa vigezo vitakavyotumika kuteua au kutengua Makamanda wa Mikoa ni udhibiti wa vitendo vya ujambazi ikiwemo wa kutumia silaha
Akizungumza kutokea Kurasini, Dar amesema "IGP umeniletea majina kadhaa kwa ajili ya zile Kamisheni mbili, hiki kitakuwa kimoja kati ya vigezo nitakavyotumia"
Kuhusu matukio ya udhalilishaji wa kijinsia, Rais Samia ametoa wito kwa Jamii kuweka mkazo zaidi kwenye suala la malezi kwani vitendo hivyo hutokea ndani ya Familia
UTAPELI MITANDAONI: RAIS SAMIA AHOJI USAJILI KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE
Rais Samia Suluhu Hassan amesema licha ya kufanyika zoezi la usajili laini za simu kwa kutumia vidole, vitendo vya utapeli na wizi mitandaoni bado vimeendelea kushamiri
Ameeleza, "Najiuliza ule usajili ulikuwa kiini macho au ni nini? Kwasababu kama tumesajili vile kila namba inajulikana, na kama kuna zisizojulikana zinatolewa na Shirika gani la simu?"
Amelitaka Jeshi la Polisi kusimamia suala hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Mtandao wa Serikali, TCRA na Taasisi nyingine za fedha za Umma na Binafsi zikiwemo Benki na Kampuni za Simu