Dar es Salaam: Jeshi la polisi lamshikilia mkazi mmoja baada ya kumkuta anamiliki silaha kinyume cha sheria

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia Mohamed s/o Kassim miaka 47, mkazi wa Mbagala kwa tuhuma za kumiliki silaha

aina fatih 13turukye Pisto yenye No, TZ C.A.R 1053515 ikiwa na magazine yake isiyokua na risasi kinyume cha sheria.

Mnamo tarehe 07/04/2020 saa 12:30 jioni huko maeneo ya kibondemaji Mbagala kikosi kazi cha kupambana na ujambazi kilipata taarifa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye ni mlinzi wa Suwata bar iliyopo kariakoo akiwa anatembea barabarani na silaha hiyo ikiwa ndani ya mfuko mweusi.

Baada ya mahojiano ya kina mtumiwa huyo alieleza kuwa silaha hiyo aliokota siku za nyuma na hakuripoti popote.

Aidha mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa ili kubaini kama kuna matukio ambayo amewahi kufanya au kushirikiana na wahalifu wengine.

SIKUKUU YA PASAKA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linatoa rai kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam kuepuka kufanya uhalifu, vurugu za aina yoyote na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka na kuendelea na jitihada za kujikinga na virusi vya corona (covid 19).

Aidha Jeshi la Polisi linawashukuru wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri waliotii amri ya serikali ya kupakia abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo ndani ya gari (level seat) na wanaokaidi agizo hilo sheria inachukua mkondo wake. Pia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dae es salaam linawashukuru wanananchi wote wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Imetolewa na:

LAZARO MAMBOSASA– SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAM.

09/04/2020
 
Back
Top Bottom