Dar Bana.....Nusura Nife!!

Dar Bana.....Nusura Nife!!

Heshima wakuu...
Mwenzenu jana nusura nife baada ya kugongwa na nyoka, maeneo ya huko Ubungo Maziwa. Ilikuwa ni mida ya jioni nikitoka katika mihangaiko ya kila siku. Baada ya kugongwa ilibidi niwahi katika zahanati zilizo jirani, lakini kila nilipoenda walikuwa wakinishangaa eti ni jambo la ajabu mtu kugongwa na nyoka Dar.
Zahanati ya mwisho nilipoenda manesi walipigwa na mshangao kabisa, eti wakitaka kujua ni wapi huko nilikokuwa hadi nigongwe na nyoka. Lakini kilichonishangaza zaidi ni kuwa zahanati tatu nilizopita hawakuwa na huduma ya kutoa kwa mtu aliyegongwa na nyoka. Ilibidi nikodi teksi inikimbize muhimbili ndiko nilipata huduma ya kwanza....

hata mi najiuliza, ulikuwa unafanya nini?
 
Mie wala simtanii. Ushawahi kujiuliza uking'atwa na nyoka kwenye kalio ama kiuno unafungaje kamba? Hapo ukute sasa mashaallah!
utani mwinhine bwana, aca tu! mku auvuling'atwa na ng'e
 
Kwanza pole sana mkuu.2.wasamehe bure waliokucheka bila kutimiza wajibu wao na amini Mungu nakupenda.3.Sinashaka kuwa umejifunza mengi kutokana na tukio hilo pamoja na hali ya majiji yetu.Pole sana
 
mishemishe za vichakani siyo nzuri ndugu yangu, kwanini usitafute nyumba za wageni?

Hakuna bosi hakukuwa na mishemishe yoyote, halafu wala sio kichaka!
 
Pole sana ,huku kwetu maeneo ya kimara ni kawaida kuumwa na nyoka hasa nyakati za mvua na hospital za huku zina huduma,mimi niliumwa na nyoka miaka mitatu iliyopita nashukuru Mungu nilienda Neema hospital na walinipa huduma muhimu.
 
Back
Top Bottom