Dar Bana.....Nusura Nife!!

Dar Bana.....Nusura Nife!!

kaeso

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
548
Reaction score
97
Heshima wakuu...
Mwenzenu jana nusura nife baada ya kugongwa na nyoka, maeneo ya huko Ubungo Maziwa. Ilikuwa ni mida ya jioni nikitoka katika mihangaiko ya kila siku. Baada ya kugongwa ilibidi niwahi katika zahanati zilizo jirani, lakini kila nilipoenda walikuwa wakinishangaa eti ni jambo la ajabu mtu kugongwa na nyoka Dar.
Zahanati ya mwisho nilipoenda manesi walipigwa na mshangao kabisa, eti wakitaka kujua ni wapi huko nilikokuwa hadi nigongwe na nyoka. Lakini kilichonishangaza zaidi ni kuwa zahanati tatu nilizopita hawakuwa na huduma ya kutoa kwa mtu aliyegongwa na nyoka. Ilibidi nikodi teksi inikimbize muhimbili ndiko nilipata huduma ya kwanza....
 
Loh. . . pole sana.

Mi najua huduma ya kwanza kabisa ni kufunga juu kidogo ya ulipogongwa ili sumu isisambae, au hata hiyo tu walishindwa?
 
Hata hiyo inaonekana walishindwa, nilihudumiwa na dereva teksi..........nilipofika Muhimbili ndipo nilidungwa sindano ya kuuwa sumu(mimi siijui ni dawa gani ile maana sio mtaalamu)
 
Labda aligongwa kwenye kiuno, wakashindwa wamfungeje.
Pole mhanga.
Loh. . . pole sana.

Mi najua huduma ya kwanza kabisa ni kufunga juu kidogo ya ulipogongwa ili sumu isisambae, au hata hiyo tu walishindwa?
 
Pole sana hapo ndo unajua huduma za msingi za jamii ,hata huduma ya kwanza hatuna. Bora ungekimbilia ubungo hapo ungepata jiwe la nyoka fasta.
 
Pole mkuu!
Zahanati zetu nyingi hasa za mijini ni business oriented,hasa Dar. Eti jiji.
 
pole sana mkuu....
Sasa wanashangaa nyoka tu, mbona huku kwetu 'new manzese' mabwepande, mlevi anaweza kuliwa na fisi makalio.
Yaani hata mimi nilishangaa sana zahanati kukosa huduma ndogo tu ya kuhudumia waliogongwa na nyoka.... Sijui wanaojeruhiwa na nge wanahudumiwa vipi!!
 
pole sana. labda wanadhanini dr hakuna nyoka. wamejisahau
 
Heshima wakuu...
Mwenzenu jana nusura nife baada ya kugongwa na nyoka, maeneo ya huko Ubungo Maziwa. Ilikuwa ni mida ya jioni nikitoka katika mihangaiko ya kila siku. Baada ya kugongwa ilibidi niwahi katika zahanati zilizo jirani, lakini kila nilipoenda walikuwa wakinishangaa eti ni jambo la ajabu mtu kugongwa na nyoka Dar.
Zahanati ya mwisho nilipoenda manesi walipigwa na mshangao kabisa, eti wakitaka kujua ni wapi huko nilikokuwa hadi nigongwe na nyoka. Lakini kilichonishangaza zaidi ni kuwa zahanati tatu nilizopita hawakuwa na huduma ya kutoa kwa mtu aliyegongwa na nyoka. Ilibidi nikodi teksi inikimbize muhimbili ndiko nilipata huduma ya kwanza....

Ulikuwa unavizia mtu kwenye nyasi nini?
 
pole sana. labda wanadhanini dr hakuna nyoka. wamejisahau
Hiki ndicho nilichokiona, maana zahanati moja nesi aliongea kwa mshangao "Dar nako kuna nyoka?? Nilidhani ni huko maporini mikoani tu?".....Nilitamani nimrukie nimpige vichwa, bahati yake maumivu yalinizidi.....
 
pole sana mkuu....
Sasa wanashangaa nyoka tu, mbona huku kwetu 'new manzese' mabwepande, mlevi anaweza kuliwa na fisi makalio.

Fisi anafuata harufu ya kinywaji au?
OTIS
 
Ulikuwa unavizia mtu kwenye nyasi nini?
Ha ha haaah!! hapana TIQO ilikuwa ni njia, na yule nyoka alikuwa anavuka nadhani alisikia vishindo na aliniona hivyo akajificha, nilivyofika jirani akanigonga kisha akakimbilia sehemu kulikuwa na mawe. alikuwa mkubwa mweusi.
 
nimjuavyo nyoka mpaka akugonge either umemkanyaga au unatishia maisha yake, hapa dar nyoka wapo ila ni wapole sio wagongaji bali kuna wakutegeshewa ndo wamejaa
 
kwaiyo hapa tunaongea na mwafirika wa sumu ya nyoka?
pole sana mkuu
 
nimjuavyo nyoka mpaka akugonge either umemkanyaga au unatishia maisha yake, hapa dar nyoka wapo ila ni wapole sio wagongaji bali kuna wakutegeshewa ndo wamejaa
Unamaanisha nilitegeshewa??
 
Back
Top Bottom