Dar: Asalimisha Bastola na risasi kwa Polisi, adai uhalifu haulipi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mifumo ya kiusalama ikiwa ni pamoja na kushirikisha wananchi katika kuzuia, kubaini, na kupambana na vitendo vya kihalifu kuanzia ngazi ya mtaa.

Katika hatua hiyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi wema limefanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Shortgun Pump action yenye namba MV 59787P iliyokatwa kitako na bastola aina ya Makarov yenye namba B.4135*1979 ikiwa na risasi tisa.

Silaha hizo zilisalimishwa eneo la Chamazi Vigoa na mtu mmoja ambaye amedai kuacha uhalifu na kudai haulipi.

Pia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 12 Juni hadi 11 Julai 2023 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa halisi wanaojihusisha na matukio ya unyang’anyi na uvunjaji nyumba usiku na kuiba akiwemo Juma Hasan (23) mkazi wa Mji Mwema na wenzake 12.

Watuhumiwa huo wamekamatwa na vitu mbalimbali vya kielektroniki vya wizi ambavyo waliviiba, vitu vilivyokamatwa ni televisheni za aina mbalimbali 13, redio 2, laptop 2, pamoja meza moja ya Tv, baadhi ya watu walioibiwa wameweza kutambua mali zao.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi ili kuwabaini wahalifu kabla hawajaleta madhara katika jamii.

Jeshi la Polisi linahimiza wahalifu wajisalimishe na silaha zao wazitoe kwani operesheni kali maalum inaendelea dhidi ya wahalifu.

1689966051738.png
 
Back
Top Bottom