Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Huyo mwanaume alikuwa mlemavu au mtu wa mitungi au kikongwe?

Mwanaume mwenye utimilifu wa mwili na akili, huwezi chomwa ndani ya nyumba na usitafute means za kutoka nje hata kwa kupitia kwenye dari, kisha kutoka kupitia roof
Omba sana yasikukute ndugu yangu, siku yake tu ilikua imefika apumzike kwa Amani mpambanaji mwenzetu.

Matukio kama hayo ukitoka siyo sababu wewe jabari sana bali Mungu tu hajakuita kwake bado
 
Sikilizia povuuu la wanaume humu sasa

Wanawake sasa wameamka, huu ndo uanamke wa shoka, sio kuja kulia lia humu sijui napigwa, sijui nanyanyaswa! Piga petrol

wanawake wa sasa hawataki ujinga, ukisaliti unasalitiwa. Ukizingua wanakuzingua. Wanaume wakae kwa kutulia na wanawake zao, vinginevyo nyuzi za lawama hazitaisha humu jamvini
 
Duh inabidi tujitahidi kucontrol hasira na usifanye maamuzi ukiwa na hasira maana majuto baadaye, sasa Neema jela inamsubiri huku mume hayupo dhamira itamsuta milele so sad

Bora yako wewe jamaa alipozingua ulileta uzi huku jamvini tukakufariji moyo na sasa unaendelea vyema. Neema kajichukulia sheria mkononi, kamaliza ye mwenyewe .
 
Sahihi kabisa kaka. Hawa wenzetu ni wavumilivu sana ukiwa nao fair, ila ukimzingua, huwa wana maamuzi ya ajabu sana. Binafsi hata katika maisha ya kawaida, huwa sipendi quarrel na mwanamke, huwa wana maamuzi ya ajabu sana hawa viumbe!

Kisaikolojia wanasema mwanamke hupenda kumuona adui yake wa kike akiteseka, ila adui yake wa kiume wao hummaliza sababu wanajua hawana nguvu za kimaumbile kupambana nao.
Nimetoka na kitu hapa
 
Sometimes tuzitafakari kwa makini hizi scenarios

Unakutana na binti ya watu.. Ana ndoto zake .. Mnayajenga na kuingia kwenye ulimwengu wa mahusiano mpaka ndoa
Anakusaidia kwa mengi mno unamtumia mpaka kusikofaa kutumika kiutu.

Unamharibu na kumharibia mengi.. Ila kwakuwa wewe ni wake anaridhia kiroho safi kabisa na bila kinyongo

HALAFU unakuja kumletea zinazomchoma moyo na kumuumiza hisia...! Muogope sana mwanamke aliyejeruhiwa
Ndio umchome mwenzio moto. Kuna watu humu mapenzi yamewahi kutujeruhi tukapoteza muda, fedha na kudhalilika lakini sikuwahi fikiria kuuwa.
 
Huyu dada alichofanya siyo sahihi kabisa na hakuna sababu itakayoweza kujustifaii hayo mauwaji. Akidakwa na yeye sheria ichukue nafasi tu.

Haiwezekani uue mwenzio km unachoma takataka
 
Bora yako wewe jamaa alipozingua ulileta uzi huku jamvini tukakufariji moyo na sasa unaendelea vyema. Neema kajichukulia sheria mkononi, kamaliza ye mwenyewe .
Kabisa nilifanya uamuzi sahihi kuspeak out humu kinachonisibu na nikasaidika, now niko poa kiasi🤔 nawashauri akina Neema wasifanye maamuzi wakiwa na hasira ni majuto baadaye
 
Kabisa nilifanya uamuzi sahihi kuspeak out humu kinachonisibu na nikasaidika, now niko poa kiasi nawashauri akina Neema wasifanye maamuzi wakiwa na hasira ni majuto baadaye

Believe me, with time utapona na utamshukuru Mungu kwa kukuvusha hapo. Sema binadamu huwa tunakosa subira wakati mwingine. Mtu kama hakutaki mwache aende
 
Back
Top Bottom