Dar: Amchoma mpenzi wake na Petroli kisa wivu wa mapenzi

Hamiwezi jua alipitia mateso kiasi gani hadi kufanya hivyo. Kuna wanaume wanajua kutesa wanawake kisaikolojia hadi ujiulize kama alizaliwa au aliokotwa
si unaondoka ukaanze upya...hata kwa sheria......sasa anaenda kuliwa na askari magereza MILELE..........hakuna kitu tamu kama UHURU binafsi ada yangu......maamuzi ya hasira ni mabaya sana
 
Sikilizia povuuu la wanaume humu sasa

Wanawake sasa wameamka, huu ndo uanamke wa shoka, sio kuja kulia lia humu sijui napigwa, sijui nanyanyaswa! Piga petrol
Nadhani itakuwa poa sana ukiyatamka haya maneno siku akifanyiwa ukatili huu mtoto wako wa kiume au mdogo wako wa kiume au kaka yako.

Ni vema kuwa makini na kauli **** mwingine. Usizungumze kwa mihemko au jazba. Huyu ni kijana wa watu na pengine ana familia na wazazi wake wanaomtegemea na kumpenda sana.

Pia huruma zaidi ni kwa huyo binti , unaweza kuta ana wazazi wake umri umeenda wanamtegemea sana , hivi wanakuja letewa taarifa kuwa binti yao amefanya tukio hilo la kikatili na ana hatia na anahatari ya kufungwa maisha au pengine hukumu ya kifo, hivi umewazia haya kabla ya kushangilia?!

Umewawazia hawa wazazi wa binti namna wameumia moyo na upweke wamejisikia kujua binti yao yupo hatiani na pengine wasimuone tena uraiani.

Dah.

Tusiwe tunajadili hivi vitu kiushabiki bali tufungue mioyo yetu na kutafakari kama wanadamu tunaishi vipi kwa sasa katika mahusiano na kushika agizo kuu la upendo?!

C
 
Back
Top Bottom