Daktari huyu alitaka kunibaka?

Daktari huyu alitaka kunibaka?

Inasikitisha sana. Siku moja nilienda katika hospitali fulani maarufu, katika nchi inayosifika kwa mengi mazuri, ili nifanyiwe "eye examination"

Nikaingia katika chumba cha daktari wa macho(ophthalmologist, if not optometrist). Nilifurahi kuona chumba chake kina vifaa vya kisasa vya upimaji wa macho kama vile Penlight, Slit Lamp (Biomicroscope), Tonometer, Fundus Camera...

Baada ya kumweleza daktari huyo kilichonipeleka pale, akaanza kuyachunguza macho yangu. Kisha akachukua penlight na kuanza kunimulika jicho moja moja. Akasogea karibu zaidi na mimi. Mkono wake wa kushoto akauzungusha nyuma ya shingo yangu na kunikumbatia huku akiendelea kumulika macho. Mimi nilitulia tuli tu kama maji mtungini. Lakini moyoni nikawa najiuliza: "hivyo ndivyo madaktari wa macho wanavyofanya eye examination?" Baadaye daktari akaiacha penlight yake akanikumbatia kwa mikono yote miwili, kisha akaniacha. Halafu akaniambia "macho yako hayana shida!"

Hebu niambieni nyinyi wazoefu wa kufanyiwa "eye exam", hivyo ndivyo madaktari wanavyopaswa kumshika mtu anayechunguzwa macho? Au huyu daktari alikuwa na lake jambo? Na angethubutu kugusa sehemu nyingine za mwili asingeisahau siku ile. Ningemkemea kwa Jina la Yesu, pepo la uzinzi limtoke. Hospitali nzima ingejua ameingia mtu asiye na mchezo na dhambi ya uzinzi.

Tujiepushe na uzinzi jamani. Wazinzi na waasherati hawataingia mbinguni. Mahali pao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti.

1 Kor 6:9
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti."
Kwanza unaonyesha kabisa ulisikitika kwanini hakuendelea kukukumbatia! Eti ungemkemea, sasa kwanini hukumkemea.
 
Hiyo ilikuwa extreme customer care mkuu. Hakukuwa na dalili yoyote ya ubakaji hapo.
Extreme customer care? Not quite. Rather, it is a blatant abuse of professional trust and a deep betrayal of the ethical responsibility entrusted to medical practitioners.
 
Kwanza unaonyesha kabisa ulisikitika kwanini hakuendelea kukukumbatia! Eti ungemkemea, sasa kwanini hukumkemea.
Watu wote wanaofanya dhambi nawasikitikia kwa sababu destination yao ni mbaya.
 
Inasikitisha sana. Siku moja nilienda katika hospitali fulani maarufu, katika nchi inayosifika kwa mengi mazuri, ili nifanyiwe "eye examination"

Nikaingia katika chumba cha daktari wa macho(ophthalmologist, if not optometrist). Nilifurahi kuona chumba chake kina vifaa vya kisasa vya upimaji wa macho kama vile Penlight, Slit Lamp (Biomicroscope), Tonometer, Fundus Camera...

Baada ya kumweleza daktari huyo kilichonipeleka pale, akaanza kuyachunguza macho yangu. Kisha akachukua penlight na kuanza kunimulika jicho moja moja. Akasogea karibu zaidi na mimi. Mkono wake wa kushoto akauzungusha nyuma ya shingo yangu na kunikumbatia huku akiendelea kumulika macho. Mimi nilitulia tuli tu kama maji mtungini. Lakini moyoni nikawa najiuliza: "hivyo ndivyo madaktari wa macho wanavyofanya eye examination?" Baadaye daktari akaiacha penlight yake akanikumbatia kwa mikono yote miwili, kisha akaniacha. Halafu akaniambia "macho yako hayana shida!"

Hebu niambieni nyinyi wazoefu wa kufanyiwa "eye exam", hivyo ndivyo madaktari wanavyopaswa kumshika mtu anayechunguzwa macho? Au huyu daktari alikuwa na lake jambo? Na angethubutu kugusa sehemu nyingine za mwili asingeisahau siku ile. Ningemkemea kwa Jina la Yesu, pepo la uzinzi limtoke. Hospitali nzima ingejua ameingia mtu asiye na mchezo na dhambi ya uzinzi.

Tujiepushe na uzinzi jamani. Wazinzi na waasherati hawataingia mbinguni. Mahali pao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti.

1 Kor 6:9
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti."
Kama hukuingiziwa wala hukuiona dhakari nje nje hujabakwa dada. Tulia.
 
Mkuu pole sana yaani uliponea chup chup ilibaki kidogo tu huu Uzi ungekuwa wa kuliwa kimasiara, by the way shikilia msimamo wako dhambi sio ujanja.
Mpe pole huyo daktari maana yeye ndiye aliyeathirika. Mbele za Mungu tayari anahesabiwa dhambi hata kwa kutamani tu.
Mt 5:28
"Lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."
 
  • Thanks
Reactions: al1
Ila wapendwa wanapenda kupigana mashine sana sijui kwanini...
Kanisani kukuta mchungaji anapiga kondoo ni kawaida sana, anawapa na mimba na scandals za ajabu sana....
 
Mimi sina maneno mengi; ila nina Neno la Mungu
Acha zako wewe...
Nyege zikikushika utamtafuta tu jamaa akukune ziishe ili ukitoka hapo ukaendelee na maombi...
Matamanio hayana cha maombi wala kufunga...
Unless uwe umeolewa.
 
Kwa Chai bora uko vizuri
Sio chai, mkuu. Uongo nauchukia kama ukoma. Hujui kwamba waongo hawataurithi ufalme wa Mungu? Soma
Ufunua wa Yohana 21:8
Lakini waoga, na wasioamini na wachafu, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, pamoja na waongo wote, urithi wao upo katika lile ziwa linalowaka moto na kiberiti
 
Ila wapendwa wanapenda kupigana mashine sana sijui kwanini...
Kanisani kukuta mchungaji anapiga kondoo ni kawaida sana, anawapa na mimba na scandals za ajabu sana....
Hao unaowasema ni wachungaji wa mshahara. Siku ya mwisho wataambiwa hivi:
Mt 7:23
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
 
Acha zako wewe...
Nyege zikikushika utamtafuta tu jamaa akukune ziishe ili ukitoka hapo ukaendelee na maombi...
Matamanio hayana cha maombi wala kufunga...
Unless uwe umeolewa.
Kama wewe ndivyo unavyofanya, basi bado hujaokoka. Bado hujamjua Mungu. Kufanya dhambi kwa makusudi ni kumsulibisha Yesu mara ya pili(Ebr 6)
 
Hao unaowasema ni wachungaji wa mshahara. Siku ya mwisho wataambiwa hivi:
Mt 7:23
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Acha zako, hata Daudi alipita na mke wa mtu na alikuwa mfalme na mtume, itakuwa hawa wachungaji njaa wa sasa...
Imani alikuwa nayo Daudi hivi sasa hakuna mtu atamfikia, mambo aliyoshuhudia na hata miujiza aliyoshuhudia hata wewe hadi unakufa hutoshuhudia...

Lakini ndio hivyo alilamba wife wa mtu..
Matamanio ya mwili yapo tu.. usijidanganye..
 
Kama wewe ndivyo unavyofanya, basi bado hujaokoka. Bado hujamjua Mungu. Kufanya dhambi kwa makusudi ni kumsulibisha Yesu mara ya pili(Ebr 6)
Siku moja utakumbuka nachosema..
Mi nakuambia uhalisia we unaleta story..
 
Mkuu, ungekuwa wa kukemea usingetulia tuli.

Ndo maana inashauriwa ikimbie zinaa sio ikemee
Yusufu alikimbia kwa sababu aliona dalili za waziwazi. Mimi sihitaji kukimbia. Yesu anasema mpingeni shetani naye atawakimbia. Anayepaswa kukimbia ni shetani(Yak 4:7-10).
 
Siku moja utakumbuka nachosema..
Mi nakuambia uhalisia we unaleta story..
Uhalisia upi? Yesu alijaribiwa katika mambo yote lakini hakutenda dhambi. Ukiokoka, anakupa uwezo wa kushinda tamaa za mwili zipiganazo na roho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom