Kama haujawahi kunywa energy drinks Hongera na Jiepushe nazo. Kama umezoea kuzitumia Tafadhali weka mpango wa kupunguza na kuacha

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,443
Peace,

Awali ya yote niweke wazi andiko langu halina kusudi la kuhafifisha au kuathiri biashara ya mtu yeyote ila ni ushuhada wa kweli na dhairi wa watu wanaonizunguka.

Nimekuwa nikisikia na kuona vijana wengi wakipendelea vinywaji vya kusisimua mwili alimaarufu "energy drinks" ziko za aina mbali mbali na bei tofauti. Vijana kama boda boda, wanafunzi na vibarua wa kazi za mikono wamekuwa watumiaji sana wa vinywaji hivi.

Nilipata kusikia na kwa sasa nimeshuhudia kuwa vinywaji hivi vina uraibu mkali sana na pia athari za moja kwa moja kwa watumiaji wa mara kwa mara. Nina mifano mingi ila nitataja michache kwa lengo la kujenga hoja na kujifunza kwa pamoja.

Kuna vijana kwenye maegesho ya boda boda nimekua nawasikia kua ili siku iende sawa lazima wanywe energy wengine wamekua hata na utaratibu wa kununua za ziada na kuifadhi ili anapoamka tu cha kwanza ni kunywa energy ndio hujiisi utayari wa kuanza kazi.

Mwezi uliopita nilikua na project ya ujenzi nikawa napita kutazama mradi unakwendaje kulinganisha na report ya msimamizi wa mradi ajabu pale site palikua na makopo ya mo-energy na azam energy mengi sana wala sikujali ila cha kushangaza kuna siku nilikuta wamepiga kazi kwa makisio ya kua mbele ya estimated target kwa zaidi ya kama 25% nilifurahi sana nikaamua kuwalipia bili zao za chakula kwa siku tatu.

Mshangao ulikua wangu waliponisihi sana sana niwaongezee bajeti kucover pia "energy" nilipohoji kulikoni msisitizo ule wakajibu "yani hata chakula hakina maana kama hakuna energy" looo !! Nikasema sawa nitaongeza bajeti ya kinywaji hicho kwa kila mmoja aise shangwe walilopiga ni kubwa mara dufu ya nilipowapatia ahadi ya kulipia chakula. Vijana wako adicted mbaya.

Kuna classmate wangu kwa sasa ni muajiriwa shirika fulani la uma kama afisa manunuzi anakiri bila kunywa energy drink anajihisi kupoteza umakini na uwezo wa kuconcetrate mpaka apate vinywaji hivi.

Sasa hivi karibuni amekua analalamika kuhisi kutetemeka hasa kipindi cha usiku na kifua kuuma na kuhisi moyo kwenda mbio sana hasa anapopata wasiwasi wa jambo hata dogo tu na kuhisi kizunguzungu mda wa jua kali akanishirikisha basi nikajaribu kubrowse mtandaoni ya kwamba nini hasa kinaweza kupelekea matatizo haya ajabu ajabu kote majibu yanahusishwa na matumizi ya kupindukia ya energy drinks.

Nikamshirikisha jamaa akasema pia yeye alikua anahisi watatizo hayo yanahusiana na vinywaji ya kusisimua mwili kwa kua matatizo yote hayo yanapomkuta na basi akapata fursa na akipiga energy mbili chap chap anakua fresh kabisa aise jamani tujihadhari.

Nikaona nifanye ufuatiliaji wa jambo hili nikawafuata boda boda nikawauliza kama kuna nyakati wanajihisi kutetemeka mikono, au kuhisi moyo kwenda mbio au kuhisi kupoteza umakini au kifua kuuma na kizunguzungu.

Kwa mshangao wakasema yote hayo yanawakuta kwa nyakati tofauti ila wakanishangaza kwa mara nyingine kwa kuniambia yote hayo yanapowakuta hununua energy ya baridiiii na kunywa na shida zote na mashwahibu hayo hupotea kwa sekunde chache tu.

Ikumbukwe vinywaji hivi havina hata muda wa miaka 10 sokoni lakini madhari yake yameanza kushuhudiwa punde tu mtumiaji anapotumia je matumizi ya muda mrefu yatakua na madhara kiasi gani ?!

Mimi sio daktari wala sina ujuzi wowote wa kitabibu lakini naona viashiria dhahiri vya madhara ya vinywaji hivi. Niliwahi kuona clip fupi ya Mo Dewji akisema hajawahi kuonja ladha ya vinywaji vyake, (jambo fikirishi sana)

Karibuni tujadili nini uzoefu wako katika matumizi ya vinywaji hivi?


download (1) (14).jpeg
 
Ni mara ya tau nakutana na uzi kama huu na zote zinaelezea madhara ya moja kwa moja ya hivi vinywaji!
Inaweza kusa tatizo ni kubwa kweli ila hatuzingatii au hatu jali!

Yote uliosema mleta mada nayashudia maana mimi nakutana nayo mara nyingi ila sijali!
Itabidi binafsi nizidishe tahadhari ,asante pia.
 
Ni mara ya tau nakutana na uzi kama huu na zote zinaelezea madhara ya moja kwa moja ya hivi vinywaji!
Inaweza kusa tatizo ni kubwa kweli ila hatuzingatii au hatu jali!

Yote ulio sema mleta mada nayashudia maana mimi nakutana nayo mara nyingi ila sijali!
Itabidi binafsi nizidishe tahadhari ,asante pia.
Ni kweli tahadhari ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom