Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
DAKIKA YA 89, KAMATI KUU YA CHADEMA 0 MH MDEE 5
Na Elius Ndabila
0768239284
Ingekuwa ni mchezo wa Soka ningeweza kusema hivyo kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA 0 na Mh Mdee 5, hasa baada ya press yake ya leo.
Mtakubaliana nami kuwa Majibu ya Mh Mbowe juu ya Wale Wabunge wa Viti Maalumu 19 yalijaa hamaki kubwa hivyo wengi kufikiria kuwa Mh Mbowe alisoma akiwa amesha leo. Taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa baada ya kamati kuu kujadiliana kwa zaidi ya saa 15.
Mh Mdee ambaye amezungumza leo, amezungumza very techinic. Amezungumza na kujibu maswali kwa ustadi mkubwa huku akiwa ametulia. Ameonyesha wazi kuwa yeye na wenzake ni zao la CHADEMA na hawawezi kukihama. Amesema hata kama hawakubaliani na matokeo hawawezi kukataa kwenda bungeni wakati ni haki yao.
Amesema Bunge ndipo mahali pekee pa kwenda kutolea kero zao na si kukataa kwenda. Zaidi amesema anapinga utaratibu wa chama chao kuwafukuza na hivyo yeye na Wenzake watakata rufaa na hawataomba radhi. Pigo lingine alipojibu swali la kuhusu Nasurt amesema akaulizwe DPP, Bwana Jera au Mahaka.
Mh Mdee anasema “Nimekuja kuongea ili kutuliza haya mambo maana sio makubwa saana, niliamua kukaa kimya ila naona uongo unasambazwa na ukiach uongo usemwe bila kutoa neno inafanya Watu waamini.
Kuna Watu wanasema tunakuja kuunga mkono juhudi, niwaambie tu Mimi nitaendelea kubaki CHADEMA na naamini na wenzangu bado wataendelea kubaki CHADEMA, sisi ni CHADEMA kindakindani, niwahakikishie Wana-CHADEMA Nchi nzima, Halima mnayemfahamu ni yuleyule.
Mh Mbowe alizungumza akiwa ametoa mishipa usoni, na amekunja sura mithili ya mtu aliyepigwa na kitu chenye ncha kali, lakini leo anajibiwa na Mh Mdee akiwa anacheka na kutabasamu, huku akipiga makombora ambayo yanasambaratisha kabisa hoja zenye hasira za CC ya CHADEMA.
Mh Mdee anasema kuwa “Tuliitwa kuhudhuria Kamati Kuu Nov 25, Mimi nilipata barua jioni kwa njia ya simu, Matiko hakupata wengine kila Mtu alipata kwa muda wake,Nov 26 tulimuandikia barua Katibu Mkuu tukimuomba asogeze kikao mbele japo kwa Wiki moja, kutokana na ile presha. Tulitaka twende kwenye kikao huku hasira zetu zikiwa zimepungua kidogo maana press ya Katibu aliongea mazito, tukaomba Wiki moja mbele, pili kulikuwa na uhamasishaji wa Watu kuja kutupiga mawe na mayai viza wakidai ni Wasaliti ndio maana tuliomba muda.
Kwa hoja hizi tu chache, ninaweza kumalizia kwa kusema Kamati kuu ya CHADEMA imefungwa magoli matatu tena ya Visigino na Mh Mdee. Na msumari wa mwisho ni kwa akina Mama aliosema walikuwa wakitoa matamko kwa kuwa walikuwa wameona fursa kwa jicho la tatu.