Dakika ya 89: Freeman Mbowe 0 vs Halima Mdee 5

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
DAKIKA YA 89, KAMATI KUU YA CHADEMA 0 MH MDEE 5

Na Elius Ndabila
0768239284

Ingekuwa ni mchezo wa Soka ningeweza kusema hivyo kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA 0 na Mh Mdee 5, hasa baada ya press yake ya leo.

Mtakubaliana nami kuwa Majibu ya Mh Mbowe juu ya Wale Wabunge wa Viti Maalumu 19 yalijaa hamaki kubwa hivyo wengi kufikiria kuwa Mh Mbowe alisoma akiwa amesha leo. Taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa baada ya kamati kuu kujadiliana kwa zaidi ya saa 15.

Mh Mdee ambaye amezungumza leo, amezungumza very techinic. Amezungumza na kujibu maswali kwa ustadi mkubwa huku akiwa ametulia. Ameonyesha wazi kuwa yeye na wenzake ni zao la CHADEMA na hawawezi kukihama. Amesema hata kama hawakubaliani na matokeo hawawezi kukataa kwenda bungeni wakati ni haki yao.

Amesema Bunge ndipo mahali pekee pa kwenda kutolea kero zao na si kukataa kwenda. Zaidi amesema anapinga utaratibu wa chama chao kuwafukuza na hivyo yeye na Wenzake watakata rufaa na hawataomba radhi. Pigo lingine alipojibu swali la kuhusu Nasurt amesema akaulizwe DPP, Bwana Jera au Mahaka.

Mh Mdee anasema “Nimekuja kuongea ili kutuliza haya mambo maana sio makubwa saana, niliamua kukaa kimya ila naona uongo unasambazwa na ukiach uongo usemwe bila kutoa neno inafanya Watu waamini.

Kuna Watu wanasema tunakuja kuunga mkono juhudi, niwaambie tu Mimi nitaendelea kubaki CHADEMA na naamini na wenzangu bado wataendelea kubaki CHADEMA, sisi ni CHADEMA kindakindani, niwahakikishie Wana-CHADEMA Nchi nzima, Halima mnayemfahamu ni yuleyule.

Mh Mbowe alizungumza akiwa ametoa mishipa usoni, na amekunja sura mithili ya mtu aliyepigwa na kitu chenye ncha kali, lakini leo anajibiwa na Mh Mdee akiwa anacheka na kutabasamu, huku akipiga makombora ambayo yanasambaratisha kabisa hoja zenye hasira za CC ya CHADEMA.

Mh Mdee anasema kuwa “Tuliitwa kuhudhuria Kamati Kuu Nov 25, Mimi nilipata barua jioni kwa njia ya simu, Matiko hakupata wengine kila Mtu alipata kwa muda wake,Nov 26 tulimuandikia barua Katibu Mkuu tukimuomba asogeze kikao mbele japo kwa Wiki moja, kutokana na ile presha. Tulitaka twende kwenye kikao huku hasira zetu zikiwa zimepungua kidogo maana press ya Katibu aliongea mazito, tukaomba Wiki moja mbele, pili kulikuwa na uhamasishaji wa Watu kuja kutupiga mawe na mayai viza wakidai ni Wasaliti ndio maana tuliomba muda.

Kwa hoja hizi tu chache, ninaweza kumalizia kwa kusema Kamati kuu ya CHADEMA imefungwa magoli matatu tena ya Visigino na Mh Mdee. Na msumari wa mwisho ni kwa akina Mama aliosema walikuwa wakitoa matamko kwa kuwa walikuwa wameona fursa kwa jicho la tatu.
 
Mbona ccm mnahangaika sana na ya chadema, huo upendo kwa chadema mmeutoa wapi ? Au ndio hata shetani hujifanya kuwa malaika wa nuru
Mdee keshasema mnamjua vizuri hajanunuliwa hatonunuliwa wala hawawazii kununuliwa kwao hongo hawaijui. Sijui umempata hapo au unavunga?

Kila kitu CCM pambania chama make sawa sio kuwazia ccm kila tukio ccm hamkosoani na kurekebishana nynyi kwa nyingi bila kuitaja CCM
 
CHADEMA imajaa wanachama wajeuri na wenye viburi Sana yani mtu anavuliwa uanachama halafu bado yeye bado anajiita mwanachama na amevaa magwanda ya chama kabisa.

Muulizeni jasusi mbobevu kilichompata alivyofukuzwa kwenye kile chama Cha lumumba.

Episode ya CDM bado inaendelea, stay tuned!
 
Mdee keshasema mnamjua vizuri hajanunuliwa hatonunuliwa wala hawawazii kununuliwa kwao hongo hawaijui. Sijui umempata hapo au unavunga?

Kila kitu CCM pambania chama make sawa sio kuwazia ccm kila tukio ccm hamkosoani na kurekebishana nynyi kwa nyingi bila kuitaja ccm
Sasa kwa akili hata za chekechea, ulitegemea aseme kanunuliwa, kapewa pesa mkuu?
 
Ya ngoswe aachiwe ngoswe! Wote hao wamechanganyikiwa baada ya Kata funua ya “NEC”
 
Mdee keshasema mnamjua vizuri hajanunuliwa hatonunuliwa wala hawawazii kununuliwa kwao hongo hawaijui. Sijui umempata hapo au unavunga?

Kila kitu CCM pambania chama make sawa sio kuwazia CCM kila tukio CCM hamkosoani na kurekebishana nynyi kwa nyingi bila kuitaja CCM
Lini nyie mmekuwa na upendo kwa halima mdee na hao wenzake? Si nyie ndio mlikuwa nawavunja mikono na kuwasimamsha kuingia bungeni. Haya hawajanunuliwa ila kamati kuu ya chama imewafuta. Sasa nyie mnataka nini?
 
Mnahangaika sana, yaani mlitegemea mambo ya ajabu ajabu kutoka kwa Halima, sasa mnabadili gear, frankly Halima amewakatisha tamaa kabisa na ile chenga ya mwili, mlitegemea Chadema ndiyo kusmbaratika, Chadema wachama wake na wapenzi wao ni kutoka moyoni. It is loyalty Vs evil, hawa 19 are just embracing the devil, CCM. There is time to sleep with the devil in order to finish it, CCM mmekwisha kwa sababu wanachama wenu wengi ni pesa na unafiki
 
Mtu anaenda kukata rufaa halafu unasema Halima 5?

Bure kabisa. Hufai kwa uteuzi na hiyo namba yako ya simu!
Wewe ni mtu mwenye heshima sana hapa jukwaani. Bila shaka wapo wanaonufaika na michango yako!

Ongeza ujuzi wa kukabiliana na hoja kinzani au fikra kinzani pasi na jazba!

Ni mtazamo wangu tu. Samahani kama umekwazika
 
Lini nyie mmekuwa na upendo kwa halima mdee na hao wenzake ? Si nyie ndio mlikuwa nawavunja mikono na kuwasimamsha kuingia bungeni. Haya hawajanunuliwa ila kamati kuu ya chama imewafuta.. sasa nyie mnataka nini ?
Mimi sipo CCM wala CHADEMA nasimamia penye akili ( uelewa) na sio upatukaji na maubabe ya kijinga, napenda mtu mwenye point Nzuri.
 
Yule dada Halima ni kichwa!!

Cheki Hekima sliyoitumia kwenye press yake!!

Anaijua miiko ya Chama, anaijua katiba ya Chama, lakini pia ni mwenye kutumia tahadhari kubwa kuwaonyesha kina Mbowe & Co hawana marifa, amewaonyesha kwamba, Hekima Yao inasoma ziro katika kutatua mambo magumu na hatarishi

Chadema inakosa vitu vidogovidogo Sana aisee
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom