mimi jibu ni [Yes]
hapa bado. wakati wote nilijiona mkosaji. kila nikimuona nasahau hata nimsalimieje..nilijikuta nikiomba msamaha bila kosa. simu, niliweka mlimo wa peke yake. ilikua ikilia mapigo ya moyo yanakwenda kasi hadi mwili unakosa nguvu. wakati mwingine nilishindwa kupokea simu yake.
yote hayo yalinikuta na zaidi. ajabu kwamba sikuweza kuwa nae. niliumia sana nilipogudua kuwa,, yeye alikua hayupo kwangu.. yeye alikuwa kawaida sana na pengine huenda alihisi kuwa najipendekeza kwake. sasa ni miaka nane 8 imepita bado sijapona.. huwa wakati mwingine sauti yake inanisumbua..... ninayo furaha nikujuze kuwa, sijaweza kumchukia mpaka sasa. bali naamini sikua chaguo lake. kupendwa raha sana.
ningebahatika kuwa nae sijui ingekuwaje,,