Dada zetu wengi wanapambana kuolewa na wazungu tu

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Kwa muda Sasa toka nihamie kufanya kazi katika bank Moja hapa Kariakoo. Katika pitapita zangu nikakutana na Dada mmoja akanialika kwenye party ya vikoba ili niwashauri namna ya kuweka pesa na kupata mikopo.

Sasa nilifika kwenye party Ile nikakuta waume wanne na wasichana umri wa Kati kama 50 hivi. Kwa haraka niliona wote wazuri sana na wengi wanafunguo za Magari.

Kadri muda wa party unavyoenda nikajitosa kupata mrembo mmoja wa kunipa company. Nikachambua wote Hatimaye nikakutana na mrembo mmoja hana kasoro.

Nikamwita akaja kwa shauku sana. Nikaropoka nimekuchagua akanijibu na Mimi nimekuchagua.
Tukacheeka sana. Baada akaleta kiti na beer zake tukaanza kupiga soga.

Ilikuwa kama zogo wadada wanabishana na kuchambana ghafla tukaingia kwenye mazungumzo mazito tukaondoka kwenye Dunia yao ya party tukawa kama wawili tu katika faraga. Tukaongea mengi sana.

Aliniambia kama tunaweza kuwa wapenzi lakini hatutaoana kwani ana date mtu mkubwa serikalini pia Hana mpango wa kuolewa na mtu mweusi anataka mzungu. Nilishangaa sana nikaona kama amajiwekea mitihani mkubwa sana. Nilini atakutana na huyo future husband wake? na ni wapi? . Hivyo Vyote hajui.
Anataka mzungu mpaka atakapokuja.
Tukamaliza party siku ile lakini bado nikawa naona kama ni dream kubwa sana kwake. Maana ni rahisi kuweka dreams ya kupata mali au nyumba lakini kukutana na mtu naona ni ngumu sana. What if wazungu wote wamkatae?

Kuna siku nilikuwa nungwi kwenye mapumziko yangu nasoma vitabu mbali mbali nilikutana na Dada mwingine tena nae aliniambia amekuja kisaka Mume mzungu.

Leo nimekutana na mwanaDada mrembo mwembamba amzuri akaniambia ametoka Mwanza Kuja Dar kusaka wazungu.

Mbona Mimi naona kama ni dreams kubwa sana kwa mtu kujiwekea kwenye Maisha?
 
Nilikuwa nayasoma mtandaoni mpaka pale college mate alipoolewa na mzungu miaka kama 65+ hivi. Nikasema yote heri, sema yule manzi alikuwa kiazi sana hafundishiki sio kwa lecturer wala vipanga darasani. Alafu mzuri ila muda wote anawaza wanaume wampe mtaji afungue duka la nguo
 
Aloooooooo.
ukikutana na wengine wa dizaini hiyo wajibu kuna wanaume pia wanaotafuta wazungu wa kuishi nao.
kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kupanga hivyo wewe usipate tabu kwa maisha aliyoyachagua yeye.
muhimu ni kuzingatia haki yako.
 
Bora wewe ulikutananae kwenye vikoba mie nilikuwa kwenye jumuhia ya hao wazungu Kuna mdada wakiafrika kaja na babu wake wakizungu,anamshauri mwanamke mwenzake (nae ni muafrika) atafute bwana lakizungu kama yeye!!! Nilitamani kulia nikamng'ate pua! Maana alikuwa anapeperusha njiwa..

Wanawake hawaaminiki anytime anyplace anaweza kukushitukiza na pigo zito ambalo hujawahi kuliona toka uzaliwe!
 
Bora wewe ulikutananae kwenye vikoba mie nilikuwa kwenye jumuhia ya hao wazungu Kuna mdada wakiafrika kaja na babu wake wakizungu,anamshauri mwanamke mwenzake (nae ni muafrika) atafute bwana lakizungu kama yeye!!! Nilitamani kulia nikamng'ate pua! Maana alikuwa anapeperusha njiwa..

Wanawake hawaaminiki anytime anyplace anaweza kukushitukiza na pigo zito ambalo hujawahi kuliona toka uzaliwe!
Pole
 
Back
Top Bottom