Nashindwa kuielewa tabia ya huyu dada kwangu mimi!

Kelsey

JF-Expert Member
Aug 9, 2023
254
474
Kuna ofisi moja nimekuwa nikienda tangu siku nyingi kupata huduma, katika hiyo ofisi receptionists ni wanawake. Katika hao receptionists kuna mmoja kila akiona nikizungumza na mwenzake yeyote hapo kwenye desk lao la reception anaonesha ishara za kukasirika. Ingawa kila nikifika tu ofisini kwao kupata huduma ananichangamkia ila inaonekana hapendi nikiongea zadi na wenzake hata mbele yake tena akiwa anasikia ninachozungumza na mwenzake yeyote ni mazungumzo yanayohusu huduma za ofisi yao tu na sio kitu kingine.

Hivi karibuni nilifika ofisini kwao huyu dada kupata huduma na baada ya hapo nikumuita pembeni huyu dada kumuomba tuongee na baada ya story za fupi nikamuomba namba zake za simu ila akataa kabisa kunipa namba zake akaniambia yeye ni mke wa mtu yaani ameolewa, nikaenda tena baada ya kama wiki moja kupata huduma, baada ya huduma nikamuita pembeni kama siku ile kumuomba namba akakataa kwa mara nyingine kunipa namba akinisisitiza yeye ni mke wa mtu hawezi kutoa namba.

Lakini sasa najiuliza, je kama kweli huyu dada ni mke wa mtu, KWASABABU gani aoneshe kutopenda mimi kuongea na mwenzake yeyote ofisini kwao? Nimejiuliza sana, je huyu dada huwa anapenda sana wateja wote awahudumie yeye tu, yaani ni kama ni mbinafsi? Na je anawafanyia kama mimi kwa kukasirika wateja wengine wanaofikaga hapo wakihudumiwa na mwenzake ambaye yuko nae reception?

Naombeni msaada wenu wadau kunifafanulia juu ya tabia ya huyu dada, je ni tabia gani hii mbona sielewi! cc Robert Heriel Mtibeli, Da'Vinci
 
Kuna ofisi moja nimekuwa nikienda tangu siku nyingi kupata huduma, katika hiyo ofisi receptionists ni wanawake. Katika hao receptionists kuna mmoja kila akiona nikizungumza na mwenzake yeyote hapo kwenye desk lao la reception

Naombeni msaada wenu wadau kunifafanulia juu ya tabia ya huyu dada, je ni tabia gani hii mbona sielewi! cc Robert Heriel Mtibeli, Da'Vinci
Wanawake sio watu mkuu.
 
Sijaelewa kama mahusiano ni ya kiofisi ..why namba majibu aseme mke wa mtu??

Ina maana hakuna wateja WA ofisi aliewapa namba??...

Jina lako nilifikiri Kelsea ...nilikuwa nasoma narudia tena sielewi kabisa ...
Mahusiano yaliyopo ni ya kiofisi tu. Mimi ni mwanaume. Hata mimi sijamuelewa
 
Back
Top Bottom