Huyu dada/mama amegusia pale pale wengi wetu tunapopaona kua katika sera CCM bado ni safi na CDM ni wanaharakati tu wasio na uzoefu wowote wa kuongoza dola huku wakipita huku na huko kudanganya tui watz...
CDM imekua ghafla na bila ya kujitayarisha kisawa sawa kwenye demokrasia ya ndani na maslahi binafsi ya kiuongozi.. ni chama kidogo lakini kutokana na kukua kwa umaarufu wake maradufu ndani ya miaka kama mi5 hivi kimejikuta overwhelmed with its own success na kuonyesha nyufa zote za chama kikongwe...
katika uchambuzi yakinifu, CDM ina hatari ya kuzorota na kufa kabisa kama itashindwa uchaguzi wa 2015 kwa % nyingi na CCM. kama nilivyoonyesha hapo juu licha ya umaarufu kushindwa kwa kishindo kutaifanya CDM na safu yake ya uongozi "kuangalia wapi walikosea na nani anahusika na makosa hayo" yaliyosababisha kushindwa vibaya wakati wakiwa na imani ya kua umma mkubwa wa watz upo nao (nikimaanisha umma mkubwa not necessarily wapiga kura), kutokana na hulka ya ubinafsi ya wanasiasa waliopata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi "wafanya makosa watakataa kuwajibika" na hapo mgogoro mkubwa wa kiuongozi utauikumba CDM na kutishia uhai wake.
ukitilia maanani kua umoja miongoni mwa viongozi muhimu wa kitaifa wa CDM umeshikiliwa na imani 2 ya kua 2015 kuna uwezekano mkubwa wa kushika dola. kushindwa kwa CDM kutakua mwisho wa umoja na mshikamano baridi huu wa hawa viongozi na wengi wao kuanza kujiuliza maswali ya kubadilisha dira yote, mipango na taswira ya chama kupata nguvu mpya ya kisiasa. Mabadiliko mara nyingi hutishia watu wenye maslahi yao na hapo hali haitokua shwari kwa CDM.
CDM lazima washinde uchaguzi wa 2015 ili iendelee kuwepo, au watone down ambitions zao na waelekeze nguvu kwenye kujenga sustainable opposition kwa kuongeza namba ya wabunge, wavutie zaidi viongozi na vijana toka vyama vingine hususan toka CCM, otherwise mwisho wa CDM kama chama kikubwa cha upinzani ni 2015.