Daah! Bora ningesoma

Daah! Bora ningesoma

ELIMU ELIMU ELIMU. Bila elimu sijui ningekuwa nafanya nini muda huu
Mimi binafsi elimu imenifikisha mahali ambapo kwenye jamii yangu hakuna aliyewahi kupafikia. Hata mimi sikuwahi kupawazia kama ningefika.

Elimu imenikutanisha na watu ambao nilikuwa naishia kuwaona kwenye TV

Shikamoo elimu.
 
Vyote vinatumika

Japo wengi wanasoma ili waje waajiriwe

Mambo ya kujiajiri yanataka mitaji, ambayo wengi wanakosa
Bila elimu bora hakuna mafanikio halisi. Planet earth inaongozwa na elimu, hapa Tanzania naona watu wazima tumeanzisha kampeni ya kipumbafu ya kubagaza elimu ionekane sio kitu si lolote matokeo yake tunalipoteza hili taifa kwa hii misimamo ya kipumbafu ya akinadotomagali
 
Dunia ya sasa elimu sio dili kuna wana kibao wamesoma wapo kitaa hawajui kesho yao inakuwa vipi na mfumo wa elimu bongo ni mbovu mno
Elimu haiwezi kuacha kuwa dili, inatakiwa ujue elimu na kuelimika ni vitu viwili fofauti. hao unao sema wamesoma ni kweli wamesoma na hakuna anayekataa eti hawajasoma ila ukweli mwingine ni kwamba wamesoma ila hawajaelimika.

Kuna watu mtaani hawajaenda shule kupata formal education ila wameelika katika nyanja mbalimbali na wanatengeneza pesa kupitia elimu walizozipata bila kwenda shule kusomea. Hii haimaanishi watu wasiende shule kusoma namaanisha watu waende shule wasome warudi wakiwa wameelimika na sio kurudi na vyeti tu.
 
Asubuhi na mapema nakutana na huu ujumbe. Naomba kuuliza kama usingesoma na kupata kibarua ulichonacho sasahivi ungekuwa wapi na unafanya nini?

Au na wewe ungesema Bora ningesoma😌
View attachment 3557298
Mie Bora nisingesoma tu
Nikikumbuka vile viboko vya mwalimu wa hesabu nikikumbuka nilivyopambana nikawa nashika namba moja darasani halafu leo hii nimeishia kuwa muuza majeneza hapa Dodoma!
Nachoka kabisa mimi😀
 
Mithali 4:13 Inasema mshike sana elimu usimuache aende zake maana huo ndo uzima wako.

Ni kweli kwa sasa changamoto ya ajira ipo ila ukweli nawaambieni Kuna utofauti kati ya aliyesoma na ambae hajasoma. Mfano Kuna siku Home Feni ilikuwa haifanyi kazi nikapigiwa simu na mimi sio fundi na sina knowledge ya ufundi.

Kwa vile chuo nilijifunza kwamba youtube Kuna kila Aina ya tutorial basi nikachecki solution yake nikawapigia simu nikawaambia wachukue fimbo yoyote wazungushe hio feni manually, baadae ikaanza kufanya kazi.

Kusoma ni kuwa na uwezo wa kumaster mazingira yako ajira ni extra tu.
 
Asijua Kusoma Barua Anaitembeza Kutwa



Elimu Haina Mbadala
 
Back
Top Bottom