Daah Ajira ngumu aisee!

Daah Ajira ngumu aisee!

Wajamen wana JF...nimetumia kila mbinu kupata kazi sijafanikiwa. Nakumbuka nilikua nikitoa copies za vyeti na CV nyingi sana...kama zaidi ya 200....nikaanza kua nazitembeza na kibegi changu cha kisomi huku nikiwa nimevalia nguo safi nadhifu za kiofisi. Nilikua nikiandika barua nyingi sizizokua na address ya ofisi..but kila nilivyoona bango la ofisi...nilikua nikikopi address yake na kwenda pemben na kupaste kwenye barua mojawapo kati ya nilizokua nikiziandaa.

Kasheshe ilikua jinsi ya kuingia pale ofisi husika. Mlangoni getin mara nyingi nilimkuta mlinzi..."unashida gani?..unaenda kumuona nani?..sign daftari hili" hayo ni baadhi ya maswali niliyokua nikiulizwa. Nikifanikiwa kumpita japo wengine walikua wakinizuia katukatu...nakumbana na mtihani wa mwisho wa pale kwa sekretari wa boss..ofisini hapo. Hawa walikua wakiniuliza.."unashida gani?..ya binafsi au ofisi?"..ukisema ya kiofisi imekula kwako...watakuuliza "una appointment letter??"..ukisema huna basi ndio hutaweza kumuona boss. Kwani mimi nia yangu kubwa ilikua ni kumeet na mwenye mbwa tu. Mwanzon ilikua ngumu sana kumet nao sana kwani swali la kusema nna appointment na boss lilinishinda sana..nikawa nafel na kujikuta sipati fursa ya kumuona. Nikabuni mbinu ingine.



Safari hii...nilivyokua nikuulizwa na sekrtar kama ni shida ya binafsi au kiofisi...nilisema shida ya binafsi.....nikawanaulizwa tena. Unafahamiana na boss?..nikawa nawajibu kwa konfidens..ndio. Ananiliza jina langu kisha boss anapigiwa simu...ngriiiii...halo boss Hamidu anataka kukuona...anasema wewe mnafahamiana..ni ndugu yako....boss nikawa namsikia anasita kidogo...Hamidu???..anyways mruhusu aingie.



Kimbembe ni kwa boss....it was funny...maboss wengi walifurahi sana...nikawa nawachana..nawaambia nyie ni wagumu sana kuwapata...na sometimes CV zetu hazifiki kwenu..ma PS au walinzi wanazichana. Niliongea yangu...wengine walikaribisha chai au chakula na wengine walinipa pesa ya nauli. But mwishoni niliwaomba Busness card zao. Hapa nilipo nina zaidi ya 120 ya kadi. Wengi walinipa matumaini kua "kama wakitangaza watanikonsider"..wengine waliniambia nisubiri baada ya miezi kadhaa...etc etc blah blah kibao.


Nilikua nikiwasiliana nao kwenye namba zao za simu kuwakumbushia. Nikawa napigwa danadana tu..longolongo kibao. Wengine wakanichenjia niwape cash kidogo...na bahati mbaya sikua na chochote.



Nilikua nikitembea sana...maofisi mbali mbali ya posta..vingunguti na kote dar es salaam. Nilikua nikituma pia kwa njia ya posta barua zingine.


Nilifanya hivyo kwa njia ya analogia na digitali.Nimetuma mails nyingi sana za kazi. Hapa sasa ivi nilikua naangalia. .toka 2009 hadi sasa nimeshatuma mails 1999+ za maombi ya kazi bila mafanikio.


Nikajiunga na linkedin website...hapa nikameet na proffessionals wengi sana....maboss kibao...nikawanawatumia CV zangu direct. I mean..nikisikia nafasi imetangazwa...naingia linkedin..nawasiliana na mtu ambae anafanyakazi sehemu hiyo. So nakua like natuma maombi mara 3...kwa huyo jamaa...kwa mails ya ofisi na sanduku la ofisi.


Kuna mtandao pia nikifakiwa kuuona..unaitwa CEOs roundtable...hapa nilimeet na ma CEOs na kuwatumia resumes zangu bila mafaniko.



Kuna tovuti za kutafutia kazi kama zoomtanzania...proffessionalapproach. ...kazibongo...vijanatz...pataajira..kokorikoo...britermonday...mwananchi etc etc..nimekua nikizitembelea kila mara mpaka tovuti za nchi za uarabu.




Ilifikia kipindi niliamua kwenda kutafuta kazi mining...kwenda kusotea kazi. Kukaa pale getini na CV zako na kusubiria mzungu wa kampuni flani apite uchonge nae unampa CV lakin hola. Nakumbuka nilipata kazi Barrick Buzwagi kama Security Officer..siku ya kwenda kuripoti nikaambiwa jina halionekani. Daah




Kiukweli nimetumia mbinu mbali mbali sana. Hata kubeba matofali pale kona ya msamvu niliwahi kubeba pia. Niliumia mikono sana na mwili kukosa nguvu. Tofali moja kubeba ni sh. 25.



Sasa waweza kujiuliza elimu yangu ipo vipi?..kiukweli nna elimu ya kawaida tu. Nilisoma seminary na kupata alama nzuri tu za fom 4 na six vilevile....chuo nikasoma mara mbili....advanced diploma ya accounts na postgraduate diploma ya accounts.



Nasikia tu watu wanasema vijana rudini vijijini kwenu mkalime....wengine...vijana mjiajili.....hapa ndo nachanganikiwa kabisa. Naanzajeanzaje sasa kwa mfano...ebu tuambiane wadau....wayeyote aliyepitia situatiation kama yangu aseme katokaje. Kwani hapa nipo nipo tu kama lipicha la michelini au lisanamu la bunduki la pale posta. Nimeganda....

Mwambie Mungu asante kwakuwa mwezi huu hautapita bila mimi kupata kazi. I promise mwezi hautapita bila kupata kazi mkuu
 
Ah!! Mbona tayari una ajira. Watu wote hao uliofahamiana nao kwenye mishe za kuomba kazi ni mtaji tosha kukiingiza kipato. Imagine ungekuwa unawauzia vest,socks,pyfume au mashuka. Amka bro.

mtaji wa kununua hayo mashuka,vest na perfum umempa ww au???
 
Amina. Mungu mwezi huu hautapita bila
Mimi kupata kazi. Amina Amina...naamini kwa njia ya Yesu nitapokea muujiza wangu.
 
kaka seminari ipi? pengine wewe ulizaliwa uwe padre, kaongee na farther wako wa miito akupe ushauri wa ziada
 
Wazo zuri kaka. But wito sina wa kua padri@ darubini
 
NiPM nikupe tacts za kutafuta kazi. Mimi nimepita huko ila baada ya kujua nifanyeje naogelea ziwani, madimbwi swimming pool, hadi kwenye ndoo ukiniwekea maji nachapa mwende.

Kikubwa zaidi ni kuwa na subra, Mungu anatoa kwa muda wake. Ki binadamu unaona kama ni mazingaombwe, usikate tamaa we endelea kuomba, acha kuhesabia cv ulizowahi tuma, JIPE MOYO.


Mkuu PM tena? Hili ni tatizo la wengi, mwaga jamvini bwana
 
Tuanzie kwenye basics

1. Asilimia ngapi ya mombi yako unaitwa?(<5%)- jaribu kufanyia kazi cv yako, cover letter na viambatanishi....makosa madogo madogo kama spelling error, fonts kachumbari, alignment, pengine na GPA labda ni Dwarf inatosha kum-turn off mtu kukuita....Google how to write a CV and cover letter....Match your CV to the particular JD +organisation...hakuna kitu kama 'one size fits all'. Umesema unaandika barua nyingi unapaste address tu?? Really...

2. Unaomba kazi sehemu gani au kazi zipi?? kwa sifa zako compee ni kubwa sana hasa za watu ambao hata wamekuzidi sifa kwa hivyo sitegemei unaomba kazi za 'accounts tu' maana UDSM+UDOM+IFM+TUMAINI+MUCOBBS+TIA+IAA+MYSORE+BANGALORE+CARDIFFF+ ETC...zinatoa watu wa kutosha kila mwaka wenye sifa na wamejipanga kwa hiyo....expand your grazing field to maximise your niche.......

3. Unaitwa kwenye usaili na kisha unakosa kazi kwa asilimia zipi? je tatizo ni kuwa huna vipawa vya usaili....fanyia kazi confidence, kujieleza vizuri, social skills, body language, research kazi unayoomba na kampuni husika vizuri, onyesha enthusiasm za kutosha hata kama fake, drop a bomb yaani, unawaacha watu dah huyu jamaa katu-impress lazima tumchukue......ongea lugha moja na anayekusaili....tell them what they want to hear......ingia google jipige msasa haswa....invest muda kiasi na resources kama internet+vitabu au hata usaili usio wamalengo kama rehersal ya kazi zenyewe....

4. Unaitwa kazini unagomea maslahi madogo? hapa inabidi ujiangalie kuwa huna hata uzoefu wa kazi, watu hawafahamu utendaji wako kwa hiyo unaweza kuanza mdogo mdogo baada ya mwaka unahamia pengine au utaongezewa kima cha masurufu....

5. Unatafuataje kazi? usilenge tu advertised job.....update profile kule recruitment agency watu wakuone wakuite kwenye intial assessment ushindwe mwenyewe....career tab kwenye 'company portal' etc...

6....

7...
 
Asante kwa ushauri mzuri. Ila hayo mawazo mara nyingi nayafuatilia sana. Naweza kukupa mgano wa Interview mbili nilizowahi kuhudhulia na kushuhudia maksi zangu.

1. Niliwahi kufanya usahili org flani...tulianza kwa usahili wa written...walikua wakitoa majibu palepale ili uweze kwenda next oral interview. Na nakumbuka kwa written niliscore zaidi ya wote..95%....na kwa oral nilifanya vizuri sana. Mpaka ikafikia wakati wa kwenda kuanza kazi. ..then nikaambiwa jina langu halionekani.


2. Ya pili nilifanya taasisi flani...tulifanya written kwanza....na ulitakiwa kupata zaidi ya 50% ndio uingie oral interview. Majibu yalitoka siku hiyo...na tukasomwa watu wote tutakao fanya oral interview siku tatu baadae huku jina langu likiwemo. Siku ya kuripoti kwenye oral..unaambiwa. ...ulisomwa kimakosa..wanakuangalizia wanasema uliskoo 49.5%.....

Nakubaliana na mawazo yako sana. Na nitayafanyia kazi
 
Kwa kuongezea..kama umesoma uzi wangu vizuri. Nimeandika. ..na kutolea mfano kwa mwaka 2012...from January to Dec...kila mwezi nilikua nikiitwa mara moja au mbili. I mean..ilivyokua ikifika jumamosi lazima nipate call ya interview mpaka zingine nikawa nashindwa kwenda kutokana na kukosa nauli.



Kuna file nilitengeneza kwa ajili ya kuhifadhi barua zote nilizokua nikijibiwa kwa njia ya posta.Barua hizi ni zile zilizojibiwa na sehemu nilizopeleka maombi bila sehemu husika kutangaza ajira. So nyingi nilijibiwa.."kwasasa hatuna nafasi uliyoomba. .jaribu kuomba mara utakapoona tumetangaza"

Nilikua nikizihifadhi na zimenisaidia sana kwani...nikiona wametangaza nafasi..naambatisha na hiyo copy kuwaonyesha kwamba niliwahi kuomba kazi kwao na docs zingine.



Kwa mwaka huu toka uanze nimeitwa mara mbili....January na march tu. Mpaka sasa sijaitwa sehemu yeyote koz nafasi nyingi zilitangazwa May na June ndo tunasubiri majibu.
 
Ukifafanua zaidi utakuwa umesaidia wengi aisee

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
....mpaka kuitwa kwenye interview it means...cover letter..cv na viambatisho wamevikubali au sio?..na kwa interview hizo zote...sidhan kama konfidens utashindwa kua nayo..koz sio kitu kigeni kwako. Anyways.....theres a saying goes by.."God's time is the best"....Oneday Yes who knows!!!
 
Shida unaonyesha una nyodo kuna sehemu umeandika unataka kuonana na mwenye "Mbwa" hizo ni nyodo Mungu apendi. back to the tpic pole sana kwa changamoto zinazokukuta usikate tamaa maisha ndivyo yalivyo. jaribu ata kuomba kufanya kazi kwa kujitolea kwenye baadhi ya makampuni.
 
Mkuu acha tu, hata sie ambbao tumemaliza vyuo juzi ni majanga tu. Kwa mfano mimi professional yangu ya banking matatizo tu, hata ukipata nafasi wanataka wakupe gross ya laki 4, kweli? Hii nchi we acha tu!
 
Nisamehe bure...ni lugha tu na niliandika nikiwa na uchungu sana.
 
Back
Top Bottom