Daah Ajira ngumu aisee!

Daah Ajira ngumu aisee!

ila umepata experience ya kutosha kwa kuzunguka na kupiga saund walinzi na ma PS wa mabosi. Hongera mkuu .
 
kaka wewe ni kama mimi lakini unajua nilifanyajeeeeeeee? rudi kijijini kaweke mambo sawa kuna mambo hayajaa kaa vizuri kwako, sali sanaaaaaaaaaaaaa, na tengeneza mahusiano mazuri na mungu, Punguza chapa chapa. all the best God is greater

Mimi nilisota tangu mwaka 2006 mpaka 2013 ndio nikapata kazi nzuri tu, kampuni kubwa, full marupurupu everybody is asking me how come you got a job that company

any way ushauri wangu wa kwanza ufuate Tengeneza mahusiano mazuri na Mungu


Mambo gani ya kukaa sawa kijijin mkuu?
 
pole! umenikumbusha mbali sana.sio peke yako uliyepitia hayo.wapo wengi na mie mmoja wapo.Nakushauri nenda na cv zako office mbalimbali ukaombe kujitolea bure na uwasisitize hautaki mshahara zaidi ya pesa ya nauli na lunch tu.nilijaribu strategy hiyo imenisaidia sana,japo sijafika nilikodream kufika lakini kwa njia hiyo nimepata kazi sehemu na sio sawa na kukaa home.
 
Unajua ma-ujanja ni kusifu na kumwabudu Mungu. Kipengele hiki watu wanakiona cha kishamba au kilichopitwa na wakati lakini kinafungua vifungo vingi sana, kinakupa kazi unayotaka, kinakuwezesha wewe kuishi kwa kujiamini.

Wacha kumchanganya mwenzako wakati yupo serious.nadhani ungemwelekeza vizuri aanzeje kumsifu na kumwabudu Mungu ili afanikiwe usiassume kwamba anajua.unataka kuniambia watu wote wanaojua kumsifu na kumwabudu Mungu hawajapitia hiki kipindi?wamepita wengi,mie mmoja wapo. Na ufahamu kumsifu na kumwabudu Mungu sio maujanja.Tunamsifu na kumwabudi kwa sababu Mungu ametupa neema hiyo.
 
Nashukuru kwa mawazo yenu jamani. Kuhusu issue za Mungu....yeye ndio kimbilio langu siku zote katika maisha yangu. Najitahidi sana kusali...nimesoma seminary...na kwasasa najitahidi sana kuutafuta uso wa Mungu na faraja kubwa kutoka kwake.
 
duuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Pole jamaa nahisi utakua umelogwa kasafishe nyota na pia onana na jacob stephen (jb) mtengeneze movie itauza kinoooma!!!!!!!!!!!!!!
 
naku PM. unipe strategy.
NiPM nikupe tacts za kutafuta kazi. Mimi nimepita huko ila baada ya kujua nifanyeje naogelea ziwani, madimbwi swimming pool, hadi kwenye ndoo ukiniwekea maji nachapa mwende.

Kikubwa zaidi ni kuwa na subra, Mungu anatoa kwa muda wake. Ki binadamu unaona kama ni mazingaombwe, usikate tamaa we endelea kuomba, acha kuhesabia cv ulizowahi tuma, JIPE MOYO.
 
Pole sana ndugu na ukishapata urudi utuambie ulitumia mbinu gani ya mwisho.
 
Ndugu kb52, mimi sio nabii lakini ninaona kitu kikubwa kiko mbele yako ambacho kukifikia haihitaji uwe umeajiriwa bali umejiajiri.

Nitarudi badae kidogo..
 
Mambo ni magumu kama unavyosema lakini kamwe hautakiwi kukata taama na kurudi nyuma katika utafutaji wa kazi kwani huwezi jua kesho nayo ni siku so inabidi kukubali kuendelea kuvumilia na kujifunza kukubaliana na hali halisi ilivyo
 
Mku I hope ulishafanikiwa kwenye hii safari yako ya matumaini.
 
Embu mtafute tajiri wa Tanzania mzee bakhresa hasa mwezi huu ajira utapata
 
Itakuwa keshapata kazi nzuri yenye mshahara na marupurupu mazuri mkuu kb52 manake ni muda sasa umepita...mkuu kb52 njoo utuambie umefanikiwa au laa!!?
 
mim hua najichomeka tu kwenye interview hta km sijaitwa ila lazma niwe nimeomba hyo kazi,nlizamia kazi flan mahali nkaulizwa jina lako nani nkawambia akasema mbna halipo nkamwambia sijui sasa akaniambia msubiri kwanza hr aje,alivokuja nlimwambia mlinipigia simu mbna tena mnasema jina langu halipo,badae akasema nisubiri mwishoni nlipga interview mkuu japo sikufanikiwa wakati mwingine unatakiwa kuwa mafia tu.
 
Wajamen wana JF...nimetumia kila mbinu kupata kazi sijafanikiwa. Nakumbuka nilikua nikitoa copies za vyeti na CV nyingi sana...kama zaidi ya 200....nikaanza kua nazitembeza na kibegi changu cha kisomi huku nikiwa nimevalia nguo safi nadhifu za kiofisi. Nilikua nikiandika barua nyingi sizizokua na address ya ofisi..but kila nilivyoona bango la ofisi...nilikua nikikopi address yake na kwenda pemben na kupaste kwenye barua mojawapo kati ya nilizokua nikiziandaa.

Kasheshe ilikua jinsi ya kuingia pale ofisi husika. Mlangoni getin mara nyingi nilimkuta mlinzi..."unashida gani?..unaenda kumuona nani?..sign daftari hili" hayo ni baadhi ya maswali niliyokua nikiulizwa. Nikifanikiwa kumpita japo wengine walikua wakinizuia katukatu...nakumbana na mtihani wa mwisho wa pale kwa sekretari wa boss..ofisini hapo. Hawa walikua wakiniuliza.."unashida gani?..ya binafsi au ofisi?"..ukisema ya kiofisi imekula kwako...watakuuliza "una appointment letter??"..ukisema huna basi ndio hutaweza kumuona boss. Kwani mimi nia yangu kubwa ilikua ni kumeet na mwenye mbwa tu. Mwanzon ilikua ngumu sana kumet nao sana kwani swali la kusema nna appointment na boss lilinishinda sana..nikawa nafel na kujikuta sipati fursa ya kumuona. Nikabuni mbinu ingine.

Safari hii...nilivyokua nikuulizwa na sekrtar kama ni shida ya binafsi au kiofisi...nilisema shida ya binafsi.....nikawanaulizwa tena. Unafahamiana na boss?..nikawa nawajibu kwa konfidens..ndio. Ananiliza jina langu kisha boss anapigiwa simu...ngriiiii...halo boss Hamidu anataka kukuona...anasema wewe mnafahamiana..ni ndugu yako....boss nikawa namsikia anasita kidogo...Hamidu???..anyways mruhusu aingie.

Kimbembe ni kwa boss....it was funny...maboss wengi walifurahi sana...nikawa nawachana..nawaambia nyie ni wagumu sana kuwapata...na sometimes CV zetu hazifiki kwenu..ma PS au walinzi wanazichana. Niliongea yangu...wengine walikaribisha chai au chakula na wengine walinipa pesa ya nauli. But mwishoni niliwaomba Busness card zao. Hapa nilipo nina zaidi ya 120 ya kadi. Wengi walinipa matumaini kua "kama wakitangaza watanikonsider"..wengine waliniambia nisubiri baada ya miezi kadhaa...etc etc blah blah kibao.

Nilikua nikiwasiliana nao kwenye namba zao za simu kuwakumbushia. Nikawa napigwa danadana tu..longolongo kibao. Wengine wakanichenjia niwape cash kidogo...na bahati mbaya sikua na chochote.

Nilikua nikitembea sana...maofisi mbali mbali ya posta..vingunguti na kote dar es salaam. Nilikua nikituma pia kwa njia ya posta barua zingine.

Nilifanya hivyo kwa njia ya analogia na digitali.Nimetuma mails nyingi sana za kazi. Hapa sasa ivi nilikua naangalia. .toka 2009 hadi sasa nimeshatuma mails 1999+ za maombi ya kazi bila mafanikio.

Nikajiunga na linkedin website...hapa nikameet na proffessionals wengi sana....maboss kibao...nikawanawatumia CV zangu direct. I mean..nikisikia nafasi imetangazwa...naingia linkedin..nawasiliana na mtu ambae anafanyakazi sehemu hiyo. So nakua like natuma maombi mara 3...kwa huyo jamaa...kwa mails ya ofisi na sanduku la ofisi.


Kuna mtandao pia nikifakiwa kuuona..unaitwa CEOs roundtable...hapa nilimeet na ma CEOs na kuwatumia resumes zangu bila mafaniko.

Kuna tovuti za kutafutia kazi kama zoomtanzania...proffessionalapproach. ...kazibongo...vijanatz...pataajira..kokorikoo...britermonday...mwananchi etc etc..nimekua nikizitembelea kila mara mpaka tovuti za nchi za uarabu.

Ilifikia kipindi niliamua kwenda kutafuta kazi mining...kwenda kusotea kazi. Kukaa pale getini na CV zako na kusubiria mzungu wa kampuni flani apite uchonge nae unampa CV lakin hola. Nakumbuka nilipata kazi Barrick Buzwagi kama Security Officer..siku ya kwenda kuripoti nikaambiwa jina halionekani. Daah

Kiukweli nimetumia mbinu mbali mbali sana. Hata kubeba matofali pale kona ya msamvu niliwahi kubeba pia. Niliumia mikono sana na mwili kukosa nguvu. Tofali moja kubeba ni sh. 25.

Sasa waweza kujiuliza elimu yangu ipo vipi?..kiukweli nna elimu ya kawaida tu. Nilisoma seminary na kupata alama nzuri tu za fom 4 na six vilevile....chuo nikasoma mara mbili....advanced diploma ya accounts na postgraduate diploma ya accounts.

Nasikia tu watu wanasema vijana rudini vijijini kwenu mkalime....wengine...vijana mjiajili.....hapa ndo nachanganikiwa kabisa. Naanzajeanzaje sasa kwa mfano...ebu tuambiane wadau....wayeyote aliyepitia situatiation kama yangu aseme katokaje. Kwani hapa nipo nipo tu kama lipicha la michelini au lisanamu la bunduki la pale posta. Nimeganda....

njoo kwenye maombi kanisa la eagt kwa mchungaji katunzi mtoni mtongani karib na reli jtano had jmoc saa kumi jpili saa 3 asubuh kama wamekutupia uxhawi utaondoka kwa jina ka yesu nimeona dada mmoja alikuja miaka 5 anasaka job kumbe wamemroga asipate kazi baada ya maombi sasa yuko kazini mungu anaweza usikate tamaa njoo kwa maombi munguyupo.
 
Back
Top Bottom