Daah Ajira ngumu aisee!

Daah Ajira ngumu aisee!

Kweli ajira ni ngumu sana siku hizi, lakini pia vipi kuhusu hizi lugha za "Mavimavi" huwa unazitumia wakati wa usaili??
 
mmmh kaka mbona kama story vile??? halafu inaonekana unajiamini kupitiliza na umejawa na hasira napata ugumu kukuamini...
 
Dogo pole sana jaribu kuomba kazi shule za kata ninajua una uwezo wa kufundisha Commerce na Accounting vizuri.
 
Pole sana mkuu,sasa hebu jaribu hii ya pccb ilotangazwa leo,Muombe Mungu na uamini kwa cfa na vigezo ulivyonavyo utaipata,ukikwama popote ni email kwa msaada wa maelekezo ya namna ya kuomba na nn kinatakiwa,
 
Dah! Wadau pole sana ndugu kwa yalokukuta huo mcba ni wa vjana wote tatizo mwenye nacho ndo anaongezewa asienacho hapat kabisa ila usikate tamaa ipo siku utayashinda tu mungu akuongoze katika hilo
 
muda wote naheshimu mawazo yako na nashukuru kwa mchango wako. Labda kuongezea hapo...nilikua nikituma maombi yangu kwa nafasi zilizokua zikitangazwa na pia nilikua nikituma na kuomba kazi hata sehemu ambazo hawajatangaza nafasi za ajira ili mradi tu cv yangu ibaki katika kumbukumbu zao na kuweza kupata kazi kiurahisi pindi watakapohitaji watu.


Kwa mwaka 2012...nilikua nikiitwa kwenye interview kila mwezi from january to december...na kila mwezi nilikua naitwa interview 2...na sijafanikiwa. Mfano... Tcaa...nssf..toll...tanesco...african barrick....yani sehemu mbali mbali..ofisi kubwa kubwa. Nilikua nabadili aina mbali mbali ya cv na cover letters...ambazo zilinifanya niitwe mara kwa mara. Nina vyeti vya kujitolea..sehemu kama bungeni..dodoma...mpwapwa district council..etc etc...ninavyeti vya safety...fire..firstaid....chemical and synide...leaderships..etc etc ambavyo nilivipata ktika trainings....so utaona ni kwa jinsi gani nilivyo. Hapa sasa ninachofanya ni kuomba kazi na zile za kuvolunteer. But majibu hayatoki...mfano za sumatra...tra..tpdc..iita..etc etc ambazo zilitoka mwezi majuz...majibu yakunaja mavimavi tu....we acknowledge sijui nini nn...yani mavimavi tu wananijibu. Na hasira sana hapa kaka.



kaka bopa hata uitwe mimi tangu 2010 nimitwa mara moja ila naamini mungu ipo siku
 
Mungu ni mwema ikifika cku nac tutapata tu
MVUMILIVU HULA MBIVU.
 
lakini sasa mimi huwa najiuliza hivi waizara ya kazi inafanya kazi gani coz mm sioni wanacho kifanya kweli kweli kwa sabaabu wanashindwa kujibu ajira mpya kulingana na wahitimu mbalimbali.coz kila mara wanapangiwa bajeti je hiyo bajeti wanayo pangiwa inaenda wapi
 
kuhusu pale TRA...tulikua zaidi ya watu 3000....waliochaguliwa ni wachache sana hawakufika hata mia. Mimi sikufanikiwa.
 
Pole sana kb52 kila jambo lina wakati wake. Tusichoke kumuomba Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Duuuh nguvu zote zimeniisha walosoma tu ndo ivi sie wa shule za kata si ndo majanga jamani uwiii...
 
Polisi sitaki kabisa kuwasikia. Jamaa waliwahi kunivuta korodan zangu. Sitaki kabisa hata hilo jina. Mavi mavi tu wale

Aaaaah! mkuu kumbe tatizo lako unachagua kazi kumbe, kkwa mwenendo huo ungezaliwa enzi ya Nyerere basi.
 
Wajamen wana JF...nimetumia kila mbinu kupata kazi sijafanikiwa. Nakumbuka nilikua nikitoa copies za vyeti na CV nyingi sana...kama zaidi ya 200....nikaanza kua nazitembeza na kibegi changu cha kisomi huku nikiwa nimevalia nguo safi nadhifu za kiofisi. Nilikua nikiandika barua nyingi sizizokua na address ya ofisi..but kila nilivyoona bango la ofisi...nilikua nikikopi address yake na kwenda pemben na kupaste kwenye barua mojawapo kati ya nilizokua nikiziandaa.

Kasheshe ilikua jinsi ya kuingia pale ofisi husika. Mlangoni getin mara nyingi nilimkuta mlinzi..."unashida gani?..unaenda kumuona nani?..sign daftari hili" hayo ni baadhi ya maswali niliyokua nikiulizwa. Nikifanikiwa kumpita japo wengine walikua wakinizuia katukatu...nakumbana na mtihani wa mwisho wa pale kwa sekretari wa boss..ofisini hapo. Hawa walikua wakiniuliza.."unashida gani?..ya binafsi au ofisi?"..ukisema ya kiofisi imekula kwako...watakuuliza "una appointment letter??"..ukisema huna basi ndio hutaweza kumuona boss. Kwani mimi nia yangu kubwa ilikua ni kumeet na mwenye mbwa tu. Mwanzon ilikua ngumu sana kumet nao sana kwani swali la kusema nna appointment na boss lilinishinda sana..nikawa nafel na kujikuta sipati fursa ya kumuona. Nikabuni mbinu ingine.

Safari hii...nilivyokua nikuulizwa na sekrtar kama ni shida ya binafsi au kiofisi...nilisema shida ya binafsi.....nikawanaulizwa tena. Unafahamiana na boss?..nikawa nawajibu kwa konfidens..ndio. Ananiliza jina langu kisha boss anapigiwa simu...ngriiiii...halo boss Hamidu anataka kukuona...anasema wewe mnafahamiana..ni ndugu yako....boss nikawa namsikia anasita kidogo...Hamidu???..anyways mruhusu aingie.

Kimbembe ni kwa boss....it was funny...maboss wengi walifurahi sana...nikawa nawachana..nawaambia nyie ni wagumu sana kuwapata...na sometimes CV zetu hazifiki kwenu..ma PS au walinzi wanazichana. Niliongea yangu...wengine walikaribisha chai au chakula na wengine walinipa pesa ya nauli. But mwishoni niliwaomba Busness card zao. Hapa nilipo nina zaidi ya 120 ya kadi. Wengi walinipa matumaini kua "kama wakitangaza watanikonsider"..wengine waliniambia nisubiri baada ya miezi kadhaa...etc etc blah blah kibao.

Nilikua nikiwasiliana nao kwenye namba zao za simu kuwakumbushia. Nikawa napigwa danadana tu..longolongo kibao. Wengine wakanichenjia niwape cash kidogo...na bahati mbaya sikua na chochote.

Nilikua nikitembea sana...maofisi mbali mbali ya posta..vingunguti na kote dar es salaam. Nilikua nikituma pia kwa njia ya posta barua zingine.

Nilifanya hivyo kwa njia ya analogia na digitali.Nimetuma mails nyingi sana za kazi. Hapa sasa ivi nilikua naangalia. .toka 2009 hadi sasa nimeshatuma mails 1999+ za maombi ya kazi bila mafanikio.

Nikajiunga na linkedin website...hapa nikameet na proffessionals wengi sana....maboss kibao...nikawanawatumia CV zangu direct. I mean..nikisikia nafasi imetangazwa...naingia linkedin..nawasiliana na mtu ambae anafanyakazi sehemu hiyo. So nakua like natuma maombi mara 3...kwa huyo jamaa...kwa mails ya ofisi na sanduku la ofisi.


Kuna mtandao pia nikifakiwa kuuona..unaitwa CEOs roundtable...hapa nilimeet na ma CEOs na kuwatumia resumes zangu bila mafaniko.

Kuna tovuti za kutafutia kazi kama zoomtanzania...proffessionalapproach. ...kazibongo...vijanatz...pataajira..kokorikoo...britermonday...mwananchi etc etc..nimekua nikizitembelea kila mara mpaka tovuti za nchi za uarabu.

Ilifikia kipindi niliamua kwenda kutafuta kazi mining...kwenda kusotea kazi. Kukaa pale getini na CV zako na kusubiria mzungu wa kampuni flani apite uchonge nae unampa CV lakin hola. Nakumbuka nilipata kazi Barrick Buzwagi kama Security Officer..siku ya kwenda kuripoti nikaambiwa jina halionekani. Daah

Kiukweli nimetumia mbinu mbali mbali sana. Hata kubeba matofali pale kona ya msamvu niliwahi kubeba pia. Niliumia mikono sana na mwili kukosa nguvu. Tofali moja kubeba ni sh. 25.

Sasa waweza kujiuliza elimu yangu ipo vipi?..kiukweli nna elimu ya kawaida tu. Nilisoma seminary na kupata alama nzuri tu za fom 4 na six vilevile....chuo nikasoma mara mbili....advanced diploma ya accounts na postgraduate diploma ya accounts.

Nasikia tu watu wanasema vijana rudini vijijini kwenu mkalime....wengine...vijana mjiajili.....hapa ndo nachanganikiwa kabisa. Naanzajeanzaje sasa kwa mfano...ebu tuambiane wadau....wayeyote aliyepitia situatiation kama yangu aseme katokaje. Kwani hapa nipo nipo tu kama lipicha la michelini au lisanamu la bunduki la pale posta. Nimeganda....

kaka wewe ni kama mimi lakini unajua nilifanyajeeeeeeee? rudi kijijini kaweke mambo sawa kuna mambo hayajaa kaa vizuri kwako, sali sanaaaaaaaaaaaaa, na tengeneza mahusiano mazuri na mungu, Punguza chapa chapa. all the best God is greater

Mimi nilisota tangu mwaka 2006 mpaka 2013 ndio nikapata kazi nzuri tu, kampuni kubwa, full marupurupu everybody is asking me how come you got a job that company

any way ushauri wangu wa kwanza ufuate Tengeneza mahusiano mazuri na Mungu
 
Kama alivyosema mchangiaji aliyepta rud nyuma na ujiulize nia wap unamekosea kama ni kwa wazee ama huna mahusiano mazur na mungu wako cs somtym tunakuwa wepes wakulaum ama kufikia kuhisi umelogwa kumbe kuna mahali hatukutenda ipaxavyo pasipo cc binafsi kujua
 
ila umepata experience ya kutosha kwa kuzunguka na kupiga saund walinzi na ma PS wa mabosi. Hongera mkuu .
 
Back
Top Bottom