D.light ni kampuni ya utapeli na bado Serikali inafumbua macho

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Hii kampuni ya D.light ilikuja na mfumo wa solar ambayo ina kifaa maalumu cha kulipa ili kuweza kupata huduma ya umeme.

Baadae wakaja na simu ambazo unalipa kwa siku,wiki,mwezi ikiambatana na kianzio kulingana na simu ilivo au kifaa chochote.

Hii kampuni sikuweza kuifahamu vizuri ila nimekuja kuigundua huku mikoani ndio imejikita kwa utapeli wao.

Kampuni hii utumia njia za mawakala wanao sambaza vifaa vyao kuaminisha kuwa wanasaidia watu kwa mikopo ya kulipa kidogo kidogo.

Kitu ambacho kimenishangaza kuhusu mkopo wa simu ambazo kwa sasa wanatumia simu za samsung series za A.

Kuna simu iliyonifanya kuwagundua ni samsung A02.

Simu hii ili kupata unaweka kiasi cha elfu 80 kama kiambatanio na fomu iliyo ya kijanja ambayo ineleza kuwa kwa siku kulipa 1600,kwa wiki 12000,mwezi 48000 na mwaka 664000.

Jambo ambalo watu waliopo mikoani wameshindwa kutambua wakiona vitu kwa njia ya mkopo wanashindwa kuelewa mkopo huu unathamani gani.

Kwa mwezi unatakiwa kulipa 48000 ila mwezi wao walio weka ni ndani ya siku 20. je kuna mwezi unasiku 20.

Thamani ya simu au vifaa vyao kwenye kurudisha mkopo vinaendana na masharti ya mikopo ambayo serikali imeweka.

Simu hii samsung A02 dukani ukiwa na cash inafika 247000 mpaka 320000 inategemea na eneo.

Kwa kampuni ya D.light ndani ya mwaka 664000 na ukiingia mkataba wanakulazimisha kuwa unaweza kulipa nusu.

Malalamiko yaliyopo ! kwa watu waliongia kupata huduma za d.light ni kwamba unajikuta ukiwa mdeni mpaka thamani ya kitu kufikia milioni.

Malipo kulipa mkopo kutojulikana,thamani za uongo kwenye vifaa ndani ya riba mfano simu inauzwa 320000 lafu ulipe ndani ya mwaka 664000 na kila mwezi ni siku 20 uwe umelipa 48000. Ukishindwa siku 20 tambua uhesabiwi ni mwezi wanakata kama siku wanazo zijua wao na mnaanza upya tena kama siku 20 upya.

Hakuna fidia na kama umeshtuka hawa kubali kuwajibika wala lolote na kukuletea mkono wa sheria.

Serikali tunaomba kuangalia makumpuni yanao kuja na kutumia kinga ya kusema wamesajiliwa kama kigezo cha kuaminika.

Hii kampuni ni ya utapeli
 
Labda ni mradi wa mtu wa serikalini, wao vibali vya kufanya kazi wamevitoa wapi?
 
Yaani kila kitu Kiko wazi unasaini mwenyewe kwa hiari yako halafu unakuja kupiga miyowe humu
 
Achana nayo, fanya mambo yako. Wao nao wako kazini mkuu.
Anayeona itamsaidia, atakopa na atalipa.
 
Mleta mada ni mpambavu

Simu zimejaa tele kkoo

Kitu gani kilichomkimbiza kuuvaa mkenge huo
 
Ndo mkopo huo ulivyo kitu kikubwa ni kuwapa Elimu kuhus mkopa faida na hasara

Mi nakumbuka mzazi wangu kipindi cha nyuma sana aliwahi kwenda bank kukopa million 8 , alitakiwa kulipa deni ndani ya miaka 5 jumla ni million 12. Anarudisha million 4 nusu ya mkopo
 
Back
Top Bottom