X men
Member
- Dec 26, 2021
- 11
- 23
Je serikali haioni jinsi kampuni ya Milvik ikishirikiana na Tigo wanavyofanya dhuluma kwa wananchi??
Kampunj ya tigo imekua ikifanya uhamasishaji wa wananchi kujiunga bima mkononi ambapo mnufaika hukatwa 5500 kila mwezi na endapo ataumwa yeye au wanufaika wengine wa familia yake kisha wakalazwa basi Tigo na Milvik watamlipa mwanachama elfu 40 kwa kila siku aliyolazwa.
Zikiwa pesa ndogo ndogo hizi wanalipa ila peleka madai makubwa hapo ndiyo utajuta. Mke wangu (mteja wao) mwaka 2021 alilazwa na mtoto MUHIMBILI zaidi ya miezi 3 na aliporuhusiwa aliwatumia Milvik document zote walizohitaji ili ku process malipo.
Shida ikaanza wakaanza kumsumbua mke wangu kwamba eti wameenda MNH ku verify hizo taarifa ila hawajaziona, tulipowaluzoa kwahiyo hizo document ni fake wakasema sio fake ila kule muhimbili hazipo, tukawaambia sasa kama sio fake kwanini hamtaki kulipa, tukataka watuambie sehemu walipoenda ku verify wakakataa, wakamtaka mke wangu (tunaishi Tabora) atoke Tabora arudi Muhimbili kuwaomba waandike medical report ingine yenye kuonyesha ile ya awali ni sahihi, tukawaambi suala la verification ni la kwenu sio mteja mbona huu ni usumbufu na hizi gharama za safari nani ata cover, kwanini nyie msitumie vyanzo zaidi ya kimoja ku verify, je mmefika kwa mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji ambaye yeye ndiye msimamizi na barua zinapitia kwake??
Je mmefika kwa madaktaribwa jengo la watoto kuwauliza , je mmeendea ku verify wapi??! Wakasema wao washaenda ku verify na hawawezi enda tena. Kwakua MILVIK walikuwa wanapaswa kulipa zaidi ya milion ilibidi tukope fedha kurudi hadi MNH kuwaelezea, majibu waliyotupa ni kwamba sisi sio wa kwanza hiyo kampuni inasumbua sana wananchi, wakasema tuwapigie pale simu ili waende MNH wakaonane na Mkurugenzi wa Huduma, Milvik wakakataa kwakusema madai yetu yalishafungwa, tulijaribu kuwasiliana na Tigo ila hakuna walichotusaidia ikabidi turudi Tabora bila kufanikisha na tukawa tumeingia hasara.
Tuliandika barua ya malalamiko TIRA na Muhimbili ila hadi leo miaka 3 hatujawahi kujibiwa!! Huu ni utapeli mkubwa unaofanywa na Tigo na Milvik kwa Watanzaia ambao unapaswa kuchukuliwa hatua. Tulitamani kuwafungulia mashtaka kwa hayo madai, hasara na usumbufu waliotusababishia ila gharama na kukosa msaada kisheria vikatufanya tukubali kudhulumiwa.
ILA NIMEONA NI BORA KULISEMA HILI JAMBO ili wengine yasije kuwakuta!!