ha ha ha na kuna watu wana mitusi kweli kweli...lakini bado wanapokea likes from like minded members...
Huwa nashindwa kuwashangaa....ila nimeshajua humu kuna teams kama za mitandao ya kitoto...si JF MMU ya those days...
Hizo timu za JF ndo zipi? Manake si wengine hata hatuzijui. Au ziko active huko kwenye PM?
Halafu humu ambapo tunatumia majina feki na wengine hata watu ambao tunawasiliana nao kupitia PM tunawapa majina feki, vipi mtu atakunyanyasa kwa jina feki?
Kama mtu humjui hata chembe naye hakujui zaidi ya jina feki la humu, ataweza kweli kukunyanyasa? Kwa mfano, mtu ataanzia wapi kuninyanyasa mimi bila za ammo za ukweli?
Sana sana ataishia kusema (na pengine hata kuamini) mambo ya uongo kabisa - kama NN ni mzee, NN sijui hivi, NN vile.....na hakuna hata kimoja kilicho na chembe ya ukweli. Watabaki ku guess guess tu na kusadiki mambo. I love it that way.
Sasa hiyo nayo inahesabika kuwa ni cyber-bullying? Mimi sidhani.
Na ndiyo maana wengine humu tuko way ahead of the curve. Never give out your 'real you' kwa watu unaozoeana nao humu kwa sababu kwa kufanya hivyo ni kuwapa fimbo za kukuchapia.
Mimi humu nina uhakika kabisa tena wa asilimia 110 hakuna anayenijua na hivyo siwezi kabisa kuwa bullied.
Nadhani watu wanachanganya kati ya trolling na cyber-bullying. Yatokeayo humu mengi huwa ni trolling tu unless watu kweli wawe wanajuana, yaani wameshawahi kukutana ana kwa ana, wanajuana majina yao halisi, na kadhalika.
Zaidi ya hapo, JF imejaa trolls tu na hakuna anayeweza kukabili trolls kama Le Mutuz (with all his vices).