zee_latown
JF-Expert Member
- Feb 21, 2026
- 523
- 927
Habarini ndugu Wanabodi wa JF!
Naenda kwenye kiini cha mada moja kwa moja.
Nina changamoto... hata nikiongea kwa upole na kawaida, wasikilizaji wangu wanadai kuwa nimechukia na nafoka,, yaani nikiongea seriously mfano kwenye jambo nyeti na la msingi, naonekana kama nafoka. Hali hii inanitatiza sana, ukizingatia mimi kiasili ni mtu muungwana na ninayependa watu.
Kuna wakati huko zamani, nilikuwa naongea na bosi wangu... sasa wafanyakazi wenzangu wa pemebni walikuwa wanasikiliza maongezi yetu.. nilipomaliza wakaja wakanishangaa sana wakisema hivi siogopi kumfokea bosi? hili liliniuma sana na ukizingatia mimi nilikuwa naongea kwa upole mno ila in a serious way,kwa sababu jambo lenyewe lilikuwa serious pia
Sasa ninahofia sana hii hali... huenda ikanieletea shida mbeleni hasa ukizingatia kuna nyakati huwa naongea na baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali... isije kuonekana nafoka na nimepandisha sauti, ilhali mimi naona naongea kawaida.
Nafahamu humu kuna wenye uwezo wa kunisaidia utatuzi wa hili. naomba msaada wa hali na mali tafadhali.
natanguliza shukrani zangu.