CWT yasisitiza mgomo upo palepale Jumatatu tar 30/07/2012

Nadhani wewe ni mmoja wa watu mnaofanya kazi huko CWT....hamuwezi kutmia zaidi ya milioni 200 kuhamasisha mgomo wa walimu hali mkijua wiki ijayo shule zinafungwa na mwalimu atatakuwa nyumbani, sasa huo mgomo utakuwa effect gani kwa serikali au wewe ni kilaza hujui hata kufikiria na kuona faida na hasara kwa pande hizi zote mbili...sio unaropoka tu ndugu!

Usidanganye watu. Walimu wakiamua kugoma hata kipindi hiki inawezekana kabisa. Walimu hata wakati wa likizo wanapaswa kuwa mashuleni. Likizo ni kwa ajili ya wanafunzi. Mfano mzuri shule yetu form 4 na 2 wanatakiwa kuendelea na session zao kipindi hiki. Sasa unasemaje timing imekosewa ?

Wahamasishe walimu kushiriki mgomo huu waache uwoga.

Zaidi unaweza kuonana na rais wa CWT ukampa mawazo yako ili usaidie walimu.

Mgomo umefuata utaratibu, inawezekana mgomo umeangukia mahali ambapo si pazuri lakini msiwakatize walimu tamaa.

Huu ukishindikana mgomo baridi unakuja. Tusubiri .
 
Walimu ni kama wanacheza mchezo wa watoto wa kinyumba nyumba, wakijiita baba/mama wangali bado hawajawa wazazi.
Mgomo gani unaanza wiki moja kabla ya kufunga? Kama kuna Mwl. kati yetu hapa aeleze kusudio la kutaka kuichimbisha serikali inayojua keshokutwa tu sensa inaanza.

Walimu wangegome pale darasa la saba, form two, four, six wanapokaribia mtihani wa Taifa, vyuoni wanakaribia UEs.

Kwa sasa tishio liko wapi? Au watakataa kwenda kuhesabu watu (sensa), hawawezi, maana kulingana na kipato chao duni lazima watahesabu wapate ujira.
Je walimu mgomo upo?
 
Kisaka80 bila shaka aliyekutuma kuleta hapa hizi propaganda atakuwa amefurahia kazi zako. Sasa nenda kachukue posho yako ya leo ukawanunulie watoto wake mkate wa leo.

Lakini utambue kwamba mtake msitake mgomo wa walimu uko pale pale hadi serikali itakapokubali kurekebisha stahiki zao kama wanavyodai.

Hizi tilalila mnazopiga hapa ninyi puppets wa serikali hazitaisaidia serikali hata kama itaendelea kutoa vitisho kwa walimu.
 
Last edited by a moderator:
Mod uliyeko zamu unastahili kuwa FIRED, huwezi kuruhusu picha za Mwamvita zivuruge mjadala muhimu wa mgomo. Kumbe ufisadi sio bungeni tu

Hata mimi nashangaa kwanini hazijaondolewa. Sioni tatizo ama kosa walimu kudai nyongeza ya asilimia 100. Nchi hii inazo pesa nyingi,lakini kwasababu ya watawala dhaifu na watawaliwa wazembe zinaliwa na wajanja wachache na wawekezaji feki.
 
Una maanisha shule zinafungwa tarehe 6 august wakati sensa ni tarehe 26 August?
 
Kwanza TZ ni nchi yao pia, sasa wanamgomea nani???!!! Kikwete? CCM? Watafute njia nyingine na siyo mgomo.
 
Kwan umeambiwa ukomo wa mgomo ni lini mpaka uanze kusema hakuna mgomo?kwa taarifa nilizonazo ni kuwa mgomo wao hauna kikomo mpaka kieleweke sasa hiyo mitihani ya taifa si itakuja ama...
 
Kama hujui hizi taratibu bora usikurupuke. Acha Uvivu wa kufikiri kama jina lako lilivyo. au unajitakia umaarufu wa bure? We amekwambia nani kuwa likzo za wanafunzi zinamhusu mwalimu? Mwalimu anakwenda likizo kwa kuomba na kuruhusiwa. Wanafunzi kuwa likizo haimaanishi mwalimu nae yupo likizo. Blah blah nyingine wala hazisaidii!
 
Ninachotaka kukufahamisha ni kuwa ukiwa kiongozi lazima very strategic.....CWT hawawezi kuitisha mgomo uanze baada ya kutoa notice serikalini ya saa 48, tena unatoa notice ijumaa saa 7 si upumbavu huo? ina maana serikali inafanya kazi kufungua ofisi jumamosi na jumapili au?

Ninanachokisema hapa ni kuwa viongozi wa CWT hawana dhamira ya dhati kuwakomboa walimu...wanaitisha migomo ya kishamba kama hii ili serikali ikizuia waseme eti tunaonewa...huo ni ujinga uliopitiliza.

kama kweli wapo stable kwanini wasingeitisha mgomo katikati ya mihula na wanasubiri shule zifunge ndio wajidai kuhamasisha migomo...huo ni udhaifu wa mukoba/CWT...! wanatumia pesa nyingi kwa kazi isiyo na tija? huo ni ujinga.

Ndio maana nasema wajinga ndio waliowao....walimu waaachane na usaanii huu wa Mukoba/CWT.

Unaweza kuwa na hoja lakini kakae chini uilete upya, maelezo yako yanaonyesha umetumwa au unatumiwa
 
muleta topic hii wewe ndiyo fisadi unayetumiwa kuleta habari za uongo hapa.Kama hujawahi kuwa mwalimu ni bora ukae kimya acha walimu wagome.Wewe jiulize mwalim akapandishwa daraja la kazi tangu 2008 hadi leo hii mshahara wake haujabandilishwa na hajawahi kwenda likizo ya malipo hata siku moja akiandika barua za mandai zinakaliwa oifsi za wakurungezi na maafisa elimu.What kind of nation we are trying to build?Walimu bila malipo mazuri watoto wetu watazidi kupata elimu duni..
 
jamani si mwache iyo kesho muone? hivi nyie wakuda mnashida gani sana na mgomo wetu???? sasa na kwataarifa yenu hadi wanafunzi wetu wako nyuma yetu na tunagoma kesho j5 wanaianagia kazini kutusaidia mbona kitaeleweka tu najua sasa hivi serikali inawaza kuacha wanafunzi peke yao shule pasi waalim ni hatari sana ila watakipata wajue kabisa uharibifu wa mali utatke na mambo ya kufanana na hayo.

waaalimu wa sasa hivi tuko na tunataka kieleweke kwamba tuko tumechok bana.

tena kinikosa humu jamvini this week mjue kabsa kwamba nitakuwa mambwepande habr ndo hiyo.
 
Rais CWT ahofia ya Ulimboka
• Awataka walimu waanze mgomo kesho

na Waandishi wetu


amka2.gif
HOFU ya kutekwa, kuteswa na kupelekwa katika msitu wa Mabwepande kama ilivyokuwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, imeanza kumtesa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mukoba alisema amekuwa akipata vitisho vya kumzuia kushiriki kwenye mgomo walioupanga kuuanza kesho, lakini amedai vitisho hivyo havimzuii kuendelea na mkakati wa kutafuta haki za walimu.
Mukoba alisema hata kama atapelekwa katika msitu huo uliojipatia umaarufu mkubwa kwa kutumiwa kuendesha vitendo vya utesaji na uuaji, bado ukweli utabaki palepale kuwa walimu wana madai ya msingi ambayo yamekuwa yakipigwa danadana na serikali.
Alibainisha kuwa watu wanaofikiri kuwa paka anaweza kugeuka simba wanajidanganya kwa sababu haki ya mtu haiwezi kuminywa na mtu yeyote hata kama ana madaraka makubwa.
“Unapomuona paka nyumbani kwako huwezi kumwita simba …eeh hata kama napata vitisho havitanifanya kuacha kutimiza majukumu yangu, hata kama mimi nitapata matatizo wapo watakaoendelea na kupigania haki za walimu, kwakuwa huwezi kuzuia na kumnyamazisha kila mtu, hasa katika masilahi ya taifa,” alisema.
Alisema anaamini kuwa kile kilichomtokea Dk. Ulimboka hakitaweza kumtokea yeye kwa sababu watetezi mbalimbali na mikataba mingi ya kimataifa ipo na inasimamiwa kikamilifu na watu wasiopenda haki za watu zipotee.
Mukoba alisema serikali haina haja ya kutoa vitisho kwa walimu kuwa mgomo wao ni batili bali iueleze umma ni kesi gani na namba ngapi iliyopo mahakamani inayozuia mgomo huo.
“Serikali imezoea kupiga porojo za kisiasa, porojo zao hazituzuii wala kutunyamazisha kuendelea na msimamo wetu wa kuanza mgomo kesho,” alisema.
Fomu za serikali
Serikali imesambaza fomu kwa maofisa elimu wa wilaya ikiwataka wazigawe kwa walimu na wajaze haraka ili wabaini wanaounga au kupinga mgomo huo.
Fomu zimeandikwa maneno ya ‘Haraka Sana’, zina sehemu mbalimbali ambazo zinamtaka mwalimu kuandika namba yake ya hundi, kuunga mkono mgomo au kutounga mkono.
Kwa mujibu wa Mukoba, sehemu ya namba ya hundi imewekwa mahususi kuwakata mishahara walimu watakaoshiriki kwenye mgomo huo.
“Nawaomba walimu waendelee na msimamo wao, maana wasiposimama imara kutetea haki zao hakuna atakayewasaidia, mgomo huo hautaathiri utumishi wao, kwa kuwa umezingatia sheria,” alisema na kukiri kuwa kutakuwa na vitisho na propaganda nyingi kutoka kwa waajiri.
Kuhusu suala la serikali lililopo mahakamani, Mukoba alisema hatua hiyo haiondoi taratibu za mgomo na kuongeza kwamba serikali isitake kutumia kivuli cha mahakama kukandamiza haki za walimu ambao wamezingatia taratibu na sheria zote za nchi katika mgomo huo.
Juzi CWT kilitangaza mgomo rasmi huku kikikamilisha taratibu za mgomo kwa kupiga kura kuunga au kukataa mgomo huo, ambapo kati ya walimu 183,000 walimu 153,848 sawa na asilimia 95 ya walimu waliunga mkono kufanyika kwa mgomo.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali na CWT kushindwa kufikia makubaliano katika siku 30 walizoipa kuanzia Juni 25 mwaka huu.
Madai makubwa ya walimu katika mgomo huo, mbali na malimbikizo ya madeni yao ya huko nyuma, pia wanataka ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho za kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55 na walimu wa masomo ya sanaa asilimia 50 na posho za mazingira magumu asilimia 30.
Mara baada ya tishio hilo la CWT, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi ya Rais (Ikulu), kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo, juzi ilitoa taarifa kupinga mgomo huo kwa madai kuwa ni batili, kwa sababu kuna kesi mahakamani inayozihusu pande hizo mbili.
“Kwa sasa shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa Julai 27, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika mahakamani na mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne Julai 31, 2012 saa sita mchana ili kuiwezesha mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi. Kwa hiyo mgomo huo si halali kwa vile shauri hilo bado liko mahakamani,” ilisema.
Maandalizi mikoani
Mkoani Mbeya, Kaimu Katibu wa CWT Mkoa wa Mbeya, Felix Mnyanyi, alisema mazungumzo kati ya walimu na serikali yameshindikana baada ya kuthibitishwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na kesho walimu watagoma.
Mkoani Mara, Mwenyekiti wa CWT wilayani Bunda, Francis Ruhumbika, amewataka walimu wote kushiriki kwenye mgomo huo kwa kutokwenda kwenye vituo vyao vya kazi.

 
“Serikali imezoea kupiga porojo za kisiasa, porojo zao hazituzuii wala kutunyamazisha kuendelea na msimamo wetu wa kuanza mgomo kesho,” alisema Rais wa CWT.Pia amesema serikali itaje namba ya kesi iliyopo mahakamani ili wasitishe mgomo.

sOURCE TANZANIA DAIMA JUMAPILI
 
Una maanisha shule zinafungwa tarehe 6 august wakati sensa ni tarehe 26 August?

Shule zinafunga tarehe 3 Agosti, halafu eti wanagoma kudai haki zao wakati tayari mock na mitihani ya kufunga shule imeshafanyika.
Ndipo tunauliza mgomo gani wakati wa likizo? Kwa mwendo huu walimu hawataja fanikiwa katika madai yao.
 
Hata kama ni siku mbili wagome inatosha kufikisha ujumbe kwa serikali kwamba siyo sikivu kama inavyojiita
 
KUNA HAJA YA KUENDELEA KUWA NA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)?



Kimsingi, chama chochote cha wafanyakazi kinapaswa kusimamia, kwa ukamilifu na kwa ufanisi mkubwa, maslahi ya wanachama wake. Hakipaswi kufungamana na serikali na kufumbwa mdomo na hivyo basi kuwa kama mbwa mkubwa abwekaye sana lakini asiye na meno.


Chama cha Walimu Tanzania kinakosa sifa nyingi za kuwa mwakilishi wa wanachama wake katika sehemu zao za kazi. Badala yake chama hiki kimekuwa na muda mwingi wa kusajili wanachama wapya lakini hakithubutu, kwa juhudi kubwa, kuwaelimisha wanachama wake juu ya wajibu na haki zao kazini kupitia mikutano na semina. Kimekuwa ni mkusanyaji tu wa ada zao na kujihusisha na mambo ya starehe na kujenga majumba kinyume cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004 kifungu cha
72 (3) (e). Kwa kifupi chama hiki kimemezwa na serikali na kulala usingizi wa pono.


Chama cha Walimu Tanzania kina mapungufu yafuatayo ya kiutendaji:


1. Wanachama wamenyimwa fursa na demokrasia ya kutoa mawazo na kutatua matatizo yao kwa njia ya mikutano katika vituo vyao vya kazi kwa sababu katiba ya CWT, toleo la tarehe 18 Desemba 2009 kifungu cha 11 ( a) – (c), haiwapi madaraka wawakilishi kuitisha mikutano katika sehemu zao za kazi;


2. Chama hakina sifa za kutosha za kujishughulisha kwa umakini na ufanisi mkubwa kutatua matatizo ya wanachama wake kwa sababu kina eneo pana mno la utendaji wake wa kazi. Chama kinahudumia wanachama wengi wa aina tofauti na wenye mahitaji yanayotofautiana kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, chama kinashughulika na walimu wa shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo. Inafaa chama hiki kubadilishwa na kuwa “Shirikisho la Vyama vya Walimu Tanzania”. Kwa mantiki hii sauti za vilio vya walimu wa shule za chekechea, sekondari na vyuo ni hafifu kuliko ya zile za shule za msingi zenye idadi kubwa ya wanachama katika CWT;


3. Mara nyingine chama kimekuwa kinaweka wawakilishi wenye sura ya maslahi ya mwajiri. Kwa mfano, siyo sahihi kwa msimamizi wa kituo cha kazi, yaani Mkuu wa Shule, Mwalimu Mkuu au Mkuu wa Chuo kuwa mwakilishi wa chama cha wafanyakazi kwakuwa hana sifa za kuwatetea na kuwawakilisha wanachama wa chama hicho;


4. Chama hakina uwazi katika matumizi ya pesa za wanachama na wasio wananachama wake. Kwa mfano, makato ya ada ya uwakala (agency fee) ya wasio wanachama yanapaswa kuwekwa katika akaunti tofauti na ile ya wanachama wake kutokana na kifungu cha 72 (3) (e) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/ 2004; na


5. Mwisho chama hiki kimeshindwa kufanikiwa katika migomo yake kwa vile kimefungamana mno na serikali.

wanasheri CWT ni kina Mabere Marando and Mr. Gabriel Mnyele; nani asiyejua ukigeugeu wa marando ata CHADEMA WANAMJUA,
 
MOD uliyeko zam DHAIFU xana unawezaje kuacha picha za huyo mwanakwenda kuingilia mjadala muhimu kuhusu harakat za ukomboz
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom