bongospecialist
New Member
- Nov 5, 2010
- 4
- 0
Heshima kwako Kizomanizo.
Mkuu asante sana umejaribu kutoa majibu ambayo wengi wamekwepa kwa makusudi.Kuna kipindi unafika unawashangaa watu hapa Jamvini habari wanazotaka ni kusifia CHADEMA tu ukikosoa utapachikwa majina ya ajabu ajabu.Mleta mada kaomba CV za wabunge wa CHADEMA kama unajua unatuambia kama hujui unakaa kimya.
Mkuu wangu CV ya Godbless Lema ni ya hovyo kuliko nilivyofikiri mwanzo.Jamaa alishindwa kufaulu mtihani wa form II kuingia form III.Ana cheti cha lugha ya kiingereza miezi 3 KIMAHAMA mkabala na Golden Rose.Mkuu mambo mengine labda ajiendeleze baada ya kuwa mheshimiwa kazi hii namwachia kamanda PakaJimmy anaweza kumshauri.
Mkuu ni kweli Lema amechaguliwa kwasababu watu wameichoka CCM si kwa ubora wa kujenga hoja hata kidogo.
Nasikitika sana kama kuna watanzania wanajiita wasomi hata hawajui maana ya CV wanafikiri elimu ndiyo Cv elimu ni sehemu tu ya Cv Kushindwa Form II haina maana huyu ni mtu asiyefaa katika jamii. Mchango wake kwenye jamii ndiyo kitu cha maana na ndicho cha kuangalia kwenye CV kuna watu maarufu duniani leo hii ambao wamefanya mambo makubwa sana katika jamii yetu na yenye maana sana na hata mengine yamewezesha mimi na wewe tuweze kuchangia mwawazo yetu na maoni mbalimbali leo hapa. Mfano Bill Gate aliwahi kushindwa sehemu fulani katika MCHAKATO wa elimu na aka( drop class). Hebu tuwapime watu kwa uwezo wao na mchango wao katika kuleta maendeleo katika jamii na si vinginevyo. Kuna watu wanajiita wamesoma sana wana GPA za nguvu, ni ma dokta, Professa na kadhalika. Lakini hawana maana yoyote katika jamii elimu yao ni sawa na zero kwani haina Impact yoyote kwenye jamii na pengine wamechangia kudidimiza jamii. Maoni yangu ni kwamba jambo lolote la maana ambalo hawa wamefanya au watafanya katika kubadili jamii maskini ya watanzania ndiyo kinatakiwa hapa na si vinginevyo lakini kama unataka kuandika porojo unaidanganya nafsi yako.