Hadi tunakwenda mitamboni hukuendelea tena kutiririka
Baada ya kuchangamshwa na hekaheka za machinjioni na kupata ujanja kidogo wa maisha ya mjini, ujio wa vyama vingi ulimpa chati sana Lusinde miongoni mwa wagogo wanaojishughulisha na shughuli za minadani na machinjio. Alikuwa msitari wa mbele kuunga mkono vyama vingi na kuhamasisha wagogo wenzie kujiunga na vyama vipya. Amepitia vyama kadhaa na ilipofika mwanzoni mwa mwaka 2005 alikwenda kwao mvumi na kuzunguka vijiji vyote vya kata hiyo kuhamasisha wananchi kujiunga na vyama vya upinzani huku akiweka wazi nia yake kugombea ubunge jimbo la mtera kupitia chadema ifikapo oktoba 2005. Baada ya mzee malecela kuona tishio la dhahiri la kupoteza kiti chake cha ubunge kwa mkamua utumbo huyu, alimwita mama yake Lusinde aishiye kijijini hapo Mvumi na kumtaka amkutanishe na mwanae. Walipoonana Malecela alimtaka Lusinde ahamie ccm kama kweli ana nia ya kuwa mbunge wa jimbo hilo na pia aahirishe nia yake ya kugombea ubunge mwaka huo wa 2005 na badala yake ajiandae kwa 2010 ambapo aliahidiwa msaada wa kifedha na kila hali kutoka kwa malecela ambaye aliahidi kutogombea tena 2010. Itaendelea...