CV ya Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu (Mr II)

Amesoma O-level miaka miwili (2), na amewahi fanya kazi kama 'celebrity'!

LOL!, like....seriously people!, hii kaandikiwa au kaandika mwenyewe? somehow I believe cause stuff he posts on his FB page are mind boggling most of the times, for him as MP??!!!, ama kweli hii ndo TANZANIA!
 
Wanaotetea vilaza kuwa bungeni hawana tofauti na wasaliti wa taifa letu,ikumbukwe tumewachagua wabunge wetu wawe wawakilishi bora katika kutetea maslahi ya watanzania na nchi yetu,kupitisha sheria kuikosoa serikali.Sasa kama kiongozi hana elimu ya ujuzi wa masuala husika tunajenga taifa la aina gani? Bunge sio kupiga meza kunga mkono,kuzomea na kuropoka maneno ya hovyo hovyo nilitegemea kama great thinker kuwashauri viongozi aina Sugu kujiendeleza kielimu kwa faida yao na wanaowaongoza.SHULE NI MUHIMU...
 

mkuu huyu na mbunge wa moro mbona anazdiwa sana tu, 85% ya wabunge wa chadema hawana shule.
 
mkuu huyu na mbunge wa moro mbona anazdiwa sana tu, 85% ya wabunge wa chadema hawana shule.
Ndio maana pro CDM wanatetea upuuzi huu ,tegemeo lao(msomi) ni Dr Slaa tu,Mbowe ndio wale wale wenye elimu ya ngedere ya kudandia miti.
 
mkuu huyu na mbunge wa moro mbona anazdiwa sana tu, 85% ya wabunge wa chadema hawana shule.

Mi nafikiri mabadiliko yaanzie kwenye katiba za vyama na hata ya nchi kwa ujumla. kama katiba inasema kuwa mtu yeyote mwenye umri wa miaka kuanzia kumi na nane na kuendelea ili mradi awe anajua kusoma na kuandika anaweza kuwa mbunge utamlaumu vipi mbunge aliyeishia darasa la saba au kidato cha nne? hata hivyo kuwa na elimu kubwa haimfanyi mbunge kuwa active ila inasaidia kuongeza wigo wa kufikiri na kuchanganua mambo so kama kwa ushauri si mbaya kumshauri mbunge wetu akaongeze elimu ila cyo kumtuhumu yy kama yeye as we are not in a position to judge them
 
Hello,ni post yangu ya kwanza. Naungana na member wenzangu, kuwa utayari na utashi unaotoka ndani ya moyo ni kitu muhimu sana katika kuongoza harakati za mapinduzi yeyote.hasa ktk nchi kama yetu ambayo mifumo tuliyonayo imetufikisha tulipo.so mh sugu kwa kiwango cha elimu aliyonayo ni mwanzo mzuri wa kuanza nao ktkt harakati alizonazo kama kiongozi,yaani huo UBUNGE.Bt kutokana na usasa na mifumuko ya kiteknologia tuliyo nayo hana budi kusogea mbele zaidi kielimu
 
Ndio maana pro CDM wanatetea upuuzi huu ,tegemeo lao(msomi) ni Dr Slaa tu,Mbowe ndio wale wale wenye elimu ya ngedere ya kudandia miti.

Usiwe na mawazo mgando kiasi hicho, hivi ukifanya performance evaluation kati ya fIV sugu na Havard University graduate Mr.Andrew CHENGE nani ata-score USIWE kilaza hivyo elimu ni zaidi katika technical issues ndiyo taaluma it is a must but with uwakilishi wa wananchi ni uadilifu na uzalendo ndiyo credit, tafadhali muacheni MR.SUGU awakilishe wana mbeya, watu wa taaluma watafanya mambo technical sugu haihitaji hilo yeye anasemea wananchi tu. Akiwa muadilifu yatosha
 
watanzania kwa kupenda Education qualifications... dunia ilishatoka huko 1800 back nyie ndio mnaona hiyo ndio CV... shame on you!
 
Sikujua Kama Mh Sugu alishawahi kuwa Security Officer (Mlinzi) wa BP. Big up Mheshimiwa kwa kuthubutu (Kutoka kuwa Mlinzi ...self employed celebrity mpaka UbuNGE).
 

Thanda usipate tabu hizi hapa:
 
Naona hujatambua kwamba Sugu hajapewa ubunge kama msomi bali kama mwanamuziki na mtu aliye na mvuto kwa jamii.

We mtu mpaka kajaza kazi yake "celebrity" hujanywea tu?

The guy has ten albums and pioneered a social movement, cut him some slack and if you want to criticize him, focus on his work. Not the paltry schooling which he had the honor of not faking he prioritized, unlike some usurpers I know.
 

Kwahiyo hakuna haja ya kwenda shuleeeeee mmh. I see
 
Tuache unafiki wala ushabiki wa siasa. Elimu ni muhimu sana katika kuleta chachu ya maendeleo kwenye familia na jamii kwa ujumla. Mbunge hata kidato cha nne hajamaliza? This is shame... Let us call spade spade na sivinginevyo.
 
Nakuunga mkono Mkuu, Enzi za Mwalimu wasomi walikuwa si wengi hivyo katiba ikapendekeza kuwa unaweza kuwa mbunge kwa elimu hiyo ndogo tu. Sasa hivi nchi imekuwa na wasomi wengi, hivyo ni wakati muafaka kwa sheria hiyo kubadilika. Wabunge wana kazi kubwa sana kwenye maendeleo ya nchi yetu hivyo inabidi wawe na elimu ambayo wanaweza kuchambua kwa umakini na kina siyo kwa kukurupuka tu.

Elimu ya degree moja si kubwa viiiile, ila angalau inampanua mtu mawazo jinsi ya kujieleza na kuchambua mambo kwa kiasi fulani. Wabunge wengi ukiwasikiliza kwa kweli ni aibu, kiswahili kingekuwa moja ya lugha kubwa duniani ingekuwa aibu kwa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…