Slaa ajitetea kuhusu elimu yake. Jionee mwenyewe
By Dr.W.Slaa :
Ndahani,
Ni haki Yao kujadili. Msiwapuuze
wala kuwakatisha tamaa kujadili.
Inawezekana kweli wapo ambao
kwa nia njema hawajui mfumo wa
Elimu wa Kanisa Katoliki ambao tok
a Seminary Ndogo ( Form 1-V1)
nimepitia Dungunyi Seminary and
Itaga Seminary of which am very
proud na ninatoa shukrani za dhati
kabisa kwa waalimu wangu wote si
tu kwa kunipa elimu bora, Bali pia
kwa kunipa misingi imara ya malezi
( formation) kwani elimu bora ni
zaidi ya vyeti.
Aidha si wengi wanaojua
Philosophia hasa wanafundisha nini.
Kwa bahati mbaya kuna watu
wanadhani wameelimika na kuwa
mavuvuzela kumbe hawajui kitu,
ndio maana ya msemo " nusu elimu
ni hatari sana". Kuna watu Leo
ukiwaambia kuwa masomo ya
philosophia( falsafa) yanahusu
subjects muhimu Kama 1) Ethics 2)
Logic 3)Epistemology 4) Cosmology
5) Metaphysics 6) Psychology na
philosophy yenyewe yaani misingi
ya philosophy hawaelewi
unazungumzia nini na si kosa lao.
Kuhoji is not an issue, issue ni je
anayehoji anahitaji kujifunza au
anahoji kwa ushabiki tu! This is the
issue at stake!
Wako watu wanafikiria Seminary
Kuu unajifunza Theolojia ( Tauhidi).
Hawajui kabisa kuwa miaka 5 ya
masomo ya Theolojia ni pamoja na
complete course on Sociology,
Anthropology, Oratory,miezi Sita ya
mwisho nilipata complete course ya
ukunga kwa kuwa ukiwaambia
Padre vijijini wewe pia ni
ambalance, hivyo lazima ujue
basics za kumhudumia mama
mjamzito unayemkimbiza hospital
ini na kadhalika. Msomi yeyote,
kabla ya kuhukumu anaanza kwa
kutafuta ukweli juu ya jambo na
kufanya utafiti. Prospectus ya
Seminary Kuu ambazo ziko affiliated
kwa vyuo vikuu mbalimbali duniani
zinapatikana, hivyo hakuna msingi
wa mtu kufanya guess work, labda
awe tu na sababu zake na au
agenda yake ambayo nintofauti na
lengo la elimu ambayo ni kutafuta
"full truth" ambayo nayo ni msingi
wa Somo la Epistemology katika
masomo ya Philosophy(Fals-afa).
Katika Vyuo vikuu, ikiwa ni pamoja
na Chuo Kikuu cha Urbaniana
( Roma) nilikosoma Mimi, pamoja na
miaka 7 ya Seminary Kuu
nilizosoma (Kibosho Major
Seminary/ Moshi na Kipalapala
Major Seminary ambazo zilikuwa
affiliated kwa Kwa Makerere
University na Ndiyo maana vyetu
vyangu ni vya Makerere University
na Urbaniana Pontifical University
Rome, 1) Nilianza na Bacclaureate
( equivalent ya BA) na kuandika
Paper baada ya Course Work, na
Licentiate ( Masters) nayo
nikaiandikia Paper na kufaulu, ndipo
nikaruhusiwa kuendelea na JCD).
2) Napennda pia kuwafahamisha
kuwa wengi kwa kutokuelewa
wanafikiria kuwa JCD inafundisha tu
Canon Law. Pamoja na Canon Law
masomo mengine ni 1) Civic Law
( ambayo ni msingi wa sheria zote
inayotokana na Roman Law), 2)
Family Law( ikumbukwe Kanisa
Katoliki ina mfumo kamili wa ki
mahakama kuanzia Courts of First
Instance hadi court of Appeal
( Sacred Rota) na Supreme Court
( signature Apostolica). Huu ni
mfumo kamili wa ki mahakama,
kwa kawaida ukijishughulish-a na
maswala yote ya ndoa,na
Patrimony. 3) Jurisprudence 4)
comparative Law French,
Commonwealth, American, Russian
kwa maana nyingine all major Legal
Systems worldwide. 5) International
Law na branches zake zote. 6)
Principles of criminal Law
( elements ambazo haiku kwenye
Comparative Law na Civic Law.
Ili kufanya Desertation yangu,
nilipaswa kujifunza Lugha 5 ( nje ya
Kiingereza ambayo kwa wanafunzi
wa English Speaking Countries
inahesabiwa kuwa Mother Tongue,
Latin ambayo kwa aliyetoka
Seminary Kama nilivyopitia Mimi
inahesabiwa Kama original
language, na Hebrew ambayo pia
kwa mtu aliyepitia Seminary it was
taken as on Original language, japo
Mimi sikuwahi kujifunza Hebrew
Seminarini). Hivyo nikachagua a)Ki
Italiano ambayo pia ndiyo ilikuwa
Mwdium of Instruction yaani lugha
ya kufundishia,b) Kijerumani
c)French d) Spanish na e)
Portuguese. Hata hivyo focus yangu
ilikuwa kwa Italian na German na
mengine matte nilijifunza kuweza
kufanya research yangu, na
kuniwezesha kusoma lakini Siko
fluent katika kuzungumza.Hii pia ni
kutokana na muda mfupi. Nilipata
course ya Wiki 3 tu ya kujifunza
Lugha kabla sijaingia darasani kwa
masomo proper.
Nimeyaweka kwa uwazi, na
ninadhani wako wanaofahamu
mfumo wa masomo katika vyuo vya
Kanisa Katoliki wanaweza kujazia.
Wako ambao tumesoma nao was
mapadre katika Pontifical
Universities za Rome, Leo
wanashika nafasi kubwa katika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania au nafasi zinging
mbalimbali kwenye Taasisi
mbalimbali. Kwa kuwa nilienda
Roma nikiwa tayari Mkurugenzi wa
Maendeleo Jimbo Katoliki la Mbulu,
nikawa Nina shuttle Kati ya
Pontifical University ya Urbaniana
na Pontifical University ya St.
Thomas Aquinas, Rome ambako
nilisomea Advance Diploma ya Rural
Development.
Nadhani sasa mnaweza kupima
kwa vigezo hivi hoja za mleta
thread hii. Mnaweza kupima nini ni
puma na nini ni mchele. Mnaweza
pia objectively kuangalia depth ya
masomo kwa kulinganisha na
propaganda nyingi zinazopigwa kwa
malengo tu ya upotoshwaji na au
Propaganda. Vyuo vikuu Biko
kwenye mitandao, mleta thread na
wengine wa aina yake wakijisumbua
kidogo tu kuingia kwenye Google
watapata ukweli bila kutafuniwa na
mtu. Tuweke uvivu wa kufikiri
pembeni tunapojadili mambo
makubwa na mazito. Nafasi ya kila
mmoja kujipatia Elimu bora ipo
Kama watu tutakubali kujisumbua na
kuacha uvivu wa kufikiri. Nchi
haitaendelea kwa propaganda na
otoshwaji, Taifa halitaendelea kwa
wivu....shika Kitabu. Soma.
Jichimbie utavuna lakini Kama
utakesha kwenye mitandao kufanya
Propaganda badala ya kuchota
elimu bora tena ya bure kwenye
mitandao utaachwa unajiozea!
Nawahimiza wote wenye kupenda
Taifa lao kujichimbia. Innovation ni
msingi wa maendelo na Innovation
haipatikani kwa majungu na umbeya
inapatikana kwa wanaochimbia
vichwa vyao kwenye utafiti,
kujisomea na kujiendeleza. Tupende
Taifa letu, uzalendo uwe kwa
matendo na sio Maneno matupu.
Dr Slaa, kwa kuchangia hii mada, ngoja nianzie mwanzo kabisa ya masomo ya upadre.
1. Baada ya Form VI na baada ya kuwa umepitia national service na umepata Division I au II (masomo ya Arts) & III (masomo ya Science) kwa mfumo ninaoufahamu mimi: aliyeomba kufanya malezi ya upadre alisoma yafuatayo:
a) Philosophy (zamani ilikuwa miaka 2, lakini sasa hivi ni miaka 3): katika philosophy kuna masomo yasiyopungua yafuatayo:
i) A history of philosphy: yaani kuanzia poets karne ya 7 BC, then cosmologists (karne ya 5 hivi BC) hadi cotemporary philosphers na African philosphers. African philosophers ni pamoja na Nkhruma, Mandela, Kaunda, Jomo Kenyatta, Nyerere, Senghor, nk. Kwa idadi ni zaidi ya wanafalsafa 200 hivi (walizaliwa wapi, walisoma wapi au hawakusoma, walifanya nini hadi mwisho wa maisha yao).
ii) Systematic philosophy:
. Logic - formal logic
- material logic
. Natural philosophy:
- philosophy of nature
. Social sciences ( modern science, scientific revolutions, physical sciences, space and time, evolution, etc)
. Anthropology (social and cultural anthropology)
. Political philosophy (+ political science) [The state, the notion of state, elements of state & law, international law, just war, forms of government, separtion of powers, jurisprudence, natural law, positivism, civil law etc]
. Philosophy of language (lingustics, semantics, hermeneutics, art, poetics, aesthetics)
. Psychology
. Metaphysics/ontology (philosophy of being)
. Epistemology (philosophy of knowledge: how do we know? what do we know? What's the meaning of doubt, question, suspicion etc)
. Natural theology (not the same as theology)
. Philosophical Ethics
. Church History
. Moral dilemmas: what's the morality of genetic engineering, HIV/Aids, homosexuality, premarital intercourse, just war, civil disobedience, human cloning, prostitution, masturbation, celibacy, abortion, pollution, rape, sexual abuse, family planning, murder, euthanasia (mercy killing), suicide, genital mutilation, strikes, unemployment, alcoholism, addiction, drug abuse, workholism?
2. Baada ya hii dose wale wa jimbo wanaenda mwaka mmoja mmoja wa pastoral experience. Wale wa mashirika wanaenda mwaka mmoja wa spiritual theology na kisha mwaka mmoja au miwili ya practical experience (jumla mika 3). Tofauti ni kwamba: watakaojiunga na jimbo watafanya kazi ndani ya jimbo wanalotoka au nchini na wale wa mashirika wanaandaliwa (kwa kawaida kufanya kazi nje ya nchi yao ya kuzaliwa ingawa baada ya muda fulani huwa wanarudi kutumikia nyumbani kablya ya kurudi tena kuendelea na utume wao. Siku hizi hata mapadre wa jimbo wanaweza kuombwa kufanya kazi nje ya jimbo au nchi yao na hivyo inabidi pamoja na mambo mengine wajifunze lugha na mila za kule wanakoenda kufanya kazi. Baada ya kipindi hiki wanarudi tena shule.
b. Theology (miaka 3 au 4 kulingana mfumo wa masomo ya chuo husika):
. Introduction to Canon Law and Marriage
. Moral theology
. Sexual Ethics
. Christology
. Pauline theology and Catholic Epistles
. World Religions (Christianity, Islam, African Traditional Religions, Shintoism, Hinduism, Budhism etc)
. Christian Anthropology
. Counselling
. Sacramental theology (including care for the sick)
. Liturgy (including public speaking/good communication)
. Inculturation (understanding surrounding cultural settings)
NB: Masomo yote haya ni kwa level ya basic priestly training kabla ya kufanya specialisation (MA, PhD etc). Kwa kawaida, wanafunzi wa masomo ya upadre haombi kuendelea na masomo ya juu kwa level ya MA au PhD, bali anapendekezwa kulingana na performance yake toka seminari ndogo (minor seminary)/sekondari hadi seminari kuu (major seminary). Mara nyingi wale wanaopata zaidi ya wastani wa 75% na vyuo vingine zaidi ya 85% ndio wanaopendekezwa kuendelea na masomo ya juu.
3. Kama Dr Slaa anavyosema, mara nyingi wanaohaji ni wale wasiojua au kama wanajua wanataka kuleta majungu kwa sababu ya chuki zao binafsi (huenda chuki za kidini au kisiasa). Kwa maoni yangu, ni kukosa uelewa mtu kuhoji usomi wa Dr Slaa. Kuhoji huku ni sawa na "unthinking intelligence" maana vyuo vyote vya malezi ya upadre vilivyo chini ya Kanisa Katoliki vinafuata sylabus ileile ulimwunguni kote na requirements ni zile za chuo kikuu na siyo tu chuo kikuu bali vyuo vinavyokubalika kimataifa na viwe vinakubalika pia kwa viwango vya Kanisa Katoliki. Mfano, mtu akisoma UDSM philosophy, kwa mfumo wa Kanisa Katoliki mtu huyo hajasoma philosophy na hivyo akijiunga na chuo cha Kanisa Katoliki ili asome philosophy anaanza upya. Vilevile kama mtu amesoma Tumaini University theology na akajiunga na malezi ya upadre lazima aanze upya masomo ya theology. Hii ni kwa sababu kwa mfumo wa Kanisa Katoliki haya masomo yanafundishwa kwa undani zaidi na ndiyo maana miaka ni mingi ili kumjengea mwanafunzi uwezi na uelewa mzuri wa masomo anayoyasoma. Mfano, mwanafunzi akijiunga na UDSM anaweza akasoma philosophy kwa muhula mmoja lakini kwa mfumo wa Kanisa Katoliki basic philosophy inasomwa si chini ya miaka mitatu.